Rais Kikwete safarini Marekani

Rais Kikwete safarini Marekani

JERUSALEM, Israel


WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu hatahudhuria mazishi ya Hayati Nelson Mandela kwa sababu ni ghali mno kusafiri hadi nchini Afrika Kusini,


Kulingana na redio ya taifa la Israeli, waziri huyo itatumia kiasi cha 7.0 milioni shekels ambazo ni sawa na Sh170 milioni kusafiri nchini Afrika Kusini pamoja na walinzi wake


HAPA BONGO INAKUAJE KUHUSU SAFARI ZA WAKUU WETU UPAND EWA GHARAMA??

lakini hela za kuwaua watoto kina mama wa ki palestina wanazo? cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Duh!!tangia nione huyu baba anarudi mara mbili mbili kwenye msiba wa mandela baaasi nikaamini ana pepo la kusafiri,dah!!!!Leo kaenda tena marekani?Hivi hiyo ndege haijawahi hata kukata japo moto kidogo utumbo akamcheza aogope awe anampa yule makamu wake anyezunguka na mikasi tu japo katripu kamoja?
Masisiem ni laana kwa kweli.
 
Rais Kikwete amewasili Dubai usiku jana akiwa njiani kwenda marekani kwa ajili ya matibabu na kufanya check up ya afya yake.

Maafisa wa ikulu wamethibitisha kuwa safari hii ni kwa ajili ya matibabu tu ingawa haijasemwa anasumbuliwa na nini

Si waboresha hospitali za nyumbani jamani. Kuna siku watapata emergency kufika airport ikawa issue. Boresha hospitali zetu zitawakomboa siku moja.
 
Pamoja kuwa ni tetesi kuna mod mmoja kafuta posts zangu kwa mahaba yake zingine kaziacha kazi kweli.

Hao jamaa nao wanakera sana sijui wanaangalia kwanza usoni?
 
Nakumbuka kuna jamaa alishawahi kusema muheshimiwa asipojua kuendesha ndege atakua na kichwa kigumu sana..kwa safari hizi..

ha ha ha ha wakifika kwenye mawingu yasiyo na mabonde awe anamuomba rubani
 
Nyie pro-Chadema najua mna chuki sana na rais wetu JK hata kama anakwenda kutibiwa tatizo lipo wapi acheni unafiki basi, juzi hapa kiongozi wenu Dr.Slaa kaongozana na girlfriend wake Josephine kwenda Ujerumani kuangaliwa afya mlishangilia sana leo JK mnaanza kuponda acheni siasa za makengengeza.

Riz,

this is too much! kuweni wazalendo basi. Hosiptali hazina vitanda jamani.
 
Last edited by a moderator:
Safari 361 times (approx) 7 days time 3000USD

361 X 7 X 3000 = $ 7,581,000/=

$7,581,000 x Tsh 1,580/= (approx) =
TSHS 11,977,980,000
(BILIONI KUMI NA MOJA NUKTA TISA TISA)!!

UTANIBEEBA LEO.......!!!

Mahesabu yako ni off vibaya sana.

Hotel anayokaa tu kwa siku moja ni zaidi ya dola 3000.
 
Mahakama iamuru amungiwe ankle bracelet kama criminals wanaokuwa kwenye probation kwasababu amezidi sasa.
 
Haya maneno mwambie Dr.Slaa ambaye alikwenda Ujerumani kutibiwa na girlfriend wake Josephine

Hata kidogo usimfananishe aliyeshika na asiye na madaraka!!
Usitake Dr Slaa afie hospitali za ndani ya nchi zisizokuwa na vifaa ili umuone mzalendo! Cha muhimu tunawahoji walioshika madaraka, kwa nini wasiboreshe mazingira ya kazi katika hospitali zetu ili tuwahukumu hadi hao akina Dr Slaa!!
(Sijui kama nimeeleweka, hasa kwako)
 
Hivi kwann tusijenge ikulu nyingine marekani huyu mzururaji akakae huko?

wiki moja trip zaidi ya tano?

Hivi marekani hawana sera ya kukamata wazururaji kama hawa?

Naona umeishiwa na hoja, kinakukera nini mtoto? au umeshashiba saa hizi unabwabwaja tu.
 
Wamarekani wampe kansa tu watusaidie kutupunguzia mzigo!

Binaadam hujafa hujaumbika. Hivi kakosea nini haswa mpaka umuombee hayo? wewe unauhakika wa leo na kesho na keshokutwa? unajuwa litakalo kufika na nani ataekusaidia dunia hii?

Amma kweli naamini sasa, watoto wa mzazi mmoja utawajua tu.
 
Haya maneno mwambie Dr.Slaa ambaye alikwenda Ujerumani kutibiwa na girlfriend wake Josephine

Naona unamwota Dr Slaa kila wakati. Tunamjadili huyu mtembezi wa dunia, dr Slaa anaingiaje hapa.

Tuambie anaumwa nini ?
 
Binaadam hujafa hujaumbika. Hivi kakosea nini haswa mpaka umuombee hayo? wewe unauhakika wa leo na kesho na keshokutwa? unajuwa litakalo kufika na nani ataekusaidia dunia hii?

Amma kweli naamini sasa, watoto wa mzazi mmoja utawajua tu.

Umejifunza nini kwa maneno hayo. Wakati mwingine na wewe una maneno machafu kwa wengine.
 
Back
Top Bottom