Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Maisha magumu sana. Yeye anachowaza ni kuteua watu wake ili apate sifa na kukusanya kodi kuwalipa wateuliwa wake.
Hana lingine..
Hadi wanafunzi wa china kawanyima mkopo. Watateseka sana ..
 
Ni wajinga tu ndo wanajisumbua kuunga mkono mambo yanayoturudish nyuma
Waambie mambo mazuri aliyofanya MHESHIMIWA siyo kutukana TU mfano waambie kanunua ndege na nyingine zinakuja,kaweka nidhamu ya kazi,katoa watumishi hewa na vitu kama hivyo RAFIKI yangu
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Ukimuunga wewe inatosha usitulazimishe...... Kama nimapenzi niwewe nayeye cc hayatuhusu
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Atampeleka nani huko mahakamani wakati mafisadi ndio walio muweka madarakani? Kina mkapa, kikwete, kinana, nawenzao akiwapeleka hao nitamuamini akishindwa never
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Yeye mwenyewe hapendi kuungwa mkono na wala hataki ushauri wa mtu, anataka aendeshe yeye kama yeye na zaidi kwa kutumia ubabe
 
Ivi Quinine ni mwanamke au mwanaume?
Nchi ni ya watanzania na si ya raisi magufuli kama huyu quinine mwenye akili za wapi sijui anavyodhani. Kama wewe ni kada la bavicha kwa akili hizi wacha mkapa awatukane, na kwa kufanya hivi nimetokea kuidharau sana chadema kwa utumbo kama kama huu uliowekwa jamvini na huyu kaquinine sijui. Wewe ni shetani kushabikia kufail kwa serkal kwa mambo yenye tija na maana katika nchi. Mim si mwanachama wa ccm ila naunga mkono baadhi a shughuli nyingi tu zinazofanywa na serikali. Utakuwa umeguswa na magufuli kwa namna moja au nyingine mana unashabikia ujinga, watanzania wengine hovyo kabisa, usijiingize kwenye kilio cha matajiri wezi as if wao walikuwa wanakusaidia kulia pindi walipokuwa wanakunyonya.
 
he was designated to fail jamaa ana roho mbaya mno wacha mwenyezi Mungu amuonyesha kwamba hakuna kama yeye anavozidi kutesa wananchi ndivyo anavyokosa Baraka za kiuongozi
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Nonesense. Vibaka wapelekwe mahakama ya mafisadi ili iweje? Na mahakama nyingine zitafanya kazi gani? Nani asiyewajya mafisadi wa nchii hii. Unafki ni dhambi mbaya sana. Kama kuna nia ya dhati aanze na wabunge kadhaa waliowahi kutajwa kwenye kashfa mbalimbali za mabilioni ya walipa kodi. CCM ni ile ile ubavu wa kushughulika na hoja za msingi haupo.
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Aliahidi kumpeleka mahakamani fisadi aliyehamia cdm ....mm km mzalendo naunga mkono hili la kumpeleka huyo fisadi mahakamani bt naona haitimizi hii ahadi.... he should be a man of his own words.
 
Heshima ya utumishi Wa umma imerudi, uzembe kazini umepungua,
Hela za dili hazipatikani siku hizi ndio maana kuna kelele hamna hela mifukoni,
viwanda kama 1000 vinafunguliwa bagamoyo ili kuongeza kodi na ajira kwa vijana,
bomoa bomoa inaendelea mbez-kibaha kupanua Barbara ya mwendo kasi bila kujali nyumba ya nani iko barabarani,
mikopo inarejeshwa kwa kasi kwa waliokokopeshwa tangu 1994 hii itasaidia kukopesha idadi kubwa zaid mwakani, safari/warsha/ semina za nje zimepungua,
utegemez Wa misaada kutoka kwa wajomba zetu imepungua, ni aibu kutembeza bakuli nje wakati rasilimali ziko za kutosha
Salamu kwako Quinine

Brother, they have eyes which do not see ears which do not hear....hata ungekesha kuwaeleza hawatakaa wakubali...Alipowatumbua wakaja na kelele kuwa anakisasi, akaamua kuacha yaliyopitia aangalie mbele wamerudi tena na makelele ame poa, hawajui wanachokitaka au kikatafuta....Just leave them as they are...Watatukuta Caanan nao watataka waadnikiwe meza za mbele....
 
Quinine Rais amepewa na wanancchi mandate ya miaka mitano kuongoza nchi na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Ndio kwanza tumemaliza mwaka mmoja, kutoa hukumu kwamba Rais atamaliza muda wake akayaacha kama alivyoyakuta ni upotoshaji or rather wishful thinking.

wakati ni muamuzi sahihi wa kufanikiwa kwa Rais...na wakati huo ni miaka mitano na sio mwaka mmoja. Lakini hata ukiamua kumpima kwa mwaka mmoja, umechagua kuyaacha mambo ya msingi yaliyokwishafanyika yenye manufaa kwa wananchi wengi.

Jambo la kwanza na kubwa lililofanyika ni kutoa ELIMU BURE kuanzia msingi hadi sekondari. usipoangalia jambo hili kwa upana,waweza kudhani ni jambo dogo,lakini ukweli ni kwamba familia zote mijini na vijijini zenye watoto wenye umri wa kwenda shule, sasa wana uhakika wa elimu ya watoto wao katika ngazi hiyo ya msingi.

Eneo jingine ambalo Serikali inachukua hatua ambalo watu wengi hawalizungumzi ni kulipa madeni. Tunaposoma habari kwamba serikali imekopa fedha kujenga barabara, hospitali n.k maana yake ipo siku tutatakiwa kulipa. Serikali ya Awamu ya tano imeingia madarakani katika kipindi ambacho madeni yaliyokopwa miaka ya nyuma yamemature na yanatakiwa kulipwa. Kwa kuweza kulipa madeni hayo ndiko kunakoifanyTanzania iendelee kuaminiwa na mashirika ya fedha ya kimataifa kuendelea kukopeshwa fedha kwa ajiili ya kutekeleza miradi mipya ambayo itawagusa wanachi walio wengi

Kuanza hatua za Kutekeleza miradi yenye tija kwa wananchi wengi. hivi sasa Serikali ipo kwenye hatua ya kupata mkandarasi wa kujenga Reli ya Kati katika Kiwango cha kimataifa. Mradi huu utafungua upya fursa za uchumi kwa wananchi wa dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Mwanza.....Reli itakapojengwa itatoa ajira kwa maelfu ya wanannchi, na itakapokamilika itarahisisha usafirishaji wa mizigo na kupunguza gharama za kufannya biashara kutokana na urahisi iwa usafiri...lakini sio hivyo tu ikikamilika itapungusa kasi ya uharibifu wa barabara zetu ambazo zimejengwa kwa pesa nyingi za walipakodi na mikopo tunayoendelea kuilipia

Kupunguza mianya ya upotevu wa fedha za umma kwa njia ya ukwepaji kodi, malipo hewa (mishahara hewa, wanafunzi hewa, zabuni hewa) pamoja na overpricing/overcharging zilizokuwa zinafanywa kwenye manunuzi ya umma ambayo mwisho wake mzigo ulikuwa unabebwa na walipakodi. Juhudi zilizokwishafanyika zinastahili kuungwa mkono,lakini zaidi ushirikiano wa wananchi wazalendo, wenye nia njema ya kuona maovu yanatoweka unahitajika sana....Rais hawezi kujua kila kitu kinachotokea kila mahala.....anahitaji ushirikiano wa wananchi, anahitaji utendaji bora wa vyombo vyake.....


Mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni.....ndani ya muda mfupi tumeona ndege yetu iliyokuwa inachechemea miaka nennda rudi inaruka.....tena ikiwa na ndege mbili mpya tunazomiliki wenyewe. Wapo watu wanabeza mafanikio hayo....pengine ni kwakuwa tumesahau tulikotoka......hivi mnajua ATCL iliwahi kukodikukodisha ndege ya zamani na kulipia mabilioni ya shilingi? leo hii tunamiliki ndege,hatudaiwi na mtu...si jambo la kubeza.


Kwa vyovyote vile, yapo mapungufu na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ndani ya mwaka mmoja, lakini hazitoshi kutoa hukumu ya kushindwa kazi wakati kuna mafanikio mengi na muda wa miaka minnne wa kutekeleza zaidi. Tumpe nafasi Rais wetu atekeleze wajibu aliopewa na wananchi ili tutoe verdict yetu vizuri baada ya miaka mitano. pale penye mapungufu tuwe wazalendo kutoa solutions zifanyiwe kazi na sio kupinga tu maana nchi hii ni yetu sote.
Umeongea vinzuri , tatizo yote aliyofanya hayana msingi shirikishi, yaani hakuna utendaji Wa kitaasisi rushwa IPO wapi nguvu ya takukuru, uwajibikaji Wa w/umma sipo wapi taasis za maadili au n hawa wakuu Wa mikoa, reli , ndege liko wapi bunge, kwenda Dodoma IPO Wa nguvu ya kibudget. Alafu eti waungwe mkono upi they know everything, future hakuna. Ila hata hivyo tumezoea kupata kidogo, tutasifia. Nchi zingine zikifanya kweli tunawaza std gauge angalia Ethiopia wanaongelea nini?, wakati maamuzi ya madiwani si kitu, nguvu ya miji,majiji Na halmashaur hoi siasa mbele, maneno matupu, macho kwenye kura hakuna lolote, ok, ok, ok.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Hujajibu hoja hata moja!Umeweka mipasho tu
 
Back
Top Bottom