Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Wapelekeni mahakamani na sio kutuletea ngojera za majungu na siasa za chuki. Acheni kuchafua watu kwa maslahi yenu maovu.
 
tatizo lililo karibu sana na wewe ndiyo mlango wa tatizo lako ,,,,,,,,maisha yako ni kile unachopenda kukukmbuka

naona mkuu amekumbuka ,natarajia na wengine wasiojulikana , kwa hili la nyalandu watakumbuka na tutajua mengi , hongera psychology
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania??

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi?????? Aibu kubwa hii.....

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Huwezi kutukana watu majizi bila kuwachukulia hatua za kisheria, kisha unataja watanzania wenzangu Ina maana hao majizi siyo miongoni mwa hao watt wenzako,
 
Chadema ni chaka salama la majizi na sasa majangili
Watu na akili za ajabu sana, hivi wezi wakihamia chadema au chama chochote kuna sheria inazuia au wanakuwa na kinga ya kushitakiwa? Nategemea kwa matamko haya ya Rais wote wanaotajwa wakamatwe na kufikishwa mahaakamani, vingenevyo ni shida!
 
bado kawakumbatia majizi wengine chungu nzima. Sijui anataka kumdanganya nani huyu!!?
upload_2017-6-13_14-5-10-jpeg.621879
 
Mikutano ya kisiasa ni haki yao ya kikatiba
Haki yyt inatakiwa iendane na wajibu. Je unafikiri kwa kauli zinazotolewa na wapinzan zinaakisi UZALENDO DHIDI YA SERIKALI NA NCHI YAO?Wengi wanadai haki lkn wajibu hawajui uko vipi.Kila mtu anahaki ya kutoa maoni bila kuingiliwa na mtu yyt.lkn je nini wajibu wake ktk kutoa maoni?Je anatimza wajibu wa kulinda heshima ya mtu?Je anatimiza wajibu wa kuhakikisha haleti sintofaham ktk jamii?Mtu anaulizwa nini kazi za chama cha UPINZANI anajibu ni kuwachochea wananchi waione SERIKALI yao haifai,kweli?Kiongoz kama huyu anadai haki ya mikutano ya kisiasa.

Kingine Mbunge kachaguliwa awatetee wananchi wa Jimbo lake lkn pia anaweza kuwatetea wananchi nje ya Jimbo lake.Mbunge jimbo lake la kawe linashida tele,badala ya kupambana awasaidie yy analilia kwenda kufanya mkutano mbeya. Ni vitu vya ajabu.Kwanini kila mbunge asisimame kwenye Jimbo lake kila siku apaze sauti kuwapigania wananchi wake na kushirikiana ktk kutatua changamoto zaid anataka aende Arusha akafanye siasa?Kuna mattz yanahitaji utashi wa mbunge na wananchi ili kuyatatua,kwanini hawafanyi hivo kila siku wako DAR kukimbizana na POLISI?Shule haina choo,mbunge anahimiza kila mwananchi aje na tofari mbili kwa ajili ya ujenzi,inashindikana nn?Au hapo panahitaji uende kwenye majukwaa ndio upige kelele?

Yako mengi sana.mimi naona wanaolilia mikutano ya kisiasa hawana hoja za mcng ktk kumkomboa mtanzania zaid ya kujinufaisha wao kisiasa. Umeambiwa piga siasa kwenye Jimbo lako,we hutak unataka uende kwenye Jimbo la mwenzio. Kwamba Jimbo lako mattz hamna?Kwamba Jimbo lako huwezi kusikilizwa au sababu ya mcng mbunge kulilia kupiga siasa kwenye Jimbo la mwenzie ni nn?
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania??

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi?????? Aibu kubwa hii.....

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Inawezekana kweli kuna majizi yamehamia CDM, lakini yeye ndo mwenye dola kwa nini asiyashughulikie hayo majizi. Pili kama alivyosema yametokea CCM lakini Raisi wetu mpenzi amesahau kuna kuna ambayo yako kule CCM bado sijui hayo atayafanya nini? CCM oye. Hayo tisa, bado sijamsikia anafanya nini ili CCM yake ikome kuwa mtambo wa kuzalisha majizi na mafisadi na kuwalinda maana kasema yeye hafukui makaburi. CCM oyeeeeeeee.
 
Bro si swala la chama, nazungumzia kauli ya Rais na mamlaka yake, kuwataja wezi anaowajua na kutokamatwa, ni tofauti sana na wengine achalia mbali chama fulani, Rais ana idara zote zinazodeal na wezi, serikali haina sababu ya kulialia kwa wananchi juu ya wezi wanaohama vyama, swala ni kuwakamata na kufikishwa mahakamani, vinginevyo hatupambani na wizi huu, wakiwa ndani ya chama tawala kimya, wakaitoka tu majizi, kweli?
 
Rais Magufuli amesema yalikuwapo majizi CCM kuliko hata ya Chadema na wengine wametoka kwenye chama hicho tawala na kukimbilia chama hicho cha upinzani.

Alisema pia kuwa wapo waliopo Chama cha Wananchi (CUF) wengine ni wabaya sana.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Mkuyuni jijini Mwanza.

“Ndiyo maana tumeamua kuijenga reli ya umeme na sio ya kuendeshwa na dizeli kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma kwa fedha za ndani za Watanzania Sh trilioni 7, nataka niwaambie kwamba hata kama itachukua miaka 10 itafika Mwanza na speed (mwendo kasi) yake ni kilomita 160 kwa saa.

“Tunataka Tanzania mpya, hilo ndiyo lengo langu na ndiyo maana nilipofika hapa sikusema CCM oyee kwa sababu yapo yaliyokuwepo CCM yalikuwa majizi sana kuliko hata ya Chadema.

“Ndiyo maana mimi niko hapa sijasema Chadema oyee, kwa sababu yalikuwepo majizi CCM yakakimbilia Chadema, ndiyo maana sijasema CUF oyee, kwa sababu wapo waliopo CUF wengine ni wabaya sana, mimi nataka maendeleo, nasema Tanzania oyee, kwa sababu Tanzania inatakiwa kujengwa na Watanzania,” alisema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alishangazwa na kutokuwapo na hata kiwanda cha drip, mabomba ya sindano na pampas hapa nchini, huku vyote vikiagizwa kutoka mataifa mengine.

“Hata mimi mwenyewe najua kutengeneza maji ya drip, wanafunzi wa chuo waliosoma kemia kwa kidato cha nne na sita wanajua kutengeneza, kwanini tusitengeneze maji ya drip badala yake tunanunua Uganda? Tunashindwaje kuwatumia wanafunzi au wahitimu wa kemia kutengeneza?” alihoji.

Pia alitoa angalizo kwa mwekezaji wa Kiwanda cha nguo cha Mwatex kilichopo Mwanza, kuhakikisha kinaongeza uzalishaji na kuacha visingizio na kama ameshindwa ni vema kukiachia ili kukabidhiwa mtu mwingine.

Rais Magufuli alionyesha pia kushangazwa na mwekezaji wa kiwanda hicho, kupewa kingine Mbeya na sasa hakifanyi kazi ipasavyo.

Aunga Mkono Juhudi za Wananchi
Akiwa kiwandani hapo, Rais Magufuli alitoa Sh milioni tatu kwa lengo la kununulia mifuko 100 ya saruji kwa shule mbili zilizopo ndani ya kata hiyo.

Rais Magufuli alimkabidhi fedha Diwani wa Kata ya Igogo, John Minja, akiunga mkono juhudi za wananchi wa kata hiyo katika kuboresha miundombinu.

Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, alimweleza Rais Magufuli kuwa wananchi wa kata hiyo wamechanga Sh milioni 15.8 kujenga matundu ya vyoo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwa aliwahi kuishi ndani ya kata hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda cha Victoria Moulders & Polybags, Manjist Singh, alisema bidhaa zinazozalishwa hapo zinauzwa Uganda, Rwanda, Burundi na ndani ya nchi na kuongeza kuwa alikianzisha kutokana na uwepo wa shughuli za kilimo na madini.

Hata hivyo, aliomba Serikali kupunguza matatizo yaliyopo soko la ndani kwa kuondoa utegemezi wa bidhaa za nje kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji wa ndani.
 
Kazi yake kulaumu tu,kusimanga na kusutana ila utekelezaji wa ufungaji wa mafisadi na majizi!

What an empty talker!
 
Back
Top Bottom