Rais kutokupokelewa na Rais mwenzake: Tutofautishe kati ya State Visit (Ziara ya Kitaifa) na Working Visit (Ziara ya Kikazi)

Rais ni Rais tu, state visit na work visit ni jambo lile lile tu, tuache ujuaji mwingi.
Mbona katika "wprk visit" ya hivi karibuni huko USA aliweza kukutana na US Vice President.

Kwa hiyo basi uwepo wa Rais wa nchi moja katika ardhi ya nchi nyingine kwa vyovyote vile ni suala lenye kuhusisha itifaki ya kimataifa na pia ya kidiplomadia kwake yeye binafsi na msafara wake wote.

Na hii ndiyo sababu ya uwepo wa ofisi ya ubalozi katika nchi husika. Rais hawezi kwenda ziara ya kikazi katika nchi nyingine kienyejienyeji tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Naona kuna utofauti kati ya Ziara ya kikazi AfDB na ziara ya mwaliko toka serikali ya Ghana. Pengine jinsi vyombo husika vinavyotoa habari huchanganya wasomaji na kushindwa kuelewa dhumuni la safari, shughuli gani itafanywa na nani ametoa mwaliko n.k

23 May 2021​

MOZAMBICAN PRESIDENT ARRIVES IN GHANA FOR STATE VISIT

The President of the Republic of Mozambique, Filipe Jacinto Nyusi, has arrived in Ghana on Sunday for a four-day state visit, ending Wednesday 25 May 2022.

President Nyusi was met on arrival at the Jubilee Lounge of the Kotoka International Airport (KIA) in Accra by Ghana’s Vice President Mahamudu Bawumia.

President Nyusi will officially commence his visit with a meeting with Ghana’s President Akufo-Addo, at the Jubilee House this Monday 23 May 2022.

The President will also pay a visit and lay a wreath at the Kwame Nkrumah Mausoleum.

Also on the agenda of the visit of the Head of State is participating alongside President Akufo-Addo inthe opening ceremony of the African Development Bank Group’s 2022 Annual Meetings, being held from 23-27 May in Accra. President Nyusi will also pay a courtesy visit to the AfCFTA (African Continental Free Trade Area) Secretariat, as well as to the Parliament of the Republic of Ghana.

On this State Visit, President Nyusi is accompanied by the Minister of Foreign Affairs and Cooperation, Verónica Macamo; the Minister of Economy and Finance, Max Tonela; the Minister of Agriculture and Rural Development, Celso Correia; by the Deputy Minister of State Administration and Public Service, Inocêncio Impissa; deputies of the Assembly of the Republic; members of staff of the Presidency of the Republic and other State institutions.

ALSO READ: AfDB’s 57th annual meetings to kick off in Accra on Monday

We ended the day by joining the Vice President to receive the President of the Republic of Mozambique, H.E. Filipe Jacinto Nyusi, who is on a three-day State visit to Ghana. pic.twitter.com/qCFylnIsjj
— Samuel A. Jinapor (@SamuelAJinapor) May 23, 2022

Source: Asaasse Radio / O País

24 May 2022
Accra, Ghana

AFRICAN DEVELOPMENT BANK ANNUAL MEETING IN ACCRA 2022

02-1-1024x501.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022
 
Usiifananishe USA na nchi nyingine. Hata Obama akija hapa leo kuangalia Tembo atakaribishwa magogoni.
Mbona katika "wprk visit" ya hivi karibuni huko USA aliweza kukutana na US Vice President.

Kwa hiyo basi uwepo wa Rais wa nchi moja katika ardhi ya nchi nyingine kwa vyovyote vile ni suala lenye kuhusisha itifaki ya kimataifa na pia ya kidiplomadia kwake yeye binafsi na msafara wake wote.

Na hii ndiyo sababu ya uwepo wa ofisi ya ubalozi katika nchi husika. Rais hawezi kwenda ziara ya kikazi katika nchi nyingine kienyejienyeji tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo rais wa Marekani akija kwa work visite, Samia atauchuna ikulu hata enda kumpokea??
Hatalazimika kwenda kumpokea, wala rais wa marekani akija kwa work visit hatadai kupokelewa na Rais! Lakini kwa kawaida sijui kwa nini (labda kwa ajili ya ukarimu), ikulu hapatakalika itabidi tu aende kumpokea! Si unajua sisi waafrika tunajisikiaga vizuri kupokea wageni!
 
Hivi raisi wa marekani anaweza akaja hapa nchini akamaliza mwezi mzimaaa bila kuonana na samiaa??
Work visit haina maana hatakiwi kuonana na Rais, ila Rais hawajibiki na ujio huo!! Japo kwa kawaida hizi nchi za ulimwengu wa tatu huwa zinawashobokea sana marais toka nchi tajiri!! Kwa sababu mshoboko tu itabidi program nyingi za rais zisitishwe ili ampokee huyu mgeni ambaye kimantiki hahusiki naye!

Lakinin niseme jambo moja, usitegemee Rais wa Marekani aje bongo kwa work visit!! Labda Rais mstaafu!!! Work visit mara nyingi zinawahusu watendaji na si mkuu wa nchi!! Ukiona Rais ana safari nyingi za nje za work visit HAPO KUNA TATIZO!!
 
Sawa tumekuelewa,ila Rais anapokelewaje na mtu amevaa safety boots?Au hii nayo ni sheria ya working visit Kwa maana ya kazi kazi?
Hakuna hata dress code Kwa watu wanaompokea Rais,wale wa Ghana walivaa kishkaji sana.
Usalama wa mkuu wetu wa nchi ukoje huko nje ya nchi?Huko nje hatuoni hata mtutu wa bunduki,ngoja awe nchini,utasema tuko Somalia!!!!
 
Mbona katika "wprk visit" ya hivi karibuni huko USA aliweza kukutana na US Vice President.

Kwa hiyo basi uwepo wa Rais wa nchi moja katika ardhi ya nchi nyingine kwa vyovyote vile ni suala lenye kuhusisha itifaki ya kimataifa na pia ya kidiplomadia kwake yeye binafsi na msafara wake wote.

Na hii ndiyo sababu ya uwepo wa ofisi ya ubalozi katika nchi husika. Rais hawezi kwenda ziara ya kikazi katika nchi nyingine kienyejienyeji tu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Work visit bado siyo kienyeji!! Lakini Rais akienda nchi za nje kama work visit HAHESABIKI KAMA NI MGENI WA KITAIFA!! ASITEGEMEE KUPOKELEWA NA MKUU WA NCHI!! ASITEGEMEE KUPIGIWA MIZINGA!! ASITEGEMEE KUKAGUA GWARIDE LA KIJESHI!! Hii ndiyo hoja iliyopo!! Watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini mama akienda nchi za nje mara nyingi hapokelewi na Rais mwenzake!! Majibu yametolewa kwa ufafanuzi wa kina kwenye post namba 1 ya uzi huu. Nchi alizotembelea kwa State visit alipokelewa na Rais!! Mfano mzuri ni alipotembelea Kenya!!
 
Sawa tumekuelewa,ila Rais anapokelewaje na mtu amevaa safety boots?Au hii nayo ni sheria ya working visit Kwa maana ya kazi kazi?
Hakuna hata dress code Kwa watu wanaompokea Rais,wale wa Ghana walivaa kishkaji sana.
Usalama wa mkuu wetu wa nchi ukoje huko nje ya nchi?Huko nje hatuoni hata mtutu wa bunduki,ngoja awe nchini,utasema tuko Somalia!!!!
Hayo ni makosa ya balozi wetu wa Ghana, maana kwenye work visit balozi inabidi ahusike sana kuandaa mapokezi ya bosi wake, akishirikiana na wale ambao rais atahusika nao kwenye ziara hiyo ya kikazi. Ilibidi awaandae pia watanzania walioko huko wampokee kwa shangwe na mambo kama hayo!
 
Tutofautishe kati ya work visit na State visit!!

State visit (safari ya kitaifa)
lazima ukaribishwe na mkuu wa nchi!! Unapewa heshima zaidi na mapokezi yake yanafanywa na mkuu wa nchi, inaweza kuambatana na kupigiwa mizinga 21 na mwisho wa siku hupewa zawadi kama ukumbusho wa ziara hiyo ya kitaifa/state visit.

Work visit (safari ya kikazi) huwa mtu hajakaribishwa rasmi na mkuu wa nchi husika! lakini yeye anadhani kuna mambo anaweza kuyafanya huko kama majadiliano au kutembelea sehemu mbali mbali kwa ajili ya kujifunza nk!

Hii ni kwamba mtu ameamua mwenyewe kwenda huko au amekaribishwa na watu fulani naye akaona kuna kuna manufaa kwake au kwa nchi yake! Hapa asitegemee kupokewa na mkuu wa nchi!! wale wanaohusika na kile kinachompeleka wanaweza kumpokea. Lakini sana sana hupokelewa na balozi wa nchi yake na raia wa nchi yake walio huko!!

State visit ndiyo hupewa heshima kubwa lakini work visit ni kama mwananchi mwingine tu!! Ndiyo maana si vizuri sana mkuu wa nchi kutoka mara nyingi kwenda nchi za nje kwa ajili ya ziara za kikazi/work visit!! Hizo ziara mara nyingi huachiwa watendaji katika maeneo husika, sana sana waziri husika!!
Ni chungu kumeza lakini ndio ukweli wenyewe!! Sasa tujiulize kati ya safari zote alizotoka nje ngapi zilikuwa ni state visit/safari za kitaifa na ngapi zilikuwa ni work visit/safari za kikazi. Ikitokea kwenye State visit Rais asipokelewe na mkuu wa nchi mwenzake au mtu mwingine ambaye ametumwa kumwakilisha mkuu wa nchi kwenye mapokezi hayo, nchi husika iliyotendewa hivyo inaweza kuwasilisha malalamiko rasmi/protest!! Hata katika mazingira ambayo mkuu wa nchi alituma mwakilishi wake (waziri mkuu au waziri wa mambo ya nje), huyo mwakilishi atakapompokea atajitambulisha rasmi kwa mgeni kuwa ametumwa na Rais kumpokea kwa niaba yake kwa kuwa kutokana na sababu zisizozuilika hakuweza kufika mwenyewe!! Ngoja nikuachie desa kidogo:

What is a state visit?

A state visit is an official visit to a foreign country by a serving head of state. In order to travel to a country on a state visit, an official must be invited by the host country’s head of state.

Visitors typically include Monarchs, Presidents and Prime Ministers.

For example, the UK has previously welcomed former US president Barack Obama and United Arab Emirates royal Khalifa bin Zayed Al Nahyan.

The US has previously welcomed the UK’s Queen Elizabeth II and Russian president Vladimir Putin.

During state visits, the host nation offers its guests the highest level of hospitality. This extends not only the visiting official, but their delegation of personnel.

The host nation covers all of the costs, including accommodation and travel costs.

Typically, head of states visiting the United Kingdom are put up in Buckingham Palace, Windsor Castle or The Palace of Holyroodhouse in Edinburgh.

According to the official British Royal Family website, these visits “play an integral role in strengthening Britain’s relationships with countries across the world”.

What happens on a state visit?

Typically, countries do not organise state visits to discuss or debate issues. They are a celebration of sort which focuses on the links between the two head of states’ nations.

Each country has their own way of welcoming head of states shaped by its own customs. However, host nations typically welcome arrivals with at least some of these events:

  • A welcome from the hosting head of state and their ambassadors.​

  • A 21-gun salute, a military honour in honour of the visiting official.​

  • A military band playing both national anthems.​

  • An exchange of gifts between the two officials.​

Following the visiting official’s arrival, a state banquet is usually held in their honour. Both heads tend to give a speech at the end of a lavish meal.

Throughout the visit, the visitor often pays visits to landmarks and historic sites. For example, Barack Obama visited the tomb of the Unknown Warrior in Westminster Abbey during his state visit to the UK in 2011.

How is a working visit different?

A working visit is similar to a state visit. It still refers to an official visit to a foreign country by a current head of state. However, they are less formal than state visits and tend to be stripped back affairs.

Most often, these visits are organised for officials to discuss issues between their two countries, rather than strengthen relations.

Unlike a state visit, the hosting head of state doesn’t need to approve a working visit ahead of the planned trip.

The hosting head of state doesn’t offer a royal welcome and a stay in their home is off the cards too.

The visiting party covers all of the costs involved and must organise their own accommodation and transport throughout their stay.

SASA TUANGALIE: Ziara ya mama huko Ghana na kwingineko ambako mama alienda ambako hakupokelewa na mkuu wa nchi je ilikuwa ni State visit (Ziara ya kitaifa) au ilikuwa ni Work visit (Ziara ya kikazi)? Natupia hapa taarifa rasmi ya ziara ya Ghana:

By Bethsheba Wambura
More by this Author

Dar es Salaam. President Samia Suluhu Hassan has on Monday May 23, 2022 left the country for Ghana on a three-day work visit, State House has announced.

During her stay in the Western Africa country, President Samia will participate in a dialogue that will discuss opportunities and challenges facing African countries including the growing impact of climate change.

“The dialogue will also look at the rising food prices and sustainable energy,” reads the statement issued on Tuesday by the presidency.

HITIMISHO: Ziara ya mama huko Ghana ni ya kikazi (work visit)! Wanaofahamu hawakuwa wanategemea mama apokelewe na mkuu wa nchi mwenzake!! Akibahatika sana ni waziri yeyote (tena si kwa kumwakilisha Rais katika mapokezi hayo) kwa nafsi yake mwenyewe! Inabidi balozi wetu huko ndiye awajibike na mapokezi ya mama kwa kuwashirikisha watanzania walio huko!!
 
Attachments

  • Screenshot_20220524-202751.png
    Screenshot_20220524-202751.png
    145.5 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220524-202708.png
    Screenshot_20220524-202708.png
    156.8 KB · Views: 11
Hayo ni makosa ya balozi wetu wa Ghana, maana kwenye work visit balozi inabidi ahusike sana kuandaa mapokezi ya bosi wake, akishirikiana na wale ambao rais atahusika nao kwenye ziara hiyo ya kikazi. Ilibidi awaandae pia watanzania walioko huko wampokee kwa shangwe na mambo kama hayo!
Bado balozi ni mteuliwa na mwakilishi wa Rais!Pia Rais ana team yake ambayo nadhani wanatakiwa waconfirm na balozi kama maandalizi yamekamilika!
Haya,naomba unijibu kuhusu masuala ya kiusalama!
 
Acha kudanganya na kulisha watu matangopori. Hakuna tofauti ya work visit na state visit kwa Rais.
Work visit bado siyo kienyeji!! Lakini Rais akienda nchi za nje kama work visit HAHESABIKI KAMA NI MGENI WA KITAIFA!! ASITEGEMEE KUPOKELEWA NA MKUU WA NCHI!! ASITEGEMEE KUPIGIWA MIZINGA!! ASITEGEMEE KUKAGUA GWARIDE LA KIJESHI!! Hii ndiyo hoja iliyopo!! Watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini mama akienda nchi za nje mara nyingi hapokelewi na Rais mwenzake!! Majibu yametolewa kwa ufafanuzi wa kina kwenye post namba 1 ya uzi huu. Nchi alizotembelea kwa State visit alipokelewa na Rais!! Mfano mzuri ni alipotembelea Kenya!!
 
Bado balozi ni mteuliwa na mwakilishi wa Rais!Pia Rais ana team yake ambayo nadhani wanatakiwa waconfirm na balozi kama maandalizi yamekamilika!
Haya,naomba unijibu kuhusu masuala ya kiusalama!
Hoja ya msingi iliyopo ni Rais kutokupokelewa na Rais mwenzake!! Watu walikuwa wanahoji ni kwa nini?? Jibu ni kwamba Rais wetu yuko kwenye work visit na SIYO STATE VISIT!! Kwenye work visit Rais mwenyeji HALAZIMIKI kumpokea Rais mwenzake, HALAZIMIKI KUMTUMA AFISA MWINGINE aende kumpokea!! Anaweza kwenda kumpokea KWA MAPENZI YAKE mwenyewe lakini SI WAJIBU WA KIKAZI!! Logistics zingine zote anatakiwa ashughulikie balozi wa Tanzania (kwa mfano) aliyeko Ghana kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za nchi anakotembelea Rais yakiwemo masuala ya kiusalama!!

Kwenye state visit kila kitu kinapangwa na ikulu ya nchi mwenyeji, na balozi wa nchi anakotoka Rais anakuwa ni mmoja wa waalikwa rasmi tu kwenye kumpokea Rais.
 
Kwahiyo work visit inahalalisha Rais kupokelewa kihuni namna Ile?Mimi sipo kwenye hizo tofauti za visits,I'm concerned na jinsi Rais anavyoshushiwa heshima Kwa kupokelewa na watu wamevaa kihuni kihuni tu!
Hata kama ni work visit,basi hata waziri wa mambo ya nje?Yaani uhuru ashuke Airport DSM,apokelewe na mkuu wa wilaya kwasababu ni work visit?
 
Kwa taarifa tu: Huu mkutano mkuu wa Benki ya maendeleo ya Afrika unawahusu kina nani hasa kuhudhuria?

The 57th Annual AfDb meetings will bring together Finance and Central Bank Governors of all the 54 Africa Countries to meet in Accra,Ghana from May 23 to 27 May 2022 for their statutory meetings of Governors of the Bank.

Wanaotakiwa kimsingi ni Magavana wa Benki kuu wa mataifa yote ya Afrika. Rais wa Msumbiji yeye pamoja na kuhudhuria mkutano mkuu huo lakini pia alikuwa kwenye state visit nchini Ghana, ndiyo maana Rais wa Ghana alimtuma makamu wake kumwakilisha kwenye mapokezi ya Rais mwenzake!!
Ila Rais kuhudhuria mkutano huo ni sawa akiona anahitaji kujifunza kitu hapo na kupata mawazo mbalimbali!!
 
Back
Top Bottom