mgombele jr
Member
- May 4, 2015
- 5
- 0
Wakati wa kufanya uamuzi ni huu,tukutane octoba pale kwenye sanduku la kura maana kuna wakati unaweza hata lia peke yako mtaani kwa sababu ya nchi hii Tanzania
Utafananisha Mtanzania wa leo na wa miaka 10 nyuma?
Leo mpaka kijijini kwenu mnaona ligi ya Uingereza kwa flat screen, yalikuwepo hayo kabla, kama ulikuwepo kabla ya Kikwete itakuwa kwa mara ya kwanza TV uliionea ulipofika mjini? Fikiri.
Kuna member anaitwa Faiza Foxy anasema JK ni best presdient after Mwinyi, na anaona nchi imekuwa na neema, utajiri, na maendeleo makubwa kuliko nchi yoyote ya Afrika, na Mtanzania anaishi maisha bora kuliko mwafrika yoyote. Subiri aje utaona.
Utafananisha Mtanzania wa leo na wa miaka 10 nyuma?
Leo mpaka kijijini kwenu mnaona ligi ya Uingereza kwa flat screen, yalikuwepo hayo kabla, kama ulikuwepo kabla ya Kikwete itakuwa kwa mara ya kwanza TV uliionea ulipofika mjini? Fikiri.
Nisingekuwa rais ningekuwa msanii wa bongo fleva
Maisha bora unayapima kwa kupanda na kushuka kwa dollar ya Kimerekani?
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Ndugu yangu kuongoza nchi si jambo dogo, ndo maana Mwalimu Nyerere aliwaambia kuwa Ikulu ni mzigo. Nyie ambao mnachonga sana hata kuongoza familia zenu yaani mkeo na watoto wawili au mmoja kama uliye naye inakushinda. Wengine hata mkipewa kuongoza kikao tu cha harusi mnachemka itakuwa kuongoza nchi. Urais ni Taasisi yamkini na wewe ukiwemo. Kusema Kikwete nchi imemshinda ina maana unajisema na wewe kuwa imekushinda. Wewe ulivyoona inakaribia kumshinda ulimsaidiaje pamoja na wenzako wanaochonga. Yapo mazuri mengi JK amefanya ila tatizo lako una roho ya ubishi. Hata nikikutajia hutakubali. Ila tafakari jinsi Watanzania wenzako wakati wa Mwinyi, Mkapa walivyokuwa wanahitaji paspoti ili kutoka Dar kwenda Bukoba. Ilibidi wapite mpaka wa Namnaga, mpaka wa Malaba, mpaka wa Mtyukula ili waende Bukoba. Lakini kwa sasa watu hao wanatumia siku moja toka Dar hadi Bukoba. Kwenda tu Lindi hapa jirani na Dar walikuwa wakitumia kati ya siku tatu hadi wiki kwa gari lakini sasa ni chini ya masaa kumi na mbili. Sasa ulitaka Kikwete akulipie mahari ndo useme kafanya vizuri. When you criticise try to be fair.uko sahihi kabisa huyu jamaa huwa sitaki hata kumuona au kumsikia kabisa kwa jinsi ambavyo aliachiwa nchi ikiwa nzuri uchumi imara na serikali ikiwa na pesa nyingi yaani ilikuwa ni kiasi cha kuiendeleza miradi aliyoachiwa badala yake nchi kaifikisha hapa tulipo leo kila kitu ni shida. Yaani huwa naikumbuka ile kauli ya mwalimu nyerere aliyomwambia wewe bado mwachie kwanza mkapa. Kumbe alikuwa na maana wewe huwezi kuiongoza nchi huna uwezo leo hii kila mtanzania analijua hilo ngoja niishie hapa maana nikiendelea kwa hasira niliyonayo naweza kujikuta natoa maneno yasiyofaa
Kaachiwa na nani wewe? wacha uongo.
Uchumi wa Tanzania ya leo si uchumi wa Tanzania aliyochukuwa Kikwete. Tulikuwa hatuna reserve ya pesa za nje hata ya mwezi mmoja leo tuna ya miezi minne.
Fikiri.
Acha ndoto za mchana mtu wewe. Kuona mabaya ni rahisi sana kuliko kuona mema hasa kwa watu kama ninyi wenye roho zilizojaa uovu. Mazuri hamyaoni. Mnafaa kuitwa mazuri blindness huu ni ugonjwa. Yaani mtu mwenye akili ya kawaida kama yako unashindwa kuona hata vitu ishirini vizuri ambavyo JK na wenzake wamefanya. Kama vyote huvioni basi ona hata uwezo wako wa kupata kisimu chako cha smart au laptop ukaweza kuandika haya. Pia ona uhuru na uwanja ulioupata kutoa maoni yako yasiyofaa. Hii yote ni kwa sababu ya Mhe. JK kuheshimu demokrasia ambayo ninyi mmeigeuza kuwa DOMOKRASIA.Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.
Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,
Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-
-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.
-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.
-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.
-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.
-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.
-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.
-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.
-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.
-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.
-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.
-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.
-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.
Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.
RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.