Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

jk means joka kuu? miaka kumi ya kutwanga maji. bora akajaribu na hiyo bongo fleva labda huko atafaulu. huyu anayemtetea anasubiri ubunge wa siku zilizobaki au? anatoa mapovu hata ukatibu kata hajapewa. au huwa anafaidi makombo pale magogoni.
 
Unamtetea au unauponda sijakupata vzr mdau ulichotaka kusema.

Na leo ameenda Dubai kuwasslimia waahezaji wa Yanga...Tanzania tukubali kuwa kwa hii miaka 10 nchi yetu ni km haikuwa na Rais makini na
 

Attachments

  • 1430725901845.jpg
    1430725901845.jpg
    49.6 KB · Views: 407
Na leo ameenda Dubai kuwasslimia waahezaji wa Yanga...Tanzania tukubali kuwa kwa hii miaka 10 nchi yetu ni km haikuwa na Rais makini na
Haah kashafika hadi Dubai dadadeki kwa hiyo atarudi after 1 week.
 
Haah kashafika hadi Dubai dadadeki kwa hiyo atarudi after 1 week.

Amepitia tu Dubai kupiga picha na hao jamaa then anaendelea na safari yake yenye watu wasiopungua 100, wengi humo ni washikaji zake wanaoenda kuangalia maghorofa Ulaya kwa kodi zetu!😉
 
Ifike hatua watz tuache unafiq kwa sababu za kisiasa kikwete kafanya mengi ya maana kuliko mabaya tatizo kushinda vijiweni na kuhuzuria mikutano ya mapadre wanasiasa angalia miundo mbinu ya tz ya sasa kama mtu wa kutembea utaelewa kero za miaka ya nyuma juu ya usafiri angalia ajira kwa vijana angalia uwekezaji wenye tija kwa nchi angalia uhuru wa vyombo vya habari miaka ya nyuma hayakuwepo haya leo kikwete anatukanwa na watoto wadogo kabisa lakini ni busara anatumia angalia mishahara kwa watumishi wa serikali. Utawala wa kikwete mema mengi kuliko mabaya tuongee ukweli kwa kuacha unafiq kilichomponza kikwete kuzuia mirija ya kiunyonyaji katika baadhi ya sekta za kidini hapo ndipo alipo likoroga huu ndio ukweli utaki andamana.
Hapa naona akili 2 zinapingana kuhusu gari Tnazania kuendelea na safari yake. AKILI1 inasema gari limeendelea na kujisifu kwa vigezo ilivotoa. AKILI nyingine inasema.... vigezo hivyo havijapeleka gari mbele kwani kusogea kidogo kama upo kwenye foleni wakati barabara nyeupe kwa maliasili zilizopo atajisifia kuwa gari limesogea wakati ulichofanikiwa ni kujitengezea foleni isiokuwa na maana!!!
HAYA kwenye gari hilo hilo wengine wanajitahidi kujaza mafuta na abiria wengine wanachota kujiwekea nje binafsi ili hali ikiwa tete wao wanasepa kivyao. Nahonda wa chombo anaona lakini analizika wanaposema tunarudisha bila kuwachukulia hatua (pesa za EPA) wengine baada ya kuona uzaifu wa nahodha wakaamua kuchota kivyao. Baadhi ya dili zikashtukiwa (ESCROW) Nakawaida ukimkamata mwizi kaiba mfano mafuta; usifikiri ni mara moja tu ndio ikatokea bahati mbaya ukamkamata; huyo kaiba sana nyuma na ile ilikuwa 40 yake. Ni sawa na kumkamata mtoto anadokoa mboga jikoni: ukamwambia rudisha bila kujua hiyo ndio tabia yake ukaikomesha. MAMBO YAKIARIBIKA NA WEWE NI SEHEMU YA TATIZO. TENAVHUFAI
NAJIULIZA UONGOZI WA GARI HILI UPO? NA hii akili inayotetea uongozi huu ukiona yote haya ni akili kubwa au ndogo?
NYIE mnaojiita ma great THINKER! Tukisoma between line misamiati yenu tuwaeleweje? KUPINDISHA MADA NIA KUPOZA MAKALI; KUPIGA WATU UPOFU; KUTETEA AJIRA AU NI SIKIO LA KUFA NUKTA.
NASUBILI NI ONE REPLY ITAEGEMEA WAPI!!!
 
kikwete hajafanya lolote zaidi ya Ku loot pesa zetu hazina.
angalia ma swahiba wake wakivyo neemeka,wameiba escrow alafu akaja kuwatetea,then yeye huyo eti anaagiza tume ya maadili kuwahoji walewale alikuwa akiwatetea.
huyu bwana ni ndumilakuwili ,ni MTU adiye aminika.muda wake uishe atuache na machungu yetu aliyotusababishia,
 
Jaman mnagundua leo kuwa kikwt nchi imemshinda? Kwan kipndi cha mkap mambo haya y mgomo hayakuepo kabisa kwn nw days mambo yamekuwa mengi yakienda hovyo!
 
Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.

Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,

Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-

-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.

-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.

-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.

-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.

-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.

-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.

-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.

-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.

-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.

-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.

-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.

-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.

Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.

RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.

Sio kama namtetea Mzee JK, ila ni kuwa Mkapa amemwachia JK hiyo ndege wakati tanki za mafuta zinavujisha. Sasa ndege ilipoananza kupungua altitude JK alitakiwa arekebishe ila ameshindwa
 
hivi nyie leo mnaweza msema kwa mazuri JK? Watu wenye akili zetu tumeona mengi na mazuri alioyafanya JK wala sikusubiri wewe ukae nyuma ya monitor uniambie JK hajafanya kitu.
 
Toka tarehe ya kwanza aliyoingia madarakani, nchi ilianza kumshinda siku hiyo ya kwanza.
 
Tatizo litakalo tumaliza nchi hii ni kuchagua watumikia vyama badala ya kutumikia wananchi. So long as matwakwa ya vyama na washirika wao yapo salama hawatajali matatizo ya wananchi, ndio maana watu kama kina faizer foxy wanatetea hata ujinga uliowazi wazi. Ni ukweli uliowazi kabisa katika miaka 10 ya uwamu ya nne nchi imeongozwa kwa viwango vya chini sana ni halali kusema nchi haikuwa na Rais kwa kipindi cha miaka 10. kwa kipindi hiki tulikua na magenge ya watalii wa ndani na nje kwa kufuja kodi za wananchi,wizi, ufisadi na uharamia wa mali asili na mazao ya maliasili.


wanaosema awamu ya nne imejenga miudo mbinu nawahangaa sana, awamu hi inachofanya ni kuendeleza kidogo tu cha yaliyoachwa na awamuya tatu.wengine watatoa mifano ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya kasi dar ukweli ni kwamba ni moja ya matumizi mabaya kabisa ya fedha za ummma yaliyowahi kutokea. unajiuliza swali la msingi hivi kweli foleni za dar zilihitaji kubomoa na kujenga upya barabara kama za morogoro na zingine?? Hata mtu mwenye akili ya kawada atakuabia kuwa foleni za dar zinasababishwa na mambo makubwa matatu.

1.msongamano kwenye makutano ambapo suluhisho lake lingekuwa fly over

2.barabara chache za pembeni zinazongi ndani ya jiji ambapo suluhisho lake lilikua kuongeza barabara za pembeni na sio kubomoa zilizopo

3. uboreshaji wa maeneo ya maegesho ndani ya jijji
lakini kwa sababu ya mihemuko ya ten percent na ufisadi wakakimbilia kubomoa ili wapate mradi mkubwa wenye rushwa kubwa.

kuna mambo mengine mengi ukiyaangalia unashindwa kuelewa utendaji kazi wa awamu ya nne.
 
uko sahihi kabisa huyu jamaa huwa sitaki hata kumuona au kumsikia kabisa kwa jinsi ambavyo aliachiwa nchi ikiwa nzuri uchumi imara na serikali ikiwa na pesa nyingi yaani ilikuwa ni kiasi cha kuiendeleza miradi aliyoachiwa badala yake nchi kaifikisha hapa tulipo leo kila kitu ni shida. Yaani huwa naikumbuka ile kauli ya mwalimu nyerere aliyomwambia wewe bado mwachie kwanza mkapa. Kumbe alikuwa na maana wewe huwezi kuiongoza nchi huna uwezo leo hii kila mtanzania analijua hilo ngoja niishie hapa maana nikiendelea kwa hasira niliyonayo naweza kujikuta natoa maneno yasiyofaa

Pole sana Bw. Nyirenda, wote tunahali ya hasira sana. Tafakari chukua hatua Oktaba sio mbali. elimisha watu wakajiandikishe kupiga kura. Duh! inaudhi sana
 
Nikiangalia viongozi waliowekwa hazina, nabaki natikisa kichwa tu! Sijui tumelaaniwa na nani

kikwete hajafanya lolote zaidi ya ku loot pesa zetu hazina.
Angalia ma swahiba wake wakivyo neemeka,wameiba escrow alafu akaja kuwatetea,then yeye huyo eti anaagiza tume ya maadili kuwahoji walewale alikuwa akiwatetea.
Huyu bwana ni ndumilakuwili ,ni mtu adiye aminika.muda wake uishe atuache na machungu yetu aliyotusababishia,
 
Ni janga la kimataifa muda uiashe aondoke uwezo wake ni kuwa diwani tukachemka kumpa nchi
 
Athari za uswahiba hizo kupeana vyeo pasipo kujali uwezo wa,mtu mahali husika pamoja na kutokuwa na msimamo kuishia kukutoyapa uzito mambo ya msingi
 
CCM haina huluma na mtu wa kawaida hasa mackini

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Fanya kuedit hapo uongeze kubwa kuliko yote

Kupaa kwa deni la Taifa toka Trl 4 alizozikuta wakati anaingia madarakani mpaka Trl 39 hivi sasa (Bado hajaondoka madarakani.!!

Tutakwisha..!!

BACK TANGANYIKA

Hivi alikuta deni la taifa likiwa 4tri na sasa kalipaisha hadi 39tri?
 
Back
Top Bottom