Rais Magufuli, hili la Kangi Lugola hujatenda haki. Sheria ya Uhujumu Uchumi inawahusu wananchi tu?

hata kwa huo muda aliokaa kama waziri ni mrefu sana kwani ulijaa;
kujipendekeza (hadi anamsifia mwanadamu mwenzie kuliko Mola wake aliyemuumba)
Ulimbukeni
kuchongea wenzie ( hasa wizarani kwake)
Acheni Mungu aitwe Mungu, BALI kikombe ulichokuwa unawanywesha wenzio sasa ni muda wako kukinywea na kamwe hutakiepuka!
 
Binafsi naona tunapigwa changa la macho

Inafahamika vibali vya kusafiri nje ya nchi hutolewa na Ikulu,je wakati ikulu inatoa kibali kwa Kangi na kundi lake waliwauliza wanaenda kufanya nini? Ni wazi lazima waliulizwa, Lugola hawezi kutoka nje ya nchi kwenda Romania bila kibali cha bosi wake!

Je ni kweli MKATABA huo ulikuwa haufahamiki mahala popote? ikiwemo ikulu? Hapana, je mpaka Lugola anaenda nje ya nchi, kamati ya makatibu wakuu,kamati ya wataalamu,wizara ya fedha,si walishaupitia mkataba au? Na je si Baraza la Mawaziri lazima lijue kuhusu MKATABA huo? Hayo mambo ya hovyo yalipitaje?
 
DPP WETU mtamchoshaaa mwakaa huuu uwiii
Mungunakupe nguvu DPP WETU mzigoo mwingine HUO unakujaaa
 
Kuna kitu kingine cha kujiuliza, mikataba ya serikali pia haisainiwi bila ushauri wa kisheria ambao hutolewa na ofisi ya mwanasheri wa serikali.

Mbona hatukusikia waziri wa katiba na sheria au mwanasheria mkuu wa serikali akiingizwa kwenye hii inayo itwa kashfa?

Walio toa vibali vya maofisa kusafiri mbona nao wana kula bata?

Mh Rais kuna nyakati huwa anatuingiza chaka bwana.
 
Tumemsikia rais akisema kuwa wizara ya mambo ya ndani inampasua kichwa kwelikweli.

Akatoka hapo akawa muwazi kwa wananchi kuwa watu wamesaini mkataba wa shilingi trilion 1 bila kufuata sheria za nchi yaani kupitiwa na bunge.

Rais akatoka hapo akatueleza kuwa hata mkataba wenyewe ni feki, maana hata serikali ikijitoa bado zile sehemu ambazo zineanza kutekelezwa lazima zitekelezwe.

Hivi karibuni kumekuwa na kawaida ya kuwaweka ndani kwa makosa ya pesa yaani Uhujumu uchumi au money laundering, Tena wakati mwingine pesa zenyewe zinazotajwa kwenye mashitaka ni vimilioni vichache.

Leo watu wamesaini mkataba mbovu wa Matrlioni ya shilingi. HIVI HAWA UNAWAACHAJE ACHAJE URAIANI KWA MFANO?

Honestly, Kama wapigaji wakubwa wa namna hii kazi yao ni kuandika barua ya kujiuzulu tu baada ya kufanya magumashi halafu wanaendelea kuwa huru then harakati zote za kutuaminisha kuwa serikali hii inapambana na vitendo vya uhujumu uchumi ni Usanii.

Kama ingekuwa China, Yaani Lugola na Andengenye wangekuwa tayari korokoroni wakisubiri kesi. Lakini huku kwetu mtu anaandika barua, anajiuzulu tu, kisha anaendelea kusubiri mafao yake na mwingine anaenda kurudi bungeni kula na kulipwa mshahara kwa kodi za wananchi. Huu ni usanii

Serikali ya awamu ya Tano ilipaswa watu kama hawa ndo wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi, siyo vijana wale wanaharakati akina Ngetti au muandishi wa habari ndugu Kabendera.
 
Serikali hii tokea ianze wahujumu uchumi hasa ni wapinzani, wakosoaji, wanahabari, wanaharakati na wafanyabiashara! Hawa viongozi wenye vyeo vya kisiasa kutoka serikalini wakiwa waktumbuliwa tu bila kucukuliwa hatua yoyote!

Kwa hiyo Rushwa inapiganwa upande moja tu huku wanasiasa wenye dhamana wakilindana kwa nafasi zao. TAKUKURU tokea jana walitakiwa wameshawahoji hao watu
 
Nilijiuliza maswali kama hayo jana,moja likuwa hili la kibali cha kusafiri kwenda nje ya nchi.kwa kumbukumbu zangu kibali mpaka mamlaka ya ikulu ukubali kitoke ni ijiridhishe beyond reasonable doubt kwamba safari hiyo ina tija kwa mhusika au kwa taifa...sasa je hili la mikataba kutokuwa na tija kwa taifa hawakuliona au ndio yala yale ya uvivu wa baadhi ya watz kusoma kupitia kilichomo?kuna mushkeli mahala
 
Hatua iliyochukuliwa na rais ni yakupongeza siyo jambo rahisi!! Ilo ndiyo LA muhimu na amesema wengine walohusika mfano ofisi ya mwanasheria mkuu wajitafakari!! Maswali mengine mnayojidai ni yakiuchunguzi hata hayana tija!! Ushaambiwa wamesaini mkataba huko huko ughaibuni na unavipengele vys hovyo!! Mkata viuno kachemsha mwacheni apumzike sasa yule aloshambuliwa sana na Lema keshachukua usukani
 
Tuendelee kuunga mkono kwa dhati jitihada za Mh Rais zakufufuwa uchumi,na tuendelee kukubaliana na Rais anaavyowatumbua Mawaziri,tumpe majina ya mawaziri wengine awatumbuwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitting Allowance dola 800: Halafu still tunasikia hali mtaani ni ngumu, watu hawana hela, kumbe fedha zipo kwa wachache.
Kuna raia wanakula nchi bhana..🤔🤔🤔 wengine wasindikizaji tu.
 
Sikuwah elewa maana ya Kusamehe wahujumu uchumi et kuwataka tu warudishe pesa..



MASIKIN NA MNYONGE , NDIO WANAFUNGWA.
 
Kwani mkataba upi ulioleta shida.
Binafsi naona tunapigwa changa la macho

Inafahamika vibali vya kusafiri nje ya nchi hutolewa na Ikulu,je wakati ikulu inatoa kibali kwa Kangi na kundi lake waliwauliza wanaenda kufanya nini? Ni wazi lazima waliulizwa, Lugola hawezi kutoka nje ya nchi kwenda Romania bila kibali cha bosi wake!

Je ni kweli MKATABA huo ulikuwa haufahamiki mahala popote? ikiwemo ikulu? Hapana, je mpaka Lugola anaenda nje ya nchi, kamati ya makatibu wakuu,kamati ya wataalamu,wizara ya fedha,si walishaupitia mkataba au? Na je si Baraza la Mawaziri lazima lijue kuhusu MKATABA huo? Hayo mambo ya hovyo yalipitaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom