Rais Hakainde Hichilema afuta rasmi Adhabu ya Kifo Zambia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,366
8,098
#JFDATA: Kati ya mwaka 2015 hadi Desemba 2021, Watu 28,670 Walihukumiwa Kifo duniani kote kwa njia ya Kunyongwa, Kupigwa Risasi, Kukatwa Kichwa na Kuchomwa Sindano ya Sumu.

Mwaka 2021 pekee Watu 2052 Walipewa Adhabu ya Kifo kwenye Nchi 56 ikiwa ni Ongezeko la 39% na 579 kati yao Wameshauawa kwenye Nchi 18 huku 80% ya Vifo vikitekelezwa na Nchi 3 (Iran, Misri, na Saudi Arabia).

Zambia imekuwa nchi ya 25 Barani Afrika na ya 110 duniani kufuta kabisa Adhabu ya Kifo baada ya Rais Hakainde Hichilema kusaini Kanuni ya kuondoa adhabu hiyo rasmi Desemba 23, 2022.
=================

Wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini Zambia wamepongeza uamuzi wa kufuta sheria mbili za wakati wa ukoloni wa Uingereza ambazo ni utekelezaji wa hukumu ya kifo na kufanya ukosoaji wa kiongozi wa nchi hiyo kuwa kosa lenye adhabu.

Rais Hakainde Hichilema, ambaye chama chake kilikuwa katika upinzani kwa zaidi ya miongo miwili, alikuwa ameahidi kwamba angefutilia mbali sheria hizo iwapo atachaguliwa kushika wadhifa wa juu.

"Rais Hakainde Hichilema ameidhinisha kanuni ya adhabu ya 2022 ya kukomesha kutolewa kwa adhabu ya kifo na kosa la jinai la kudhalilisha jina la Rais, ambalo limekuwa kwenye vitabu vya sheria vya Zambia tangu enzi za kabla ya uhuru," msemaji wa rais Anthony. Bwalya alisema katika taarifa yake Ijumaa.

Mwanaharakati wa haki za binadamu Brebner Changala alisema uamuzi huo ni hatua kubwa katika kuondolewa kwa sheria za kikoloni ambazo hazifai katika utawala wa kidemokrasia nchini humo.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Mazungumzo ya Sera Caroline Katotobwe alisema Wazambia sasa watazungumza kwa uhuru.

"Kama wadau tunafurahi kwamba sheria hii kandamizi hatimaye imefutiliwa mbali. Hivyo kuruhusu wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru bila hofu ya kufunguliwa mashtaka kama ilivyokuwa siku za nyuma," alisema.

Zambia ilipata uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964. Taifa hilo la kusini mwa Afrika lina watu milioni 18.
===================

Zambian rights activists Saturday hailed as a "huge milestone" a decision to scrap two British colonial-era laws: the death penalty and making criticism of the country's leader a punishable offence.

President Hakainde Hichilema, whose party was in opposition for over two decades, had promised that he would scrap the laws if elected to the top job.

"President Hakainde Hichilema has assented to the penal code of 2022 abolishing the imposition of the death penalty and the offence of criminal defamation of the president, which has been on the Zambian statute books since (the) pre-independence era," presidential spokesman Anthony Bwalya said in a statement on Friday.

Human rights activist Brebner Changala said the decision was a "huge milestone in the removal of colonial laws that do not fit in the democratic dispensation of the country".

The executive director of the Centre for Policy Dialogue Caroline Katotobwe said Zambians would now speak freely.

"As stakeholders we are elated that this repressive law is finally done away with. Thus, allowing citizens to freely express their views without fear of prosecution as was the case in the past," she said.

Zambia gained independence from British rule in 1964. The southern African nation is home to 18 million people.

AFP
 
Attachments

  • Death Sentences and Executions 2021.pdf
    2.5 MB · Views: 3
Welldone President H&H,death sentence ni ukatili wa hali ya juu na pia science imethibitisha kuwa adhabu hii haijatibu tatizo la watu kuua, Tanzania nasi tuachane na adhabu ya kifo, na pia adhabu ya 30yrs kwa rapist nayo haileti matokeo chanya, rapist ikithibitishwa kwa foresinc investigations wawe castrated then waachiwe huru
 
Kuanzia mwaka 2023 na kuendelea tutegemee kusikia matukio mengi ya kihalifu kutoka kwa majirani zetu.

Kikawaida adhabu ya kifo ipo nchi nyingi sana ila haitekelezwi na kusudi la kufanya hivyo ni kuonesha msisitizo kwa wahalifu kuna adhabu kali.

Unapoifuta kabisa ina maana kubwa hasa kwa wahalifu na hali hiyo itaongeza matukio ya kihalifu. Sheria zinalindwa kwa uwepo wa adhabu kali sana
 
Tuna adhabu ya 30yrs in jail kwa rapists, ujambazi wa kitumia silaha, je matukio haya yanapungua hapa nchini?,jifanyie uchunguzi mdogo
 
Wakati huohuo kuna watu wanafungwa huku kwa kukosoa Mapaka😁😁😁
AIp4FA.jpeg
 
Welldone President H&H,death sentence ni ukatili wa hali ya juu na pia science imethibitisha kuwa adhabu hii haijatibu tatizo la watu kuua, Tanzania nasi tuachane na adhabu ya kifo, na pia adhabu ya 30yrs kwa rapist nayo haileti matokeo chanya, rapist ikithibitishwa kwa foresinc investigations wawe castrated then waachiwe huru
Adhabu haitolewi kutibu tatizo la kuu watu. Maana hata kuwafunga maisha wauaji haijawahi kutatua tatizo la kuua, bado mauaji yameendelea kuwepo.

Hakuna sababu ya kujali maisha ya mtu ama watu ambao hawakujali maisha ya wengine.

Hatu hawawezi kuendelea kulipa kodi ili kuendelea kuwalisha na kuwatunza wauaji, watu ambao hawakujali maisha ya watu wengine.

Jamii ina changamoto nyingi na za muhimu. Kuna mahitaji ya muhimu na ya msingi ambayo yanahitaji utatuzi, hozo pesa za kutunza wauaji zielekezwe huko kwenye madawa, barabara, vifaa tiba, madawati, na makundi mengine yanayohitaji msaada.

Adhabu ya kifo ni muhimu kuendelea kuwepo sio kwa sababu kwamba inazuia ama inatibu tatizo la mauaji bali kwa sababu hakuna haja na umuhimu wa kuwatunza wauaji.
 
Fair enough mkuu, wewe umeamua kunyonga wauaji (wakati wengine hawakuhusika kabisa na mauaji)huoni nawe utakua unafanya kosa la kuua!,ukipata muda Google uone nchi za Scandinavia zimefanikiwa vipi kuhusu death sentences na pia soma kuhusu states za US ambazo hazina death sentences
 
Mkuu, ambao hawakuhusika hilo ni kosa kwa sababu ni kuwaonea, tunanyonga wale waliohusika, ambao wametiwa hatiani kwa ushahidi usiotia shaka. Kwa mfano, kwa forensic investigation na advancement ya teknolojia katika kupambana na uhalifu, USA mtu haonewi kwa kuhukumiwa kifo,, labda huko nyuma ambako DNA teknolojia haikuwepo ila wote wanaohukumiwa kifo wametenda hilo kosa.

Tuangalie Scandinavia unakosema, mauaji hayapo, nikimaanisha yameisha kabila ni zero baada ya wao kuondoa adhabu ya kifo? Kama sio zero yanatoka wapi?

Huko USA kwa state ambazo hazina death sentence, mauaji yameisha kabisa ni zero ama yapo, kama yapo yanatoka wapi?

Kwa hiyo utakubaliana na mimi kwamba kuondoa adhabu ya kifo ama kuiacha hakujazuia watu kuuana, watu watauana hadi mwisho wa Dunia, sio kwa sababu adhabu ya kifo ipo ama haipo.

Hoja yangu inabaki pale pale, mtu anaeua mwenzake, tena kwa sababu za kipumbavu huyo hana sababu ya kuonewa huruma maisha yake. Hakuna sababu ya kutoa rasilimali zitumike kumlisha na kumtunza, huyo hana thamani kwani hakuona thamani ya maisha ya mwenzake. Huyo ni kumalizana nae mapema. Rasilimali zielekezwe kwenye maeneo ambayo kuna mahitaji ya msingi, sio kwa wauaji.

Mfano, huko mtwara kesi za watu kubaka watoto wadogo wa shule, darasa la 2, la 3 na kuendelea, wanabaka kisha wanaua, watoto wadogo wasio na hatia yoyote mtu kama huyo aue mtoto wako halafu ulipe kodi kumtunza magereza, hiyo akili ama mavi?
 
Back
Top Bottom