12STONE
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 1,190
- 409
Nimejaribu kufuatilia kwa makini na hatua kwa hatua tangu huyu mzee aingie madarakani ili nibaini ni kipi ametenda hata tumkumbuke baada ya kuondoka kwake madarakani Octoba 2015. Nimegundua kwa 97% mkuu wa kaya ameshindwa vibaya mno kuleta MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA aliyotuahidi.
Mh.MKAPA alimwambia nakuachia Nchi kama ni Ndege wakati huo ilikuwa iko kwenye RUNNING,Alichopaswa kufanya ni kuipaisha tu ili ikifika Octoba ili ndege hio itue ikiwa imesheheni unono na urojorojo, Uchumi ulioimara kwa kila MWANANCHI. BADALA YAKE NDEGE HIO JK ALIIZIMA,
Tumaini la Wananchi likapotea, kila kitu kikavurugika:-
-Mfumko wa bei kwa BIDHAA zote ukawa juu.
-Shillingi yetu ikaporomoka kwa KASI MPYA,NGUVU MPYA na ARI MPYA.
-Tatizo la umeme mpaka kesho ni kitendawili Nchini.
-Ujambazi umerudi kama ilivyokuwa zama za kale hadi Polisi wanauawa na silaha kuibiwa VITUONI.
-Ziara za nje ya Nchi za kutembeza BAKULI LA OMBA OMBA (BLO)Awamu ya nne inaongoza kwa safari zenye kulitia hasara Taifa letu.
-Waandishi wa Habari na Wanaharakati kuuawa na kuteswa.
-Umwagaji damu usio wa lazima kutokea kwenye maandamano.
-Ajali na ongezeko la vifo na vilema vimekithiri awamu ya nne.
-Mikataba mingi inayohusu RASILIMALI ZETU imesainiwa kwa SIRI na WACHINA bila Raia kujua kinachoendelea ndani yake.
-KATIBA PENDEKEZWA ni kiini macho uhalisia UMEENGULIWA na BATILI imewekwa mbele.
-DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA -Uandikishwaji wake unacheleweshwa kwa MAKUSUDI.
-Hata ndani ya CCM uchaguzi wa kumpata Mgombea Urais hali ni tete mpaka leo.
Kwa uchache tu haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha kuwa NCHI IMEMSHINDA JK MWANZO MWISHO.
RAIS ajaye anatakiwa awe ngangari kweli kweli la sivyo JAHAZI LITAZAMA.