Rukwa kinara kwa majaribio ya Utapeli kupitia simu. Dar inaoongoza kwa usajili wa laini yawa ya 3

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Ripoti ya Takwimu za Mawasiliano Tanzania iliyotolewa na TCRA mwezi Septemba, imeonesha Mkoa wa Rukwa umekuwa Kinara wa Majaribio ya Utapeli kupitia simu ikiwa na Majaribio 8,450 kwa kipindi cha Julai hadi Septemba

Hata hivyo kwa mujibu wa Ripoti hiyo, Rukwa inashika nafasi ya 25 kwenye orodha ya Usajili wa Laini za Simu Tanzania ikiwa na idadi ya Laini 1,102,411

Aidha, Dar es Salaam inayoongoza kwa idadi ya Usajili wa Laini za Simu ikiwa na Laini 12,355,089 imekuwa nafasi ya tatu kwa Majaribio ya Utapeli kupitia Simu ikiwa na Majaribio 3,273 kwa Julai hadi Septemba

1698415440012.png


image.png
 
Back
Top Bottom