Rais Magufuli aongeza muda kwa usajili wa laini kwa alama za vidole

Mi najiuliza unawezaje kuzifungia laini ambazo hazijasajiliwa laini ambazo hazitambuliki kwenye mfumo labda wafanye makampuni ya simu kitu ambacho kitawakosesha wateja kwahiyo hawataweza.
Laini ambazo zipo kwenye mfumo hizo zilizosajiliwa ndizo unaweza kufanya hivyo ni Kama micro chip akiwa nayo mtu ni rahisi kumtrack kuliko asiye kuwa nayo

Nimewaza tu
 
Vipi hawajamtoza buku hao wahuni ya kusajilia?

Sijui kwa nini yupo soft sana ku-deal na kiini cha tatizo?

Anadanganywa au na yeye ni sehemu ya hilo tatizo?

Hata angeongeza miezi sita kwa NIDA hii hakuna lolote.

Imetuchukua miezi 18 kupata namba pekee na si ID yenyewe!

What do you expect in 20 days?

Hao wagonjwa walioongezewa muda idadi yao ni negligible kwa wasiokuwa na namba ya NIDA.
 
Mzee anatuchanganya kidogo...hapo nyuma yeye alisema line hazitafungiwa mpaka wananchi wote wapate vitambulisho vya NIDA..ameona siku zimekaribia kuisha ameenda kusajili...kisha kaongezea siku ishirini za kusajili...whether una kitambulisho au hauna...whether kuna foleni kubwa na usumbufu NIDA au la....tatizo limetengenezwa tena...na litatatuliwa kwa muundo wa kutengeneza tatizo jingine..


...One has a problem for every solution...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee anatuchanganya kidogo...hapo nyuma yeye alisema line hazitafungiwa mpaka wananchi wote wapate vitambulisho vya NIDA..ameona siku zimekaribia kuisha ameenda kusajili...kisha kaongezea siku ishirini za kusajili...whether una kitambulisho au hauna...whether kuna foleni kubwa na usumbufu NIDA au la....tatizo limetengenezwa tena...na litatatuliwa kwa muundo wa kutengeneza tatizo jingine..


...One has a problem for every solution...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama na hapa ulichanganywa basi unachanganyika kirahisi sana.
 
Hatujui tushike yupi tuache yupi, Lugola alisema serikali ishafikis idadi ya waliotaka hivyo hakuna mwananchi simu yake itazimwa.

Mara mkuu mwenyew kasema hazitazimwa sabab vitambulisho Nida hawajakamilisha zoez nchi nzima mara leo zimetoka siku 20 halafu watazims
 
Zoezi hili ni nyeti sana ukilinganisha na malengo ya serikali ya kuanziahwa kwake. Kinachonisikitisha ni zoezi hili kufanywa na vijana wasio wazalendo ama ni sababu za njaa au la.

Kilichonifanya nilete bandiko hapa, wiki moja iliyopita nilipita njiani nikamkuta kijana anasajili laini za simu. Mimi pia nikaona nisajili laini yangu moja iliyobaki, laini zingine tayari nilikuwa nimeshazisajili, zamu yangu ilipofika yule kijana alianza kunihudumia, alianza akinitaka kutaja namba ya kitambulisho nikafanya hivyo, kisha nikataja namba yangu ya simu baadaye alama za vidole nikaweka, sina uhakika kama mpangilio wa utaratibu ni sahihi, nikaona taratibu hizi ameanza kuzirudia, tena akanipiga picha, hili la kupigwa picha ndiyo lililonishangaza zaidi na kunipa wasiwasi mkubwa.Sababu laini zangu zingine nilizosajili hakukuwa na utaratibu kama huo. Nilimwambia yule kijana kwamba ninawasiwasi na utaratibu anaoutumia kusajili laini za simu na kwamba huenda kitambulisho changu anatumia kusajilia namba ya simu isiyoyakwangu. Yeye akanijibu basi kama ninawasiwasi niende kwa kijana mwingine aliyekuwa jirani yake ambaye pia alikuwa wajisajili laini.

Niliamua kuondoka kuelekea kwenye ofisi za Halotel kwa kuwa nilikuwa mjini niliamini kule wasingeweza kufanya ujanjaunja kama kijana wao alivyotaka kuniingiza mjini, nilipofika nakueleza shida yangu nilianza kusajili laini yangu. Yule msajili Kila akitaka kukamilisha usajili unagoma. Kumbe ile laini yangu ilikuwa imeshasajiliwa tayari na Yule kijana wa kwanza ndipo nikaamini kwamba alikuwa akakamilishia usajili yale mengine aliyotaka kuendelea nayo ilikuwa janjajanja tu. Sijui hizo laini wanazosajili kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine wanazipeleka wapi wasiwasi wangu mkubwa yasijeyakawa yaleyale kama ilivyosasa kabla ya ujio wa wa zoezi la usajili wa laini kwa alama za vidole.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom