Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

ndio uzuri wa jf. waliyokula kiboko ya jpm wanapata mahali pa kupumua na kujifariji. lakini ukweli upende ukatae nchi imeanza nyoka. ufisadi uzembe na ubadhirifu vimepungua sana. hela ya umma hailiwi ovyo tena ndio maana wapiga dili wanalia kilio cha msiba huku kwenye mitandao.
Umetumia kipimo gani kujua ufisadi umepungua.
 
Sure, huwezi kufanikiwa kwa kumrudisha nyuma mwenzako na kumsimanga. Naona giza mbele huko tuendako. Kikwete is silently watching
 
Sijapata kuona Mtu anayeenda safari ya mbali kwenye njia yenye vikwazo vingi akajifunga kitambaa machoni na akafika salama! Serikali ile imeshindwa kutambua kuwa moja ya macho yake ni vyanzo vya habari na vyombo vya habari...tutarudi nyuma ya Square One tu...

Kama kumuunga mkono Bwana Yule ni kusema NDIYO basi tunaendelea kwa kasi ya hajabu hapajapata kutokea..........

Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
 
Hahaaaaa! Waliokwepa kodi hata miaka ya nyuma wanasakanywa na TRA, Wafanyakazi hewa wanafukunyuliwa, ...na mengine mengi, vipi kwa Mafisadi tuwasubiri wapya? 'Bussiness Unusual'😵😵

Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.

I think you have psychological problems. wewe unaona nchi inasonga mbele? hao wahujumu uchumi ni wanani kama siyo hilo lichama lenu lisilowahurumia watanzania? the country is going backward everyday
 
mbwembwe zote za mahakama ya mafisadi zimeishia wapi? hivi kuna wa kumfunga paka(fisadi) huko ccm? watakataje tawi walilolikalia? kama EPA ilimwingiza jk ikulu na huyu naye kaingizwa na ESCROW sasa unajifunza nini hapo? ccm ni ufisadi na ufisadi ni ccm. mkakati wa kuzuia bunge live ulilenga kuficha na kulea ufisadi,hii sheria ya mitandao ni mwendelezo uleule wa kuficha mafisadi
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Pamoja na mapungufu yanayojitokeza na yaliyojitokeza kwenye utawala huu sioni kama ni sahihi kufurahia kushindwa kwa juhudi za serikali katika kupambana na watu wanaoficha sukari , ujangili na uwindaji haramu, kuuza na matumizi ya dawa za kulevya na mengineyo yenye muelekeo huo.... juhudi za kupambana na hayo mambo kama zingefanikiwa na hata hivyo hazijashindwa kwakuwa sio rahisi kutokomeza ujangili au uuzaji wa madawa ya kulevya ndani ya muda mfupi...itachukua muda na kama serikali ikifanikiwa kudhibiti matumizi mabovu ya kodi za wananchi na rasilimali..naamini taifa hili litapiga hatua kwa kiasi kikubwa...hata kama serikali haitoweza kutokomeza kwa sasa naamini kutakuwa kuna misingi ambayo itakuwa imeachwa kwenye uwajibikaji
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Kama haitaji msaada wa mtu utamlazimiasha?....

mwache superman sie vilaza tumcheck akirun show...siku ikihitaji mawazo na ushauri wetu tutampatia.... namkumbuka jay mo the return I the superman....ahahaha....hawa kina Leo hawa huwa wanajoona superman balaa.

nchi ya watu mil 50 haiwezi kuongozwa na mawazo ya mtu mmoja anayeamini kuwa hakosei na haitaji kukosolewa unafhani malaika bana ....hata malaika wanakoseaga na mungu anawaadhibu yeye nadhani ni mungu ndio maana hakosei na hakoselewi.
 
Kukatw pumzihakuepukiki ikiwa kila kitu wewe pekee ndo unayejua
 
Pamoja na mapungufu yanayojitokeza na yaliyojitokeza kwenye utawala huu sioni kama ni sahihi kufurahia kushindwa kwa juhudi za serikali katika kupambana na watu wanaoficha sukari , ujangili na uwindaji haramu, kuuza na matumizi ya dawa za kulevya na mengineyo yenye muelekeo huo.... juhudi za kupambana na hayo mambo kama zingefanikiwa na hata hivyo hazijashindwa kwakuwa sio rahisi kutokomeza ujangili au uuzaji wa madawa ya kulevya ndani ya muda mfupi...itachukua muda na kama serikali ikifanikiwa kudhibiti matumizi mabovu ya kodi za wananchi na rasilimali..naamini taifa hili litapiga hatua kwa kiasi kikubwa...hata kama serikali haitoweza kutokomeza kwa sasa naamini kutakuwa kuna misingi ambayo itakuwa imeachwa kwenye uwajibikaji
Hakuna mtu anafurahia kushindwa kwa serikali bali tunamkumbusha tulivyokuwa tunamwambia ni vigumu kuibadili nchi bila kuuvunja mfumo uliojengwa kwa takribani nusu karne kwa kutumia watu walewale.
 
Unafikiri miaka mitano ni mingi leo hardly kabakiza 3yrs.

Kwa Tanzania ni ndoto kuzifikia nchi ulizozitaja kwa sababu hatuna sera za kitaifa bali tuna sera za vyama kiasi kwamba akiingia rais mpya anakuja na sera zake,

leo Magufuli ana sera ya viwanda kesho akiingia mwingine anaitupa analeta ya kilimo kwanza.

Ndugu yangu wala sio ndoto kuzifikia nchi nilizotaja.....with hardwork and commitment ya kila mwananchi inawezekana.

Pili sidhani kama uko sahihi sana unaposema kila kiongozi anakuja na sera zake na unavyotaja kuwa Magufuli kaja na sera ya viwanda.... ukweli ni kwamba Tanzania kama nchi ina mpango wake wa maendeleo wa miaka 15 ujulikanao kama Long Term Perspective Plan click hapo uuone na kuusoma Downloads | Long term perspective plans

Mpango huo ulizinduliwa 2011, na unakwenda hadi 2026. Ndani yake ndio inatoka mipango ya maendeleo ya miaka mitano.... kwa ufupi tu chini ya mpango huo miaka mitano ya mwanzo yaani 2011-2015 focus ilikuwa ni kuweka mazingira ya kukua kwa uchumi (unleashing latent potential for growth) ambapo mkazo ulikuwa ni kujenga miundombinu ya barabara na umeme....ndio maana kipindi hicho barabara nyingi zimejengwa na miradi ya umeme kubuniwa na kutekelezwa. Kuanzia 2016-2020 Focus ya mpango huo ni kujenga uchumi wa viwanda utakaotumia malighafi zinazozalishwa nchini.....ni kwa muktadha huo hata Ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2015 ikaji allign na mpango wa maendeleo wa Serikali yake wa kuweka mkazo kwenye maendeleo ya viwanda nchini....na hicho ndicho alichokinadi Magufuli nchi nzima na ndicho anachoendelea kufanyia kazi.....tumpe nafasi miaka mitano afanye kazi tuone matokeo.
 
Ndugu yangu mipango yetu huwa ni white paper tu ikiandikwa inawekwa kabatini hakuna wakufuatilia,

hata kama mpango wa viwanda ulikuwepo tangu 2011 kwa nchi yetu kila rais ana priorities zake, umeshamsikia Magufuli akigusia Kilimo Kwanza, je kilifanikiwa hadi asikikazanie, kama hakikufanikiwa unategemea viwanda anavyoanzisha vitatoa wapi malighafi.

Tanzania haina rod map yeyote ya kufikia hayo maendeleo unayoyatamani kila rais anayeingia anatumia trial and error method kutawala au nitoke vipi.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Hahahahhahahahahahahaahhahaahhhahahahahhahahahahaahhahahahahahahahahahhaahahahhaahhahahahahahahahahahahahahahahaha
 
Jibu hoja madawa ya kulevya yameisha au kamfunga nani? fisadi yupi kafikishwa mahakamani nk nk.
Hawa jamaa wagonjwa hasa. Wanatuaminisha kuwa sasa nchi imeshafikia uchumi wa kati. Maana hatuoni jitihada zozote, lakini wanatuambia mheshimiwa keshaweza kila kitu. Basi tuanze kutoa misaada kwa nchi maskini maana ndio lengo letu.
 
Back
Top Bottom