Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Kangi Lugola aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya ndani, alikuwa anaonesha uzalendo wake kwa kuvaa shati lililonakshiwa kwenye mifuko na bendera ya Taifa! Huku akitembea muda wote na kitabu cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwingine alijinasibu uzalendo kwa kuvaa tai yenye rangi za Bendera ya Taifa karibia muda wote.
Nina hakika wawili hawa hawajawahi kukutana na maswali ya moja kwa moja yanayohitaji majibu ya kikatiba, nukuu na vifungu vyake! Walijinasibu uzalendo kwa sababu ya tumbo!
Asilimia 95 ya watendaji kwenye mamlaka zetu hawajawahi kuisoma Katiba, hawaijui, na hawaifuati na hapa ni pamoja na Kiti chenyewe. Wanaweza na kujua ni wakati tu ule wa kukishika kitabu kidogo cha Katiba wakati wa kuapa.
Wanaoijua Katiba, kuisoma, kuichambua na kuitumia katika maisha ya kila siku ni wananchi wachache walioko nje ya mfumo wa kaliba mbalimbali, wasomi na wanasheria pamoja na wazee wachache wastaafu waliobaki.
Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji karibia wote wakusanye leo uwape mtihani rahisi wa maswali machache ya Katiba ujionee maajabu ya Dunia kwa alama watakazopata, na hii ni pamoja na kiti chenyewe!
Matamshi ya kuita Katiba ni makaratasi tu yanaangazia tatizo kubwa mbleni kuliko tunavyodhani.
Eeh Mungu isaidie Tanganyika iweze kuvuka salama.