Rais Hakainde Hichilema amuapisha askari aliyemtendea wema akiwa gerezani kuwa naibu kamishna wa Magereza

Huyo Rais naye hana akili, hauwezi teua cheo kikubwa hivyo kwa sababu askari wa cheo cha chini alikutendea wema, chagua kutokana na uwezo wa mtu sio mahaba yake.
Sio kuwa alimtendea wema kwa maana ya favors bali alikuwa akifanya kazi professionally following rules, regulations and guidelines bila uonevu wa kukomoana kwa sababu either za kisiasa au unyama tu usiozingatia human rights mambo ambayo HH aliona ni wema wa hali ya juu kwa askari magereza yule kuwa kwenye mstari ulionyooka wakati serikali ilikuwa kandamizi na askari wengi wakifanya kazi kwa mihemko ya kukomoa watu.
 
Kwa upinzani huu ambao unapigania matumbo yao. Sahau kabisa swala la wapinzani kushinda uraisi miaka hii kumi au ishirini ijayo, kwanza hawana wagombea wa kuwawezesha kushinda hata ubunge, achilia mbali uraisi. Labda muazime kama mlivyoazima mwaka 2015. Hichelema hakutumia ujinga huu waliotumia hao wapinzan wenu mwaka 2015 ndio maana kashinda uraisi maana wananchi walimuamini kwa anachosimamia. Sio kigeu geu kama wapinzan njaa wenu. Hata ukitizama sura za wapinzani wa Tanzania na huyo Hichilema utaona tofauti kubwa ya kiuongozi kati yao. Wapinzani wa Tanzania sura zao zinaonekana zipo kimasilahi zaidi wakati wa Zambia sura yake imekaa kimageuzi mageuzi na yenye muonekano wa kuwajali watu wake.

View attachment 1922946

View attachment 1922949

View attachment 1922954
Even Hakainde Hichilema was mocked and ridiculed, he had his highs and lows na hata mwanzilishi wa UPND late Anderson Mazoka aliteswa na Frederick Chiluba na aliporwa ushindi katika kinyang'anyiro cha urais na baada ya kufariki HH akapokea mikoba kuendeleza 'libeneke'. Kwenye siasa huwa kuna ridiculous fanatics na huwa wanatambulika kwa mitazamo yao lakini huwa haibadilishi realities on the ground, Kibongobongo upumbavu uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi pamoja na vyombo vya dola ndicho kilichoturudisha nyuma na kutusababishia kufika hapa tulipofika.
 
Njia ya Mungu ni fumbo

RAIS HAKAINDE HICHILEMA AMUAPISHA ASKARI ALIYEMTENDEA WEMA AKIWA GEREZANI KUWA NAIBU KAMISHNA WA MAGEREZA. KUNA SOMO LA KUJIFUNZA

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameteua Bwana Kuyomba Bwalya kuwa Naibu Kamishna Jenerali wa magereza "Zambia Correction Service".

Hichilema aliwekwa 2kizuizini katika mahabusu gerezani chini ya Askari kijana mdogo anayeitwa Bwalya mwaka 2017, ambapo alibambikiwa mashtaka ya uhaini " treason" akituhumiwa kutaka kumuua Rais wa Zambia wakati huo Edgar Lungu.

Kiongozi huyo wa Upinzani wakati huo, alibambikiwa mashtaka ya uhaini kwa kile Jamhuri ilichodai kuwa alikataa kuupisha msafara wa Rais Edgar Lungu ambapo upelelezi ulidai kuwa ulibaini kuwa lengo la Hakainde ilikuwa kumuua Rais Edgar Lungu kwa ajali ya gari.

Hakainde aliachiwa HURU baada ya kusota gerezani kwa takribani miezi minne baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kumfutia mashtaka hayo kutokana na Jamhuri kukosa ushahidi wa kudhibitisha uhaini aliokuwa anatuhumiwa nao.

Wakati Rais Hakainde akimuapisha Bwalya na maafisa wengine juzi Jumatano, Rais alimsifu Bwalya kwa kufanya kazi kwa weledi uliotukuka na kuzingatia Sheria na Katiba licha ya mazingira magumu ya utawala kandamizi na unyanyasaji wa utawala dhalili, dhalimu na katili wa Rais Edgar Lungu.

Rais Hakainde amemuamuru Kamishna Jenerali Fredrick Chilukutu na Naibu Kamishna Jenerali Bwalya wa huduma za kitaifa za kubadili tabia kuyafanyia mageuzi makubwa magereza yote nchini Zambia.

"Kipekee nizungumze na nyinyi ndugu zangu wawili wa huduma za kurekebisha tabia katika magereza yetu" alisema 2Rais Hakainde

“Mimi ni mhitimu wa taasisi hiyo (magereza) na ninajua kabisa kinachoendelea katika taasisi hiyo. Wanapaswa kuwa vituo vya marekebisho ya tabia, kwa sasa sio bali magereza yamegeuka kuwa vituo vya mateso, unyanyasaji, udhalilishaji na mauaji. Mazingira ya magereza ni magumu na mabaya sana kwa sisi mahabusu, kama mahabusu wa zamani natuma ujumbe kwenu kwamba uteuzi wenu haukuwa wa bahati mbaya, niliteua kwa makini sana kwa kuzingatia ndoto na sera yetu ya kuliunganisha na kuliponya Taifa hili na hili nitalisisitiza katika kila sherehe za uapisho kwa wateule wapya ili tuweze kutoka katika siku za kutengwa hadi siku za kujumuishwa lakini zaidi kwako hakikisha unayafanyia mageuzi makubwa sana magereza yetu ili yawe vituo vya kurekebisha tabia na sio vituo vya mateso." Rais Hakainde

"Nawaamuru mkaondoe msongamano katika mahabusu na magereza. Kama mhitimu katika mahabusu na magereza yetu ninafahamu kwamba kila sero " cell" ilijengwa kwa ajili ya kuweka mahabusu 20 pekee lakini kwenye sero ambayo Mimi niliwekwa mahabusu tuliishi watu 170 kwa wakati mmoja, kama una UTU na ubinadamu unaweza kuelewa aina ya mateso Mimi na mahabusu wengine wanayopitia katika Taifa hili. Haiwezekani Wazambia tusishi katika Taifa HURU kwa mateso makali kuliko hata kipindi cha ukoloni kabla ya UHURU sasa huu UHURU utakuwa na faida gani? Hebu fikiri hapa katika hii sero usiku ukiingia kila mtu anataka alale, unalala wapi na vipi, hakuna sehemu ya kulala, hakuna usingizi katika sero zetu, mahabusu wanateseka sana" amehoji Rais Hakainde

"Sikujua kuwa siku moja ningetupwa gerezani na ninyi nyote hapa hakuna anayejua hatima yake, huenda hata wewe kamishna general na Naibu kamishna general kesho mkawa mahabusu je mtajisikiaje kuishi katika sero na magereza zenye mateso makali namna ile?" Anaendelea kuhoji Rais Hakainde

"Bwalya ni kijana mdogo, tulikutana katika hayo mazingira magumu niliyowaeleza. Alikuwa boss wangu. Licha ya Mazingira hayo magumu ya utawala kandamizi wa Rais Edgar Lungu lakini bado alihakikisha anafanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria, Katiba na kiapo." Ameongeza Rais Hakainde

"Bwalya anafahamu kile ninachokiongelea, na Mimi ninakifahamu kile ninachokisema. Ndiposa nikatazama na kujiuliza huyu kijana mdogo kabisa anawezaje kutenda HAKI na kufikiri sawa sawa katika mazingira ya utawala wa dhuluma na kandamizi namna ile? Bwalya alikuwa boss wangu nilipokuwa nimetupwa mahabusu gerezani. Nilifahamika zaidi kwa sababu wakati mwingine sikukubali baadhi ya amri ambazo niliona zinaenda kinyume na HAKI zangu za binadamu. Lakini huyu kijana alinielewa alijua ipi ni sahihi na ipi sio sahihi. Alikuwa boss wangu na leo anaapishwa na mmoja wa mahabusu wake. Maisha yanabadilika, maisha yanazunguka. Meza imepinduka. Alimalizia Rais Hakainde.

Kuna somo muhimu sana hapa. Jifunze kutenda wema siku zote uwe huna madaraka au una madaraka wewe mtendee wema kila mtu, huwezi jua kesho inaleta nini kupitia wema au ubaya wako.

Usimuonee mtu maana yawezekana hata wafungwa na mahabusu unaowaonea leo huko magerezani kesho mmoja wapo akawa boss wako.

Watu unaowaonea na kuwatesa leo ukiwaona wao sio lolote na sio chochote huenda kesho wakawa ni msaada mkubwa na wewe ukawa miongoni mwa wanaohitaji msaada wao.

Usimdharau mtu yeyote kwa sababu tu ya hali yake ya leo ukilinganisha na hali yako. Heshimu kila mtu maana hujui kesho unayemdharau atakuwa wapi na wewe unayejiona umefika utakuwa wapi.

Tumia madaraka, cheo chako, fedha zako na Elimu yako kuunganisha watu, kusaidia watu, ufanyike furaha na tabasamu katika nyuso za waliopoteza furaha maana kesho ipo na hujui inakuja na maajabu gani.

Ubaya HAUFI na wema HAUFI na kumbuka wema na ubaya vyote ni mbegu ambayo humea kwa wakati muafaka.

Zaidi sana usisahau kuwa kuna kitu kinaitwa Karma! Huyu jamaa huwa hamsahau mtu hata kama itachukua muda gani. What goes around comes around. Ukitenda ubaya UTALIPWA MABAYA na ukitenda wema UTALIPWA MEMA kwa saa, njia na wakati usioutarajia.

Usipande miba katika njia yangu maana huenda kesho ukalazimika kuipita njia yangu ukiwa huna viatu.

Rais Hakainde Hichilema aliapishwa kuwa Rais wa Zambia baada ya kumshinda Rais Edgar Lungu kwa ushindi wa kishindo. Hakainde alichaguliwa kuwa Rais baada ya kugombea mara 5 bila mafanikio. Hapa pia liko somo la kutokukata tamaa, ukishindwa jaribu tena na tena na tena hadi utakapofanikiwa.

Wema unalipa, tenda wema nenda zako
Kwa hiyo sasa anawapa watu vyeo kwa kulipa fadhila?
 
Kwahiyo wabunge wa ccm wanapigania wananchi?
Kilo ya nyama sasa hivi ni 8500. Juzi kati tu nilinunua kwa 6000.
Vipi kuhusu miala ya simu? Kwa uongozi mzuri wa CCM. Ukitumiwa 5,000 kwenye simu. Ukienda kwa wakala. Unatoa 4900. Wanakata 100 tu.
Mafuta yameshapanda bei. Sasa hivi wamebakiza kuuza nchi tu watu waende wasikojulikana.
Mpk ifike 2022. Tutaheshimiana tu.
Nyama lazima iwe anasa tu.
Watu tunaangalia mambo ya msingi yaliyofanywa, yanayofanya na yatayofanywa na serikali kama vile kujenga shule nying zaidi nchini kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wetu, kujenga hospital nyingi zaidi kwa ajili ya afya zetu na za watoto wetu, pia kuhakikisha kina mama hasa wanaojifungua hawatembei umbali mrefu sana kufuata huduma za matibabu, kujenga barabara nyingi zaidi ili kuwarahisishia wakulima waweze kuingia mijini kuuza mazao yao kwa haraka zaidi na kujipatia riziki zao, kuongeza huduma za upatikanaji wa maji na umeme nchi nzima nk. Swala la kupanda bei nyama au baadhi ya bidhaa liko karibuni dunia nzima kwa sasa kutokana na madhara ya corona (hii ni kwa mtu mwenye akili timamu na asieendekeza mahaba ya siasa uchwara ndio atanielewa) na sio tu Tanzania au Afrika peke yake. Ukiona swala la kula nyama lina umuhim sana kwako zaidi ya ujenzi wa hizo hospital, shule, barabara nk basi fuga ng'ombe wako mwenyewe.
 
Miaka 50+ bado serikali ya CCM inahangaika na kujenga shule na hospitali?
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
Katika maisha tunaangalia hivi vitatu
1. Food
2. Shelter
3. Clothes
Km hivyo vitatu huwezi kuvimudu hata gharama za hospital na shuleni huwezi kuzimudu. Mtu mjinga ndiyo atakuelewa
Km hapo huwezi kumudu kununua kilo ya nyama ya 8500 hizo gharama za matibabu utaziweza?
Hospitali za serikali kumuona daktari ni 5,000. Bado matibabu ushajiuliza ni shiling ngapi? Km nyama kwako siyo kipaumbele, endelea kula matembele huku madaktari wanasisitiza angalau kwa wiki 1 unatakiwa ule angalau vipande 2

Watu tunaangalia mambo ya msingi yaliyofanywa, yanayofanya na yatayofanywa na serikali kama vile kujenga shule nying zaidi nchini kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wetu, kujenga hospital nyingi zaidi kwa ajili ya afya zetu na za watoto wetu, pia kuhakikisha kina mama hasa wanaojifungua hawatembei umbali mrefu sana kufuata huduma za matibabu, kujenga barabara nyingi zaidi ili kuwarahisishia wakulima waweze kuingia mijini kuuza mazao yao kwa haraka zaidi na kujipatia riziki zao, kuongeza huduma za upatikanaji wa maji na umeme nchi nzima nk. Swala la kupanda bei nyama au baadhi ya bidhaa liko karibuni dunia nzima kwa sasa kutokana na madhara ya corona (hii ni kwa mtu mwenye akili timamu na asieendekeza mahaba ya siasa uchwara ndio atanielewa) na sio tu Tanzania au Afrika peke yake. Ukiona swala la kula nyama lina umuhim sana kwako zaidi ya ujenzi wa hizo hospital, shule, barabara nk basi fuga ng'ombe wako mwenyewe.
 
Even Hakainde Hichilema was mocked and ridiculed, he had his highs and lows na hata mwanzilishi wa UPND late Anderson Mazoka aliteswa na Frederick Chiluba na aliporwa ushindi katika kinyang'anyiro cha urais na baada ya kufariki HH akapokea mikoba kuendeleza 'libeneke'. Kwenye siasa huwa kuna ridiculous fanatics na huwa wanatambulika kwa mitazamo yao lakini huwa haibadilishi realities on the ground, Kibongobongo upumbavu uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi pamoja na vyombo vya dola ndicho kilichoturudisha nyuma na kutusababishia kufika hapa tulipofika.
Usikwepeshe upumbavu na ujinga uliofanywa na upinzani mwaka 2015 kwa kukubali kutema big jii (dr Slaa) kwa sababu ya chapati ya kuonjeshwa (Lowasa) Mwaka 2015 kila mtu alikuwa tayari kwa mabadiliko na hakika kama wapinzani wangesimama imara bila wenyeviti wa ukawa (Mbowe, Mbatia na magenge yao) kuvuta hela na kurubuniwa na mbinu za CCM basi wangeshinda mchana kweupee. Since kipindi kile watu wengi wameiona Chadema na vyama vingi vya upinzani kuwa ni wababaishaji tu wanaopigania matumbo yao. Ni afadhali katika uchaguzi ule kwa upande wa uraisi wangemuachia dr Slaa au wangempitisha mtu mungine ambae hana kashfa nzito kama zile walizomvika wao wenyewe Lowasa. Yeye Lowasa angeshawishiwa agombee kwanza ubunge, lkn kwa vile jamaa walikuwa na tamaa ya pesa kwa ajili ya kwenda kula bata Dubai na Afrika kusini wakaamua bora wauze ile nafasi ya uraisi kwa fisadi ili agombee (hata kama watakuwa wamewa disappointed wapenda mabadiliko wa ukweli) ilimradi wao tayari mambo yao yatakuwa yanawaendea vizuri kutokana na mamilioni ya shilingi waliyopewa. So kumfananisha mtu anaesimamia kile anachokiamini mh Hichilema na hawa wazee wa fursa ni kujiaibisha tu bure.
 
Huyo Rais naye hana akili, hauwezi teua cheo kikubwa hivyo kwa sababu askari wa cheo cha chini alikutendea wema, chagua kutokana na uwezo wa mtu sio mahaba yake.
Mkono wa Mungu ukiwa juu ya mtu, haijalishi elimu yake mkuu
 
Huyo Rais naye hana akili, hauwezi teua cheo kikubwa hivyo kwa sababu askari wa cheo cha chini alikutendea wema, chagua kutokana na uwezo wa mtu sio mahaba yake.
Naona hujawaelewa somo, unasoma tu kama kasuku lakini huwezi kuelewa ndio maana kwa uelewa wako huo mdogo unafikiri huyo askari magereza alikuwa akimpendelea bwana HH alipokuwa mahabusu.

Jaribu kuuliza walioelewa wakueleweshe, uwe free tu kuuliza, nimeona wa kama wewe wamo humu hauko peke yako.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Km tukiangalia pande zote kumbe inawezekana hata wale covid19wanaobezwa siku moja wanaweza wakawa vinara wa CDM meza hugeuka tuweke akiba ya maneno
 
Ili kuepusha kisa kama hiki, nahisi, ndio maana kuna time vifungu fulani fulani vya katiba husimamishwa
 
Usikwepeshe upumbavu na ujinga uliofanywa na upinzani mwaka 2015 kwa kukubali kutema big jii (dr Slaa) kwa sababu ya chapati ya kuonjeshwa (Lowasa) Mwaka 2015 kila mtu alikuwa tayari kwa mabadiliko na hakika kama wapinzani wangesimama imara bila wenyeviti wa ukawa (Mbowe, Mbatia na magenge yao) kuvuta hela na kurubuniwa na mbinu za CCM basi wangeshinda mchana kweupee. Since kipindi kile watu wengi wameiona Chadema na vyama vingi vya upinzani kuwa ni wababaishaji tu wanaopigania matumbo yao. Ni afadhali katika uchaguzi ule kwa upande wa uraisi wangemuachia dr Slaa au wangempitisha mtu mungine ambae hana kashfa nzito kama zile walizomvika wao wenyewe Lowasa. Yeye Lowasa angeshawishiwa agombee kwanza ubunge, lkn kwa vile jamaa walikuwa na tamaa ya pesa kwa ajili ya kwenda kula bata Dubai na Afrika kusini wakaamua bora wauze ile nafasi ya uraisi kwa fisadi ili agombee (hata kama watakuwa wamewa disappointed wapenda mabadiliko wa ukweli) ilimradi wao tayari mambo yao yatakuwa yanawaendea vizuri kutokana na mamilioni ya shilingi waliyopewa. So kumfananisha mtu anaesimamia kile anachokiamini mh Hichilema na hawa wazee wa fursa ni kujiaibisha tu bure.
Hichilema amepitia kila aina ya dhoruba, hizo rubbish ulizozijaza hapa zisizo na proof na ku-display ujinga na ni ushabiki mandazi kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Lowasa na Slaa are one and the same, opportunists. Miscalculations ndiyo ziliwapoteza opposition parties wakidhani popularity ya Lowasa ni added advantage lakini kama HH ame-battle kwa kipindi kirefu basi kinachotakiwa ni kuzidi kupambana pasina kukata tamaa.
Siasa huwatoa watu ufahamu na kuandika ujinga wa story za vijiweni kudhihirisha, Gwajiboy alidai(back then) kuwa kilichomtoa Slaa opposition side ulikuwa ni uamuzi wa mke wake ambaye ambition yake ilikuwa ni kuwa first lady hivyo baada ya kuona mumewe si mgombea urais akamuamuru mumewe wahame ni si blah blahs nyinginezo(hii ni kama Gwajiboy hutoa kauli za kuaminika).
 
Kwahiyo wabunge wa ccm wanapigania wananchi?
Kilo ya nyama sasa hivi ni 8500. Juzi kati tu nilinunua kwa 6000.
Vipi kuhusu miala ya simu? Kwa uongozi mzuri wa CCM. Ukitumiwa 5,000 kwenye simu. Ukienda kwa wakala. Unatoa 4900. Wanakata 100 tu.
Mafuta yameshapanda bei. Sasa hivi wamebakiza kuuza nchi tu watu waende wasikojulikana.
Mpk ifike 2022. Tutaheshimiana tu.
Nyama lazima iwe anasa tu.
Tenda wema uondoke
 
Hichilema amepitia kila aina ya dhoruba, hizo rubbish ulizozijaza hapa zisizo na proof na ku-display ujinga na ni ushabiki mandazi kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Lowasa na Slaa are one and the same, opportunists. Miscalculations ndiyo ziliwapoteza opposition parties wakidhani popularity ya Lowasa ni added advantage lakini kama HH ame-battle kwa kipindi kirefu basi kinachotakiwa ni kuzidi kupambana pasina kukata tamaa.
Siasa huwatoa watu ufahamu na kuandika ujinga wa story za vijiweni kudhihirisha, Gwajiboy alidai(back then) kuwa kilichomtoa Slaa opposition side ulikuwa ni uamuzi wa mke wake ambaye ambition yake ilikuwa ni kuwa first lady hivyo baada ya kuona mumewe si mgombea urais akamuamuru mumewe wahame ni si blah blahs nyinginezo(hii ni kama Gwajiboy hutoa kauli za kuaminika).
Wewe ni mmoja wa wanufaika wa mfuko wa mwenyekiti kupitia ruzuku inayopigwa kinyemela chamani, au kama sio mnufaika basi kuna mnufaika fulan aliefanikiwa kukuingiza chaka na kukufanya usiwe na uwezo wa kutambua mapungufu yanayofanywa na hao unaowatetea.
 
Njia ya Mungu ni fumbo

RAIS HAKAINDE HICHILEMA AMUAPISHA ASKARI ALIYEMTENDEA WEMA AKIWA GEREZANI KUWA NAIBU KAMISHNA WA MAGEREZA. KUNA SOMO LA KUJIFUNZA

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameteua Bwana Kuyomba Bwalya kuwa Naibu Kamishna Jenerali wa magereza "Zambia Correction Service".

Hichilema aliwekwa 2kizuizini katika mahabusu gerezani chini ya Askari kijana mdogo anayeitwa Bwalya mwaka 2017, ambapo alibambikiwa mashtaka ya uhaini " treason" akituhumiwa kutaka kumuua Rais wa Zambia wakati huo Edgar Lungu.

Kiongozi huyo wa Upinzani wakati huo, alibambikiwa mashtaka ya uhaini kwa kile Jamhuri ilichodai kuwa alikataa kuupisha msafara wa Rais Edgar Lungu ambapo upelelezi ulidai kuwa ulibaini kuwa lengo la Hakainde ilikuwa kumuua Rais Edgar Lungu kwa ajali ya gari.

Hakainde aliachiwa HURU baada ya kusota gerezani kwa takribani miezi minne baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kumfutia mashtaka hayo kutokana na Jamhuri kukosa ushahidi wa kudhibitisha uhaini aliokuwa anatuhumiwa nao.

Wakati Rais Hakainde akimuapisha Bwalya na maafisa wengine juzi Jumatano, Rais alimsifu Bwalya kwa kufanya kazi kwa weledi uliotukuka na kuzingatia Sheria na Katiba licha ya mazingira magumu ya utawala kandamizi na unyanyasaji wa utawala dhalili, dhalimu na katili wa Rais Edgar Lungu.

Rais Hakainde amemuamuru Kamishna Jenerali Fredrick Chilukutu na Naibu Kamishna Jenerali Bwalya wa huduma za kitaifa za kubadili tabia kuyafanyia mageuzi makubwa magereza yote nchini Zambia.

"Kipekee nizungumze na nyinyi ndugu zangu wawili wa huduma za kurekebisha tabia katika magereza yetu" alisema 2Rais Hakainde

“Mimi ni mhitimu wa taasisi hiyo (magereza) na ninajua kabisa kinachoendelea katika taasisi hiyo. Wanapaswa kuwa vituo vya marekebisho ya tabia, kwa sasa sio bali magereza yamegeuka kuwa vituo vya mateso, unyanyasaji, udhalilishaji na mauaji. Mazingira ya magereza ni magumu na mabaya sana kwa sisi mahabusu, kama mahabusu wa zamani natuma ujumbe kwenu kwamba uteuzi wenu haukuwa wa bahati mbaya, niliteua kwa makini sana kwa kuzingatia ndoto na sera yetu ya kuliunganisha na kuliponya Taifa hili na hili nitalisisitiza katika kila sherehe za uapisho kwa wateule wapya ili tuweze kutoka katika siku za kutengwa hadi siku za kujumuishwa lakini zaidi kwako hakikisha unayafanyia mageuzi makubwa sana magereza yetu ili yawe vituo vya kurekebisha tabia na sio vituo vya mateso." Rais Hakainde

"Nawaamuru mkaondoe msongamano katika mahabusu na magereza. Kama mhitimu katika mahabusu na magereza yetu ninafahamu kwamba kila sero " cell" ilijengwa kwa ajili ya kuweka mahabusu 20 pekee lakini kwenye sero ambayo Mimi niliwekwa mahabusu tuliishi watu 170 kwa wakati mmoja, kama una UTU na ubinadamu unaweza kuelewa aina ya mateso Mimi na mahabusu wengine wanayopitia katika Taifa hili. Haiwezekani Wazambia tusishi katika Taifa HURU kwa mateso makali kuliko hata kipindi cha ukoloni kabla ya UHURU sasa huu UHURU utakuwa na faida gani? Hebu fikiri hapa katika hii sero usiku ukiingia kila mtu anataka alale, unalala wapi na vipi, hakuna sehemu ya kulala, hakuna usingizi katika sero zetu, mahabusu wanateseka sana" amehoji Rais Hakainde

"Sikujua kuwa siku moja ningetupwa gerezani na ninyi nyote hapa hakuna anayejua hatima yake, huenda hata wewe kamishna general na Naibu kamishna general kesho mkawa mahabusu je mtajisikiaje kuishi katika sero na magereza zenye mateso makali namna ile?" Anaendelea kuhoji Rais Hakainde

"Bwalya ni kijana mdogo, tulikutana katika hayo mazingira magumu niliyowaeleza. Alikuwa boss wangu. Licha ya Mazingira hayo magumu ya utawala kandamizi wa Rais Edgar Lungu lakini bado alihakikisha anafanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria, Katiba na kiapo." Ameongeza Rais Hakainde

"Bwalya anafahamu kile ninachokiongelea, na Mimi ninakifahamu kile ninachokisema. Ndiposa nikatazama na kujiuliza huyu kijana mdogo kabisa anawezaje kutenda HAKI na kufikiri sawa sawa katika mazingira ya utawala wa dhuluma na kandamizi namna ile? Bwalya alikuwa boss wangu nilipokuwa nimetupwa mahabusu gerezani. Nilifahamika zaidi kwa sababu wakati mwingine sikukubali baadhi ya amri ambazo niliona zinaenda kinyume na HAKI zangu za binadamu. Lakini huyu kijana alinielewa alijua ipi ni sahihi na ipi sio sahihi. Alikuwa boss wangu na leo anaapishwa na mmoja wa mahabusu wake. Maisha yanabadilika, maisha yanazunguka. Meza imepinduka. Alimalizia Rais Hakainde.

Kuna somo muhimu sana hapa. Jifunze kutenda wema siku zote uwe huna madaraka au una madaraka wewe mtendee wema kila mtu, huwezi jua kesho inaleta nini kupitia wema au ubaya wako.

Usimuonee mtu maana yawezekana hata wafungwa na mahabusu unaowaonea leo huko magerezani kesho mmoja wapo akawa boss wako.

Watu unaowaonea na kuwatesa leo ukiwaona wao sio lolote na sio chochote huenda kesho wakawa ni msaada mkubwa na wewe ukawa miongoni mwa wanaohitaji msaada wao.

Usimdharau mtu yeyote kwa sababu tu ya hali yake ya leo ukilinganisha na hali yako. Heshimu kila mtu maana hujui kesho unayemdharau atakuwa wapi na wewe unayejiona umefika utakuwa wapi.

Tumia madaraka, cheo chako, fedha zako na Elimu yako kuunganisha watu, kusaidia watu, ufanyike furaha na tabasamu katika nyuso za waliopoteza furaha maana kesho ipo na hujui inakuja na maajabu gani.

Ubaya HAUFI na wema HAUFI na kumbuka wema na ubaya vyote ni mbegu ambayo humea kwa wakati muafaka.

Zaidi sana usisahau kuwa kuna kitu kinaitwa Karma! Huyu jamaa huwa hamsahau mtu hata kama itachukua muda gani. What goes around comes around. Ukitenda ubaya UTALIPWA MABAYA na ukitenda wema UTALIPWA MEMA kwa saa, njia na wakati usioutarajia.

Usipande miba katika njia yangu maana huenda kesho ukalazimika kuipita njia yangu ukiwa huna viatu.

Rais Hakainde Hichilema aliapishwa kuwa Rais wa Zambia baada ya kumshinda Rais Edgar Lungu kwa ushindi wa kishindo. Hakainde alichaguliwa kuwa Rais baada ya kugombea mara 5 bila mafanikio. Hapa pia liko somo la kutokukata tamaa, ukishindwa jaribu tena na tena na tena hadi utakapofanikiwa.

Wema unalipa, tenda wema nenda zako
Makonda alishawahi kupewa guy ushauri na Chidi Benzi
Akaupuuzia

Sasa hivi yupo Nye kwa vile jumong anamhusudu

Isingekuwa hivyo zingekuwa jeraaaa
 
Back
Top Bottom