Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Rais kaishiwa pumzi, karudi square one

Punguza upuuzi nyie ndo mnakua wa kwanza kusema raisi haongozi nchi vzr...afu unatuletea pumba zako hapa eti ameshindwa....kwa hiyo mliomba ashindwe ili mpate cha kuongea....nyie msio jielewa ndo mnaona tumerudi kulekule....lakin kwa wenye timamu wanajua nidhamu iliyopo kwa taasisi za serikali...na huduma zinavotolewa bila ubaguzi...sasa nyie kazeni kuomba ashindwe...mwisho mtashindwa nyie...maana hadi 2025 mtakua mmenyooka..

Wewe unaumwa na tumbo sio bure! Haya nenda ukaharishe kisha ulale! Ni wapi niliposema kwamba namwombea ashindwe? Mimi nimesema matumaini ya watu yanaanza kuyeyuka kwa sababu hawajaona wahujumu wa kweli wakishughulikiwa, mafisadi na wauza madawa ya kulevya wakishughulikiwa! Watu wanatumbuliwa halafu baada ya siku kadhaa watu wale wale wanateuliwa tena kwenye nafasi nyingine! Hayo ndio aliyoahidi kwenye kampeni zake? Hatumwombei ashindwe bali tunataka afanye kweli, sio usanii wa kisiasa!!!
 
Mwisho wa siku kila kitu kitarudi pale pale hata na kuzidi. Tusubiri kuona matumizi makubwa ya takrima kuliko ilivyokuwa awali.
 
Siasa za wazungusha mikono ni kufurahia mambo yanapoenda mrama ili wapate cha kusema. Nilichongundua kuwa mtaji wa wapinzani wa Tanzania ni matatizo ya wananchi wanapoona matatizo ya wananchi yanatatuliwa huona kuwa kibarua chao kiko matatani. Ndio wapinzani tulionao.

Kwa hiyo na wewe unawakosoa wapinzani kwa sbb umepata cha kukosoa?

Ni mwendo wa kukosoana tu, wapinzani wanawakosoa na nyie mnawakosoa wapinzani.....
 
Ukitawaliwa na mawazo ya siasa hadi katika mambo mazito ni dhahiri kuna dalili za kuelekea kuwa kochaa au mwehu kamili.ni ndoto tu.
Kuna gazeti limeandika mkuu, sio maneno yangu hayo! Jamaa anaonekana kwa marafiki zake according to hilo gazeti!
 
Kila kitu alichodhani atakirekebisha kimeanza kurudia hali yake ya zamani.

Moto wa kupambana na mafisadi ni kama umezimika baada ya kuambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi, tumerudi palepale.

Wakati anaingia alikuta TRA inakusanya bn 900 hadi tn1, yakaongezeka hadi tn1.5 leo yamerudi kule kule bn 900 sijui ya Nov inawezekana yameshuka zaidi.

Spidi ya kubomoa nyumba zilizojengwa mabondeni na kinyume cha sheria ulianza kwa mkwara ukapiga breki kwa mama Lwakatare, leo tumerudi kule kule.

Machinga ni vurugu mechi, ondoa rudisha ondoa, tatizo halijatatuliwa limebaki palepale.

Tumbua tengua teua mwisho tumeishia kuteua walewale tuliowatumbua hatuja solve kitu tumerudi kule kule.

Mikopo ya wanafunzi sio tu tumerudi tulipokuwa yaani square one bali hata uwezo wa serikali kulipa umepungua kulinganisha na serikali iliyopita.

Serikali imeshindwa hata kuajiri na kupandisha madaraja watumishi wake, ni kama tumerudi square one.

Alipoingia alizuia safari za nje akazuia sikukuu za kitaifa, leo watumishi wanasafiri kama kawaida na juzi tumesherehekea sikukuu ya Uhuru aliyoikataa mwaka jana, mambo yamekuwa business as usual.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni kama ndiyo yamezidi, pamoja na ahadi ya serikali yake kutatua kadhia hiyo ni kama tumerudi kule kule.

Kuna mengi ambayo alidhani rahisi kuyafanya yameanza kumshinda mfano, sukari ya Bharesa, pembe za ndovu, madawa ya kulevya, majangili. Nina uhakika anaweza kumaliza muda wake akayacha kama alivyoyakuta.

Naomba kutoa hoja.

Quinine.
Waulize vizuri wazee wa faru Joni,, watakwambia kama wamerudi square one au moto unawawakia
 
Alipofanya figisu na kumtoa Mramba na Yona jela mwanzoni kabisa nikajua tu kushnehi, hakuna cha kupambana na ufisadi au mjomba wake ufisadi!
Mali zao zingekuwa seized na wangefungwa haswaaaa vizuri. ..sikuelewa kuachiwa kwao.
 
Waulize vizuri wazee wa faru Joni,, watakwambia kama wamerudi square one au moto unawawakia
Nakuhakikishia moto wa faru John utazimwa kama mshumaa, kama ni mfuatiliaji wa mambo yuko wapi masamaki, mpemba, flow meters, ICDs, haroon mulla, makontena, watu wanapiga dili kama kawaida,

kama hao wote wameonekana hawana hatia watashindwa ya faru john tutaambiwa alikufa basi end of the story.
 
.... mambo yatakuwa sasa tu ngoja tunyooshe inji... kwi kwi kwi...iiiiii
 
Bado kuna mazuri mengi mfano ni elimu bure, ajira walimu wa sayansi ,kufufua ATCL

Katika yote nimependezwa na utekelezaji wa kazi Sera ya ardhi ktk mikoa mbalimbali
Jitoe ufahamu tu
Mfupa uliomshinda fisi kibogoyo atauweza kweli?? Tatizo la nchi hii ni ccm kufilisika kwa mawazo mapya magu lazima atashindwa tu kupambana na mfumo uliompa madaraka.
 
Mkuu Amesahau Kusali ROZARI ndo maana mafanikio yana rudi back.
ngoja nikamkumbushe ROZARI yake nahc atakuwa amesahau.
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Kumbe ilikuwa ni Mahakama ya Vibaka na sio Mafisadi. Ndio maana tuiona Escrow, Lugumi na Meli Chakavu zikipotezewa.
 
USIJALI RAIS WETU MPENDWA,JPM.TUNAOKUUNGA MKONO KWA KAZI YAKO NZURI TUPO WENGI SANA INGAWA HATUNA MANENO MENGI.TUNAKUOMBEA KWA MUNGU WA T.B.JOSHUA AENDELEE KUKUSIMAMIA NA KUKUONGEZEA HEKIMA.NINATAMANI BAADA VIPINDI VYAKO VIWILI(2) VYA MIAKA 10 KATIBA IBADILISHWE UTAWALE TENA MIAKA MINGINE 10 YA ZIADA.HAPO NDO TUTAKUWA TUMEFAIDI VIZURI MATUNDA NA MATOKEO YA UONGOZI WAKO MZURI ULIOTUKUKA.UBARIKIWE,JPM.
 
Ubuyu huo, shilawadu tumerudi mule mule Kama TFF ilivyo rudi enzi ya ndolanga
 
Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
Juzi tuu wabunge wa kijani walimegewa mijihela ili kupitisha ule mkandamizo... Au ulikuwa ughaibuni mwenzetu..? Naongopa ?

Sent from mTalk
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Si jambo ya kusherekea/kufurahia kisa tabiri zetu zinatimia bali la kusikitikia na kulitatua kwani mengi yanagusa maisha yetu na kututesa kama sio wenyewe bali wapedwa wetu

Tanzania, nitaipenda na kuilinda hadi kikomo cha uwezo wangu.
 
Vibaka na mafisadi wengine hawa hapa. Acha kuandika uongo Mkuu. Mafisadi na Vibaka wa CCM wamenyooka kuanzia lini!?



Mahakama ya mafisadi itafanyaje kazi wakati vibaka wote mmenyooka? Thats the whole point....unapaswa kulalamika ikiwa ufisadi unaendelea huku watuhumiwa hawafikishwi mahakamani
 
Back
Top Bottom