Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Nilijua huu Uzi umeanzishwa na BAVICHA kwa lengo la BAVICHA kujitokeza kutoka mafichoni na kuja kulalamikia hapa Jf.. Kweli mmekamatwa sana.
 
Kilichomshinda na kitamtia Aibu ni kuhamia Dodoma, ni vigumu sana na siku akihamia itakuja muujiza wa ajabu yaani utaoshangaza watu Duniani
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
Wapi Lugumi? Wapi mnunuzi wa Kivuko chakavu? Wapi wanunuzi wa mabehewa? Wapi ilipo chenji ya Rada? Chenji ya bunge la katiba? Zipo wapi pesa za kiwanda hewa kule Lindi?
 
Hayo ni yako. Haya hujayaona?

Ununuzi wa ndege
Ujenzi wa reli
Elimu bure
Nidhamu makazini
Kuwajali masikini
Nafuu ya maisha
Kujitegemea
Kuwathibiti mafisadi
Kurejesha mashamba


Acha porojo wewe. Waswahili husema ukiona manyoya ujue keshaliwa. Ukiona mtu anaandika hayo uliyoandika ujue amekamatika katika mojawapo.
Kuhamia Dodoma imemshinda na huko kote unapodai kaleta mabadiliko bado kuna changamoto nyingi sana.
 
Hakika akiweza kuhamia Dodoma tu ajue vingi ataviweza lakini akifeli kuhamia Dodoma kila kitu atafeli.
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Hayo ni mawazo ya watu waliopigwa kwenye Box la kura.
 
Toto lililo jinga kupindukia no like linalifurahia kusikia baba yake hana pesa ya kumlipia ada. Na hii ndio alili ya waunga mkono hoja hii.
 
Ni kwa waliopungukiwa maarifa tu ndo wanaoweza kuunga mkono hoja hii ya hovyo. Ka una maarifa timamu huwezi kuleta hoja hii ukafikiri ndo jambo jema kwa nchi na kwamba tulishabikie hapa JF. Sisi kama watu waungwana yatupasa kumuunga mkono mheshimiwa raisi kuhakikisha nchi inakaa kwenye mstari na inakuwa na maendeleo chanya na si kumdhihaki na kuonyesha juhudi zake ni bure na kwamba nchi iendelee kuendeshwa hovyohovyo kwa kuendekeza wahujumu uchumi, wauza madawa ya kulevya, mafisadi na majanga mengineyo ktk nchi.
mnaweka raia mahabusu bila makosa afu mnsema muungwe mkono? that's a joke.
 
ni kweli naona yamerudi yale yale, teuzi za kirafiki, meri ya bagamoyo, faru john, madawa bado hajakomesha, umeme wanakata bila taarifa kweli tumerudi kwa kasi ya ajabu.
 
Five Years my friend, kuwa na subira.. Mabadiliko ni kazi isiyo ya lele mama. Kwote tunakosifia leo wamepiga hatua China, Vietnam, Singapore,Indonesia, na nchi zinazochipukia hivi sasa Ethiopia, Rwanda nk zimepitia changamoto kubwa zaidi ili kufika walipofika....
Dira hakuna Mzee, walichora ramani wakaanza kuitumia siyo mambo yetu hayo, wanasiasa ndiyo wanaamua mambo ya kitalaamu, kila siku matamko yasiyo na lengo, Jk alikuwa anajenga taasisi, yeye afanye monitoring tumalize kazi siyo mambo hayo ya kuua mede kwa SMG, We need wide scope. Giza Giza tupu, mulika labda utaona. Nguvu ya taasisi ndiyo inayojenga Rwanda.
 
Back
Top Bottom