Tuambie faru john yuko wapi?. Mengine nakuuliza soon baada ya kujibu hili.Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Mungu aepushie mbali aisee. Japo tunahitaji kunyooka kidogo kwa kukumbatia laana na janga la nne katika taifa letu aka fisiem.Asubiri balaa la njaa linakuja mda si mrefu
changamoto huwa zinaisha?Kuhamia Dodoma imemshinda na huko kote unapodai kaleta mabadiliko bado kuna changamoto nyingi sana.
Ndugu yangu mipango yetu huwa ni white paper tu ikiandikwa inawekwa kabatini hakuna wakufuatilia,
hata kama mpango wa viwanda ulikuwepo tangu 2011 kwa nchi yetu kila rais ana priorities zake, umeshamsikia Magufuli akigusia Kilimo Kwanza, je kilifanikiwa hadi asikikazanie, kama hakikufanikiwa unategemea viwanda anavyoanzisha vitatoa wapi malighafi.
Tanzania haina rod map yeyote ya kufikia hayo maendeleo unayoyatamani kila rais anayeingia anatumia trial and error method kutawala au nitoke vipi.
Hizo document zako za ku google hazisaidii kama implementation ni sifuri, tunataka uonyeshe shamba kubwa tangible ambalo serikali imeli fund au inali-operate na kuwa mfano kwa secta binafsi, sio kutuambia to google.Huo ni mtizamo wako binafsi ambao hausindikizwi na ushahidi wa kutosha. Zaidi ninachoona tatiso la Msingi haujasoma hata hiyo Kilimo kwanza unayoililia na kudai Magufuli haitekelezi....
Nikusaidie.....click Kilimo kwanza - Google Search utaona kuna document inaorodhesha nguzo 10 za kilimo Kwanza........ ukipitia moja baada ya nyingine, utagundua Utekelezaji wa Kilimo kwanza ulishaanza kutekelezewa na hadi sasa unaendelea kutekelezwa.....hata hii industrialization drive inayoendelea sasa hivi ni NGUZO YA SABA ya kilimo kwanza....hivyo sio kweli kwamba Rais Magufuli ameacha kutekeleza kilimo kwanza......baadaye nitakupa evidence ya baadhi ya mafanikio ya kilimo Kwanza chini ya programu ya SAGCOT jinsi inavyowakomboa watanzania wengi kutoka kwenye umasikini. Ofcourse changamoto zipo....lakini hazifuti mafanikio
Kizazi cha kenge katika ubora wenu. Ukame ukija mnakata viuno kwa furaha mkiamini kuwa hata mvua iko upande wenu kisiasa.Asubiri balaa la njaa linakuja mda si mrefu
Hizo document zako za ku google hazisaidii kama implementation ni sifuri, tunataka uonyeshe shamba kubwa tangible ambalo serikali imeli fund au inali-operate na kuwa mfano kwa secta binafsi, sio kutuambia to google.
Usione uvivu kusoma Quinine...madhara ya kutosoma unaishia kutoa flimsy arguments based on hisia. Take time to read upate ufahamu mpana ili utoe uchambuzi au critique iliyo informed.
umetaka kujua tangiable results za kilimo kwanza/sagccot ninafurahi kushare nawe ila tafadhali uzisome usiishie njiani....maana ni ndefu kidogo.....
Ukisoma nguzo za Mpango wa Kilimo Kwanza ambazo nimekutumia utabaini programu ya SAGCOT ilianzishwa kutekeleza mpango huo.
SAGCOT ilianzishwa mwaka 2011 na wabia 20 (waliojumuisha makampuni madogo, ya kati na makubwa ya ndani na ya kimataifa; Serikali na Wabia wa Maendeleo).
Hadi mwaka, 2016, wabia wameongezeka na kufikia 105. Kati ya hao asilimia 75 ni makampuni binafsi. Wabia waliobakia ni Taasisi za Serikali, Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa na Taasisi zisizo za kiserekali (Non State Actors).
Hasi sasa SAGCOT imeweza kupata ahadi za uwekezaji zinazofikia U$ bilioni 1.20. Kati ya hizo asilimia 25 inawekezwa katika maeneo mbalimbli hususan katika uzalishaji wa mazao, uingizaji na usambazaji wa pembejeo, usindikaji wa mazao mbalimbali pamoja na masoko ndani na nje ya nchi.
Mazao yanayopewa kipaumbele ni mazao ambayo wadau wa SAGCOT wanayafanyia kazi. Hivi sasa mazao ya Mpunga, Soya, Horticulture (Mboga na Mtunda mbalimbali), Nyanya, Viazi Mviringo, Ufugaji wa Kuku na Ngombe wa Maziwa ni baadhi ya mazao ambayo yanapendelewa na Wabia katika uwekezaji.
SAGCOT imeanzisha Kongani ya Ihemi (Ihemi Cluster) inayohusisha mikoa ya Iringa na Njombe. Kupitia uzoefu uliopatikana katika kuendeleza biashara ya mazao ya kilimo katika Kongani hiyo, hivi sasa SAGCOT imeamua kuanzisha Kongani nyingine ambayo itapanua wigo wa shughuli zake hususan katika mikoa ya Morogoro au Mbeya.
Baadhi ya miradi ya kujivunia ambayo imewekezwa nchini kutokana na Ubia wa SAGCOT ni pamoja na:
(i) Kiwanda cha kusindika Nyanya - Mkoani iringa. Kinauwezo wa kusindika tani 200 za nyaya kwa siku. Ni uwekezaji wa US$ milioni 7.0
(ii) Mashamba ya Mbegu za Madhindi na Soya Hekta 3,000 na Kiwanda cha kusindika chakula cha kuku tani 70 kwa saa na kutotoa vifaranga vya kuku laki 3 kwa wiki. Uwekezaji huu upo Iringa.
(iii) Ufufuaji wa Shamba la Mbegu la Dabaga hekta 1,000. Tija katika shamba hilo imefikia wastani wa tani 8.5 za mahindi kwa hekta. Shamba hilo sasa ninawafikia wakulima wadogo 4,000 kwa lengo la kuongeza maradufu uzalishaji wa mahindi katika mashamba yao na pia kuazisha kilimo cha Soya. Jumla ya US $35 milioni zimewekezwa na uwekezaji unaendelea
(iv) Ujenzi wa mitambo na maghala ya kuhifadhi mbolea Kurasini Dar es Salaam ambapo jumla ya US$ 25 milioni zimewekezwa
(v) Shamba la mpunga la Kilombero lenye ukubwa wa Hekta 5,000 limeendelezwa lote na moja ya mashamba makubwa ya mpunga barani Afrika. Jumla ya UD$ 65 milioni zimewekezwa katika shamba hili. Aidha, jumla ya wakulima wadogo 7,000 wamenufaika na utekelezaji wa kilimo bora cha mpunga ambapo tija katika uzalishaji kwa wakulima hao imeongezeka kutoka chini ya tani 1.0 za mpunga kwa hekta hadi tani 5.6 kwa hekta.
Aidha, jumla ya $ 0.6 zimewekezwa katika mkoa wa Njombe kwa ajili ya kufundisha wakulima wadogo mbinu bora za kilimo cha viazi mviringo. Aina bora 8 za mbegu za viazi zimeandikishwa nchini. Juhudi hizi zinalenga kupata uwekezaji usiopungu US$ 150 kwa ajili utafiti na usindikaji wa zao la viazi mviringo.
Hadi sasa inakadiriwa kuwa jumla ya wakulima wadogo 50,000 wananufaika kwa viwango mbalimbali kutokana na utekelezaji wa mpango huu wa SAGCOT
Aidha, taasisi za fedha, wawekezaji wa zana za kilimo na madawa ya kudhibiti visumbufu wameongeza ajira na kufungua matawi hapa nchini na pia kuajiri wafanyakazi wataalam ambao hivi sasa wanahudumia wakulima.
Aidha, katika ngazi ya kimataifa, SAGCOT iliweza kuwa chachu muhimu katika uandaaji wa mpango wa Serikali ya Marekani ya FEED THE FUTURE na baadaye barani Afrika unatekelezwa mpango wa GROW AFRICA ambao unahisha takriban nchi 12 . Nchi hizo kwa kiwango mbalimbali zinatekeleza utaratibu ambao kwa sehemu kubwa wamejifunza kutoka mpango wa SAGCOT. Kutokana na mafanikio ya mpango huo. Mwaka huu, nchi za bara la Asia wamenzisha mpango wao wa GROW ASIA.
na bado mkuu.Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.
Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.
Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.
Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.
Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.
Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.
Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.
Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.
Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.
Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.
Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.
Naomba kutoa hoja.
Quinine.
Rais gan toka aingie madarakan nchi imekumbwa na majanga had mvua zimegoma kunyesha,amelaaniwaAsubiri balaa la njaa linakuja mda si mrefu
Lake mtu halimtapishi!
- Kanunua ndege sita
- Ujenzi wa Reli ya Kati kwq Standard Gauge
- Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Uganda hadi Tanga
- Kudhibiti ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma
- Ujenzi wq Hostel pale UDSM
- Nyumba za Magomeni Kota
- Kupandisha bei ya korosho kutoka shilingi 1000 hado 4000
- Ujenzi wq Barabara ya Mwenge hadi Morocco
- Ununuzi wa Meli mpya Ziwa Tanganyika na Victoria
- Umeme wa uhakika. Hakuna mgawo kwa sasa
- Nk nk
Povu jingiNi kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.