Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Rais Kikwete nchi imemshinda mwanzo mwisho

Anayesema hakuna mazuri aliyoyafanya JK atakua ni mnafki,kiukweli JK as shemeji yangu kwakua kamuoa dadangu (Mwalim mwenzangu)amefanya mengi sana mazuri,hapa ntaorodhesha machache tu.
1.Kuwasamehe baadhi ya wezi wa EPA
2.Kushindwa kutumia vyombo vya dola kuitambua KAGODA AGRICULTURE
3.Kuwatimua watu juu ya pesa za escrow while si za umma
4.Kuongeza kiwango cha ufaulu,ambapo kwa sasa mtoto mwenye divisheni four ya 34 anasoma advance level
5.Kupambana na ujangili
6.Kupambana na wauza unga
7.Kuwa na mawaziri wachapa kazi,sijui huwa anawapataje
8.Kuwa mkali sana kwa wanaojihusisha na rushwa
9.Kuboresha huduma za afya,kila kata kuna zahanati
10.Kuondoa kero ya maji mijini hasa Dar es Salaam
11.Kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima
12.Kutopenda kusafirisafiri kwenda nje ya nchi hasa amerika

Tusisahau:
13. Kuikoroga nchi kuhusu mchakato wa katiba mpya.
14. Kuifilisi hazina ya nchi.
15. Kutengeneza mazingira ya chama tawala kusambaratikia mikononi mwake.
16. Kusimamia vyombo vya dola kuua RAIA wanaotetea maslahi yao, nk nk
 
Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.

Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,

Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-

-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.

-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.

-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.

-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.

-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.

-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.

-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.

-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.

-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.

-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.

-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.

-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.

Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.

RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.
Kwa haya uliyoyasema,me naona JK aongezewe muda tu wa kutawala
 
Ifike hatua watz tuache unafiq kwa sababu za kisiasa kikwete kafanya mengi ya maana kuliko mabaya tatizo kushinda vijiweni na kuhuzuria mikutano ya mapadre wanasiasa angalia miundo mbinu ya tz ya sasa kama mtu wa kutembea utaelewa kero za miaka ya nyuma juu ya usafiri angalia ajira kwa vijana angalia uwekezaji wenye tija kwa nchi angalia uhuru wa vyombo vya habari miaka ya nyuma hayakuwepo haya leo kikwete anatukanwa na watoto wadogo kabisa lakini ni busara anatumia angalia mishahara kwa watumishi wa serikali. Utawala wa kikwete mema mengi kuliko mabaya tuongee ukweli kwa kuacha unafiq kilichomponza kikwete kuzuia mirija ya kinyonyaji katika baadhi ya sekta za kidini hapo ndipo alipo likoroga huu ndio ukweli utaki andamana.

Udini Umekujaa.Bila shaka wewe ndie uliyeidanganya CCM iweke MAHAKAMA YA KADHI kwenye Ilani yake.
 
Swali lako lishatoa jibu wewe ni mnafiq

umeshindwa kujibu maswalili maisha yetu ni ya kubahatisha ule mkanda tuliojifunga mwaka 78 umezidi kutubana hasa wakati huu rais ambaye safari za kwenda nje ya nchi ni nyingi kuliko safari za kukagua miradi ha ha ha ha ha ha

utakuua wewe unatetea visivyotetewa
 
Majitu mengine sijui kwa nini yalizaliwa. Unaudhi dada FOXY. Usiweke CCM yako mbele kwenye masuala muhimu. Kwa hiyo wewe shule yako inakusaidia kushabikia huo ujinga unaouita? Taabu sana.
 
jk hajafanya lolote la maana kiongozu dhaifu mzembe asiye na dira kuliko wote afrika kwa sasa kila analojaribu anashindwa sijui ana mkosibgan huyu jamaa atike tu oktoba sina cha kumshukuru na lazima.atuombe.msamaha kwa kutupotezea miaka 10.
 
Wewe dada unakufuru maisha yamekua magumu maji watu hawana udogoni maji kila nyumba leo hii aibu
treni kwenda mwanza ilikua ya uhakika
maisha magumu kariakoo sio tanzania nzima Maisha magumu unayaona kwenye tv tu
hujawahi kuwaona baba mama na watoto sita wanalala chumba kimoja hapa hapa dsm
ulivyoambiwa kuwa uyaone sio maghorofa ya hapo kariakoo
hebu njoo huku kwetu hatuingii ndani bila kuvuka mavi choo kimoja watu 20 hebu acha masikhara
unajua tunadaiwa dollar ngapi ?
mbaya zaidi dollar imepanda wewe bibi mnafki sana

Wewe unakunya barabarani afu unasingizia CCM? Blackblaskut nyama-mkebe we!!
 
Tuache ushabiki,kiukweli tumepiga hatua kubwa katika maendeleo.
Kinachokosekana sasa kitajazilizwa na Rais ajaye.
Mh.Rais Kikwete amepambana kadri alivyojaariwa na Mwenyezi Mungu kuwasaidia Wananchi wake,kipindi cha uongozi wake kilikuwa kigumu sana kuliko awamu zote.
Tumpongeze hakika ameweza kutuachia ujasiri wa ushindani miongoni nchi zetu washirika,mwenye akili na aone.
 
Hebu fafanua kidogo,amepambana na nini?haya tunayoyaandika huwa hayafutiki ujue,watu watakuja kuyasoma hapa,isije ikawa unaaandika hapa kumbe mwenzetu unanufaika na mfumo uliopo
 
Wewe unakunya barabarani afu unasingizia CCM? Blackblaskut nyama-mkebe we!!
Zamani huduma ya choo ilikuwa bure,kuanzia April 24 huduma ya choo ni Tsh 300/= iwe kunya au kukojoa,sasa kama serikali ya CCM ingeweka utaratibu wa huduma za vyoo za bure asingekunya barabarani,so anakunya barabarani kwakua CCM imeshindwa kuweka huduma za choo za bure,usidhani 300/= ni hela ndogo,juzi pale kituo cha daladala cha mbezi mwisho nilimsikia mzee mmoja akisema "Yaani Kukojoa tu 300/=!!!!....kukojoa tu....hakuna sabuni wala nini?"
 
Meli ya kwenda bukoba hadi leo imepaki inataka matengenezo 16bl tu irudi kubeba ndizi na abiria
Je hii meli haijawahi tufanya faida ya hiyo 16bl?
Je watu wa bukoba sio muhimu hadi akanunua mimeli ya kivita wakati nchi haipo vitani??

Cc watu wa lumumba
 
hebu njoo huku kwetu hatuingii ndani bila kuvuka mavi choo kimoja watu 20 hebu acha masikhara
unajua tunadaiwa dollar ngapi ?

Zamani huduma ya choo ilikuwa bure,kuanzia April 24 huduma ya choo ni Tsh 300/= iwe kunya au kukojoa,sasa kama serikali ya CCM ingeweka utaratibu wa huduma za vyoo za bure asingekunya barabarani,so anakunya barabarani kwakua CCM imeshindwa kuweka huduma za choo za bure,usidhani 300/= ni hela ndogo,juzi pale kituo cha daladala cha mbezi mwisho nilimsikia mzee mmoja akisema "Yaani Kukojoa tu 300/=!!!!....kukojoa tu....hakuna sabuni wala nini?"

Soma vizuri mwenzako huyo analalamika anajisaidia kwenye mlango wa nyumbanikwake. MO11 ameshindwa hata na yule teacher wa Kibasila aliyekuwa anajisaidia kwenye mabeseni..ahh
 
Attachments

  • 1430584451633.jpg
    1430584451633.jpg
    77 KB · Views: 348
  • 1430584493997.jpg
    1430584493997.jpg
    69.5 KB · Views: 322
  • 1430584531721.jpg
    1430584531721.jpg
    58.4 KB · Views: 317
Soma vizuri mwenzako huyo analalamika anajisaidia kwenye mlango wa nyumbanikwake. MO11 ameshindwa hata na yule teacher wa Kibasila aliyekuwa anajisaidia kwenye mabeseni..ahh

umeelewa lakini au umelewa ?
 
Shilingi ya Tanzania imeporomoka dhidi ya dola ya Marekani kutoka 1,500 wakati JK anaingia madarakani hadi 2,000/= . Hii maana yake ni nini? Umechumi umeporomoka mnoooooo. Nchi kwa kiasi kikubwa imekuwa ya wachuuzi badala ya wazalishaji; tunanunua zaidi kutoka nje tunauza kiduchu. Yote haya yanasababishwa na mikataba mibovu ya uwekezaji; faidi inayotokana na uwekezaji katika madini inazinufaisha nchi watokazo hao mabepari sisi tumebaki na 10% na shanga.
 
Kwa haya uliyoyasema,me naona JK aongezewe muda tu wa kutawala

Ndio mbinu mbadala inayoandaliwa kwa siri na kwa ujanja ujanja,(ila ameshagonga mwamba) miaka 10 ameshindwa hata ajiongezee miaka mingine tutakachoambuliwa ni HASARA ZA KUDUMU.
Nia ya kujenga Nchi haimo ndani yake na ni kujilimbikizia akiba kwa vizazi vya familia yake tu.
 
Fanya kuedit hapo uongeze kubwa kuliko yote

Kupaa kwa deni la Taifa toka Trl 4 alizozikuta wakati anaingia madarakani mpaka Trl 39 hivi sasa (Bado hajaondoka madarakani.!!

Tutakwisha..!!

BACK TANGANYIKA

Kuna member anaitwa Faiza Foxy anasema JK ni best presdient after Mwinyi, na anaona nchi imekuwa na neema, utajiri, na maendeleo makubwa kuliko nchi yoyote ya Afrika, na Mtanzania anaishi maisha bora kuliko mwafrika yoyote. Subiri aje utaona.
 
Unazungumzia kikwete gani na nchi gani maana kwa hii nchi ya tanzania na kikwete wetu hatuna shida taifa linasonga mbele kwa spidi ya ajabu.
 
Kuna member anaitwa Faiza Foxy anasema JK ni best presdient after Mwinyi, na anaona nchi imekuwa na neema, utajiri, na maendeleo makubwa kuliko nchi yoyote ya Afrika, na Mtanzania anaishi maisha bora kuliko mwafrika yoyote. Subiri aje utaona.
Naungana na faiza foxy jk is the best one kama hutaki unaacha kalitoa taifa mbali sana sasa linakimbia kwa maendeleo.
 
Back
Top Bottom