Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,997
- 3,933
- Thread starter
- #61
Tumemsikia wenyewe Rais wetu, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, alipokuwa akitengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, akitoa sababu kuwa ni kutokana na waziri huyo kusaini mkataba nje ya nchi, wa kuingiza vifaa vya zimamoto, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja
Kama madai ya Rais Magufuli ni ya kweli, ni kwanini Jeshi la Polisi nchini halijamkamata Mheshimiwa Lugola na kumfungulia mashitaka ya utakatishaji wa pesa nyingi kiasi hicho?
Tunajua kuwa yupo mwandishi wa habari, Eric Kabendera, anayeendelea kusota rumande, kwa zaidi ya miezi 6 sasa, kwa tuhuma za utakatishaji pesa wa shilingi milioni 170
Tunajua pia yule mfanyakazi wa kituo cha haki za binadamu, Tito Magoti, naye amefunguliwa mashitaka ya utakatishaji pesa wa shilingi milioni 17 pekee!
Inakuwaje kwa hawa akina Lugola, ambapo kwa Maelezo ya Rais wetu Magufuli, amewatuhumu kushiriki kusaini mkataba wa kununua vifaa vya thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja, waeendelee kukaa uraiani, ambapo Rais mwenyewe ametuhakikishia kuwa wanahusika na utakatishaji pesa wa zaidi ya shilingi trillion moja?
Hivi ni kipi kikubwa ni trillion moja ya Kangi Lugola au shilingi milioni 17 za Tito Magoti?
Kama Kangi Lugola hajafunguliwa kesi ya utakatishaji pesa basi tutajua kuwa hili suala ni la kisiasa
Tusaidiane katika kulidadavua suala hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu
Kuna Maswali mengi sana nyuma ya Pazia.
Naomba kusema wazi ; Mimi ni miongoni mwa Muumini wa Juhudi za Maguful; kiukweli anajitahidi Kwenye baadhi ya mambo.
Lakini namna ya Uongozi wa Magufuli mpaka leo nimeshindwa ku define leadership style ya Gufuli.
1 Anatuelezea sana matatizo badala ya kutupa majibu na solution.
2. Katika tumbua tumbua zake; hakuna hata mmoja aliyewajibika au kuwajibishwa kisheria hata upige Billions of Money
3 .Nyuma ya ishu ya Kangi kuna maswali mengi kuliko majibu.
The whole thing ya Kangi Lugola won’t make any sense until he has brought forth to the law.
Otherwise this is another Customer Retention. Yaani you treat Diabetes you end up in BP; now you will have to deal with Diabetes and BP —Business as Usual