Rais Magufuli aongeza muda kwa usajili wa laini kwa alama za vidole

Kumbe rais naye Airtel! Maskini TTCL!

nyoka hana tako

Mh. Rais baada ya kujisajili atoa sababu za umuhimu wa kila mtu kusajili laini yake, maana hata nchi za ulaya zilizoendelea lazima usajili laini yako ya simu huku ukionesha pasipoti kwa ajili ya usalama, mwisho wa nukuu.

Leo sijaona ulinzi mkali wa wale askari wenye bunduki waziwazi labda Chato ni mahali salama na wananzengo hawahitaji kutishwa.


Source: Global TV online.
 
Hizo siku ishirini nina wasiwasi wataongeza tena, unless hao NIDA watoe vitambulisho/ namba kwa waombaji wote, tena ndani ya siku hizo, hadi wale waliopanga foleni kujiandikisha sasa hivi, na wale watakaokwenda kesho na keshokutwa na.........!!

Sent using Jamii Forums mobile app
...nilidhani ingependeza zaidi kama mheshimiwa angeyaishi maisha ya mwananchi Wa kawaida anayetafuta kuandikisha no take japo kwa masaa Matatu tu kwenye foleni ndio ningemuelewa kidogo!
Lakini hii ya kusajili simu yake akiwa kasafishiwa njia kabisa..?!?...na wakati huku Kibamba mi mzee Wa miaka 60 nimeisha kwenda kujiandikisha Mara ya NNE sasa na kukuta bonge la foleni liliyokwenda shule na ninaishia kukata tamaa tu na kurudi nyumbani?!?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli leo Dec 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwataka Watanzania kusajili laini zao kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na TCRA, JPM ametangaza kuongeza siku 20 kwa ambao hawajakamilisha zoezi hilo.
_
Rais Magufuli amefanya usajili huo wa laini yake kwa alama za vidole Chato, Mkoani Geita ambapo ameongeza siku 20 kuanzia Jan 01, 2020 hadi Jan 20, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia December 31, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.
_
Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya siku 20 alizoongeza kukamilika hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa “usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi, unaepusha uhalifu”
 
Usajili hautakiwi kuwa na mwisho tunawakosea sana vijana ambao kila tarehe wanafikisha miaka 18

iyo tarehe 20 unaweza kuta vijana zaidi ya elf20 wamefkisha miaka 18 kwahyo ukisema mwisho maana yake hakuna mtu mpya ataruhusiwa kusajili line?

Mpaka sasa ivi kuna line ml 16 hazijasajiliwa maana yake kwa siku zilizobaki kama 24 ni wastani wa kusajili line 660,000 kwa siku kitu ambacho ni uongo hakiwezekan kwa mifumo iliyopo.

fanyeni swala liwe endelevu au pelekeni maafisa kila kijiji na kila mtaa.
 
TUNAMSHUKURU MH.RAIS,LAKINI BADO PIA HUO MUDA NI MDOGO MNO,SPEED YA JAMAA WA NIDA NI NDOGO MNO.
#TUNAOMBA AONGEZE MIEZI 3,
#USAJILI WA LINE KWA NJIA ZA KADI YA KITAMBULISHO CHA TAIFA TU NDIO UKUBALIKE.
#WANAOPOTEZA SIMU ZAO IWE NI LAZIMA KUZI RENEW KWA KITAMBULISHO CHA TAIFA.
#GHARAMA ZA AFIDAVITY ZIONDOLEWE KABISA PAMOJA NA AINA ZOTE ZA TOZO NDOGONDOGO ZIFUTWE,KWANI VITAMBULISHO HIVI VIMETENGENEZA DILI TAYARI KWA BAADHI YA WATENDAJI WA NGAZI MBALIMBALI.
#
 
Kama kawaida
Tengeneza tatizo halafu Tatua..

Sasa yule waziri aliyejitutumua kuwa tarehe 31 ni mwisho na serikali haitaongeza siku ataweka wapi sura yake.

Kama vipi iwe Teua Tengua
Unawajua Wanasiasa Wewe??
Wana Roho Ngumu, Sura Chachu
 
Back
Top Bottom