Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Acha kutokwa na povu, kaainisha hoja zake, njoo na hoja kinzani siyo kuja na hoja za kutafuta huruma ya watu.
hoja gan gan zisizo na data mkuu? hoja zinaendana na data/ushahidi wa kitakwimu sio kama alivyofanya hapo kuchukua hisia na kupost si sahihi.
 
na Kuna watu ndani ya ccm wanamishemishe asitoboe 2020..baada ya mianya yao ya Wizi kuwekwa super glue w
kwa hiyo wewe unshabikia wizi baada ya kuzibwa mionya ya wezi???

Tatizo la nchi hii ni ccm.....[/QUOTE]
refer kauli ya Dr Slaa aliposema kwamba ukiitoa CCM ndo na matatizo ya nchi yamekwisha? hebu tuweni serious bwana punguzeni hisia mruhusu akili zitumike..!!
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Tunamuunga mkono tatizo ni kwamba hatupigi hatua
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Naomba kuongezea hata ile vamia vamia ofisi za serikali nayo tumerudi kule kule
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Sasa hiyo Mahakama ilianzishwa ya nini kama mafisadi wanaweza kunyooshwa bila ya Mahakama hiyo?
 
Hii ni sawa na dereva mwanafunzi anayeendesha mita 70 kwenda mbele kisha unamwambia weka gia namba mbili naye anweka ya reverse na gari linarudi mita 90 ila yeye anaamini amekwenda mbele mita 160
Duuu hatarii [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Hii ni sawa na dereva mwanafunzi anayeendesha mita 70 kwenda mbele kisha unamwambia weka gia namba mbili naye anweka ya reverse na gari linarudi mita 90 ila yeye anaamini amekwenda mbele mita 160
Duuu hatariii[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
MTanzania anaemuunga mkono Magu akili yake itakuwa sio nzuri huyo,watanzania tulikuwa na furaha awamu ya nne ya utawala wa CCM,awamu hii ya tano watanzania wamegubikwa na ukungu mzito wa majonzi,maisha ya mtanzania yamekuwa hayana uhakika wa kesho..

Mimi ni mmoja katika watanzania waliokuwa wakimfagilia Magufuli,lakini baada ya kuona vipi anafanya kila juhudi kuwanjima haki za msingi watanzania hapo nikamuona hana maana hata kidogo..

Katika historia Tanzania haijawahi kutokea watanzania kuwa na woga kama awamu hii,Nchi yoyote yenye raia wenye woga wa maisha haiwezi kupata maendeleo ya aina yoyote,nidhamu ya woga ni moja katika kitu kinacholeta umasikini kwa mwanadamu...

Watanzania ni watu wa kujituma,watu wa kujaribu mbinu tafauti katika kuleta maendeleo katika maisha yao,sijui humu ndani ya JF kama kuna anaefahamu hili neno Bongo limekujaje au nani kalibuni,kama mtataka kujua nitakufamisheni lakini kwasababu hii mada hausiano na hilo jina basi tupotezee tu..

Magufuli ilikuwa haina haja ya yeye kama raisi kuanza kubaguwa anaowatala,ilikuwa haina haja ya kuwanyanyasa watanzania walikuwa wana mawazo tafauti na yeye,yeye alikuwa anatakiwa akumbuke kuwa ni raisi wa watanzania wote,walio na mawazo kama yake na wasio na mawazo kama yake..

Ukianza kuwafanya unao watawala wabaguane,huwezi kuleta maendeleo katika nchi, kama raia hawalewani,leo hii raisi anafika hadi kusema "hawa msiwavunjie ni wapiga kura wangu",Je raisi wetu ana tawala kwa visasi...,Mh Zitto ameshawahi kuwa Tanzania ina tawaliwa na washamba,hii ni kweli raisi wetu ni mshamba..

Mwalim Nyerere wakati wa utawala wake alikuwa anasisitiza sana utani miongoni mwa makabila ya watanzani,utani ni moja katika mila na jadi za waTanzania,utani unaleta maelewano katika jamii...

Raisi wetu Magu hataniwi ukimtania anakufunga,ukimwambia ukweli anakufunga,ukimkosoa anakufunga,raisi haambiliki,anaona anaowatawala ni wajinga mwerevu yeye peke yake,hivi sasa waTanzania hawataniani tena,waTanzania wameanza kuzungumza ukabila na udini...

Huyu raisi hafai kututawala watu wapole na wastarabu kama waTanzania.....,tutafutieni mwengine
 
From hero to zero. Yule Dada kule Twitter kasema kweli
 
MTanzania anaemuunga mkono Magu akili yake itakuwa sio nzuri huyo,watanzania tulikuwa na furaha awamu ya nne ya utawala wa CCM,awamu hii ya tano watanzania wamegubikwa na ukungu mzito wa majonzi,maisha ya mtanzania yamekuwa hayana uhakika wa kesho..

Mimi ni mmoja katika watanzania waliokuwa wakimfagilia Magufuli,lakini baada ya kuona vipi anafanya kila juhudi kuwanjima haki za msingi watanzania hapo nikamuona hana maana hata kidogo..

Katika historia Tanzania haijawahi kutokea watanzania kuwa na woga kama awamu hii,Nchi yoyote yenye raia wenye woga wa maisha haiwezi kupata maendeleo ya aina yoyote,nidhamu ya woga ni moja katika kitu kinacholeta umasikini kwa mwanadamu...

Watanzania ni watu wa kujituma,watu wa kujaribu mbinu tafauti katika kuleta maendeleo katika maisha yao,sijui humu ndani ya JF kama kuna anaefahamu hili neno Bongo limekujaje au nani kalibuni,kama mtataka kujua nitakufamisheni lakini kwasababu hii mada hausiano na hilo jina basi tupotezee tu..

Magufuli ilikuwa haina haja ya yeye kama raisi kuanza kubaguwa anaowatala,ilikuwa haina haja ya kuwanyanyasa watanzania walikuwa wana mawazo tafauti na yeye,yeye alikuwa anatakiwa akumbuke kuwa ni raisi wa watanzania wote,walio na mawazo kama yake na wasio na mawazo kama yake..

Ukianza kuwafanya unaoa watawala wabaguane,huwezi kuleta maendeleo katika nchi kama raia hawaendani,leo hii raisi anafika hadi kusema "hawa msiwavunjie ni wapiga kura wangu",Je raisi wetu ana tawala kwa visasi...,Mh Zitto ameshawahi kuwa Tanzania ina tawaliwa na washamba,hii ni kweli raisi wetu ni mshamba..

Mwalim Nyerere wakati wa utawala wake alikuwa anasisitiza sana utani miongoni mwa makabila ya watanzani,utani ni moja katika mila na jadi za waTanzania,utani unaleta maelewano katika jamii...

Raisi wetu Magu hataniwi ukimtania anakufunga,ukimwambia ukweli anakufunga,ukimkosoa anakufunga,raisi haambiliki,anaona anaowatawala ni wajinga mwerevu yeye peke yake,hivi sasa waTanzania hawataniani tena,waTanzania wameanza kuzungumza ukabila na udini...

Huyu raisi hafai kututawala watu wapole na wastarabu kama waTanzania.....,tutafutieni mwengine
 
  1. Kanunua ndege sita
  2. Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
  3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
  4. Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
  5. Ujenzi wq Hostel pale UDSM
  6. Nyumba za Magomeni Kota
  7. Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
  8. Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
  9. Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
  10. Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
  11. Nk nk
Aisee pamoja na yote uliyoainisha c sawa kwa kias hicho hilo la la umeme naomba usilisemee huku bora hata kipnd cha mgao kuna ttzo la umeme haswa...pia ununuz wa ndege na ujenz wa barabara hyo mwnge moroco...ni hatua nzur ila zinamsaidia vp mwananchi wa kawaida?kati ya wapanda ndege hapa nchin na wasiopanda wap wengi??....narudia ni hatua nzur ila hapa tuangalie masilah kwa wananchi kitaifa.
 
Back
Top Bottom