Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Utendaji unaendana na Elimu.Umeshafanya Tathmini ya shule za Sekondari na Vyuo ambavyo wakristo wanavyo ukilinganisha na Waislamu?.Umeshafanya Tathmini ya kuona ni Wakristo na waislamu wangapi wako kwenye Mashirika Makini ya kimataifa na yale ya Kibinafsi ambayo Udini hauna nafasi?.Nyie endeleeni na Kampeni za Kisiasa Misikitini ila mwisho wa Siku mtajikuta mmejaa kwenye Siasa lakini Vichwani Zero.

Wewe mdini,

Unadhani hakuna waislamu wasomi? Kwataarifa yako Wapo wengi sana kulinganisha na unavyofikiri. Ila changamoto iliyopo ni upendeleo wanaopeana wakristo katika serikali. Kama unataka kulifahamu zaidi kasome hiyo dhana ya mfumo kristo utaielewa nini nazungumza pia fuatilia jumuiya za kiislam zenye wasomi kama Tampro DIC na nyenginezo. Halafu angalia kuna akina nani mule?halafu jiulize kwanini hawapewi fursa . Na graduate wa kiislam sasa hivi wengi mno Wapo mitaani hawana kazi is it a coincidence au sijui utajaza mwenyewe.

Usijidanganye kwa kuiangalia bakwata ukadhani hamna wasomi wa kiislam
 
Kipuyo,

Hapo ndio unapokosea usawa mnataka katika Urais tu mbona HAMTAKI USAWA KATIKA UTENDAJI AMBAPO ASILIMIA 90 MMEJAZANA WAKRISTO ???? Kama sio udini ni nini kinachowasumbua? Na nyote wafia udini hamlizungumzii hili mnalifumbia jicho ndio maana nikawaambia tuondoleeni uduwanzi wenu mtaliharibu taifa kwa propaganda zenu Za udini.

Mdondoaji,
Hii tathmini ya asilimia tisini(90%) ya wakristo serikalini mmeipata wapi?nani kaifanya?
Kwa kadri ya ninavyofahamu wafanyakazi kwenye maofisi huwa hawaapishwi so huwaoni wakishika vitabu vya dini na kuwatambua kwa dini zao.
Wapo wengi wenye majina wanayofanana na ya wazung lakini ni waislamu tena wale wenye siasa kali kwani imani si jina bali ni moyo wa mtu.Na hivyohivyo kwa wakristo kuna wenye majina ya kiarabu tena si moja bali mawili hadi matatu lakini ni wakristo.
Sasa nyie mmejiridhisha vp kuwa wafanyakazi wengi ni wakristo?
Hata ingekuwa hivyo,je hawana sifa?
Najua hii ni propaganda mnayojazana misikitini ili kuibua chuki na kuendelea na zile ngonjera zenu za mfumo kristo zisizo na mashiko.
Wakuu wa idara nyeti ni wa dini yako lakini hamuongelei hilo kazi kung'ang'ana na wafanyakazi wa kima cha chini na wasio na sauti.
Kila mnalolifanya na kuliwaza tunalijua,
Wewe unafikiri madudu ya serikali ya awamu hii yangekuwa kwenye awamu ya mkiristo si kila siku mngekuwa barabarani?
Mfano wa watu wenye majina ya yanayoshahabiana na ya kikristo lakini si wakristo ni Benard Membe na IGP Ernest Mangu.
Kwa hiyo hadi hapo takwimu zenu za 90% ni pumba na ni za kuwadanganya wajinga tu.
 
rais ajaye sio tu kwamba atakuwa mkristo bali ni kwamba atakuwa MKATOLIKI. na atatoka CCM (WHETHER YOU LIKE OR NOT).....nyerere(mkatoliki), mwinyi(muislamu-suni),mkapa(mkatoliki), kikwete(muislamu-suni)....
yeyote ajaye lazima awe mseminary toka katholic na huyu si mwingine bali ni.............. BM
 
Mkristo Pombe Magufuli mimi naona atatufaa sana ninaan dika hivi kama muislam ninayeoona mbali sana,huyu jamaa mbali na dini au kabila yake naamini atakuja tufikisha mbali sana watanzania hawa wengine sijui akina Makamba na wengineo ni wababaishaji watupu wanaweza kutuletea sokomoko moja baya sana hapa nchini ila kuna suala la kiongozi kuwa mtu tough sana hilo nalo ni lazima tulitupie macho sana kwani hivi sasa katika maeneo yetu ya hapa afrika mashariki maadui zetu wanazidi kujipanga na wote dua zao kubwa ni kuona tanzania inasambaratika kwa namna yeyote ile kwa hiyo tunahitaji tumpate rais ambaye ataweza kuja pambana na hizi changamoto za namna hii na pia awe mbabe wa aina fulani hivi asije chezewa na vimtu kama vile akina kagame na kundi lao zima huyo ajaye ni lazima awe mtu makini sana hii amani tuliyonayo ndio sababu kubwa ya kuchukiwa na majirani zetu wengi makwao wenzetu wanauana ka kuku kwa visababu vidogo vidogo tuu.Amani yetu ni lazima tuilinde kwa nguvu zote.
You're spot on!Dr Magufuli is an excellent choice for the Presidency but the problem is,He's from the ruling party (old,corrupt and ineffective system) which needs systematic overhauling=new political party to lead the country.
 
Wewe mdini,

Unadhani hakuna waislamu wasomi? Kwataarifa yako Wapo wengi sana kulinganisha na unavyofikiri. Ila changamoto iliyopo ni upendeleo wanaopeana wakristo katika serikali. Kama unataka kulifahamu zaidi kasome hiyo dhana ya mfumo kristo utaielewa nini nazungumza pia fuatilia jumuiya za kiislam zenye wasomi kama Tampro DIC na nyenginezo. Halafu angalia kuna akina nani mule?halafu jiulize kwanini hawapewi fursa . Na graduate wa kiislam sasa hivi wengi mno Wapo mitaani hawana kazi is it a coincidence au sijui utajaza mwenyewe.

Usijidanganye kwa kuiangalia bakwata ukadhani hamna wasomi wa kiislam

Sijasema hakuna wasomi waislamu.Nimekuuliza kuhusu idadi ya Sekondari na Vyuo maana hicho ndicho kigezo cha jamii yenye mwamko wa Elimu.Nimekuuliza vilevile kuhusu ushiriki wao katika taasisi zisizo za kidini za kitaifa na kimataifa.
 
Mkuu jmushi, japo ni kweli, ila hili lilitokea byance tuu, hakuna utaratibu huo!.

Kwenye mada yangu Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?,

nilisema hivi


Na kwenye mada yangu hiiKete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote Katika Urais wa JMT?!.


nilisema hivi


Kwa vile hizi ni dhana tuu ila pia ndicho kilichotokea, ili kusimamisha dhana hii isiendelee na kugeuka "grund norm" haujafika wakati sasa, lazima tufike mahali tuamue by affirmative actions against dhana hizi kwa kuchagua the contrary ?!.

Pasco
Tuchaguwe contrary kwa kuepuka dhana?

Hiyo ni dhana ama ndo ukweli wenyewe?This thing has happened wewe unazungumzia dhana?

What kind of affirmative action can be taken?

Hoja yangu yenyewe haizungumzii juu ya kutake any action against or for anything whatsoever!
 
Tuchaguwe contrary kwa kuepuka dhana?

Hiyo ni dhana ama ndo ukweli wenyewe?This thing has happened wewe unazungumzia dhana?

What kind of affirmative action can be taken?

Hoja yangu yenyewe haizungumzii juu ya kutake any action against or for anything whatsoever!
Mkuu J.Mushi, dhana ni jambo linalotokea with a specific pattern as if limepangwa kumbe halikupangwa bali limejitokea tuu natural by chance, mfano hakuna kupokezana urais kati ya bara na visiwani, wala hakuna kupokezana urais kati ya Wakristu na Waislamu bali ilitokea tuu by chance, na pia by chance, marais wote walipokuwa Wakristo ika happen wakawa ni Wakatoliki!.

Baada ya kuibaini hii pattern kama hazitafanyika juhudi zozote za kuibadili, hiyo pattern inaweza kabisa kujirudia 2015 kwa rais kuwa Mkristo na Mkatoliki.

Affirmative action against ni juhudi za makusudi to change the pattern kwa kuhakikisha baada ya rais Mwislamu, aje rais Mwislamu tena na akija Mkristo asiwe Mkatoliki!, ili kubreak hiyo pattern na kuifuta hiyo dhana!.
Pasco
 
Mkuu J.Mushi, dhana ni jambo linalotokea with a specific pattern as if limepangwa kumbe halikupangwa bali limejitokea tuu natural by chance, mfano hakuna kupokezana urais kati ya bara na visiwani, wala hakuna kupokezana urais kati ya Wakristu na Waislamu bali ilitokea tuu by chance, na pia by chance, marais wote walipokuwa Wakristo ika happen wakawa ni Wakatoliki!.

Baada ya kuibaini hii pattern kama hazitafanyika juhudi zozote za kuibadili, hiyo pattern inaweza kabisa kujirudia 2015 kwa rais kuwa Mkristo na Mkatoliki.

Affirmative action against ni juhudi za makusudi to change the pattern kwa kuhakikisha baada ya rais Mwislamu, aje rais Mwislamu tena na akija Mkristo asiwe Mkatoliki!, ili kubreak hiyo pattern na kuifuta hiyo dhana!.
Pasco
Daah! Mkuu nakubali you are working extremely hard towards your goal!

Hiyo pattern ni sawa tu endapo itakuwa broken bila ya madhara yoyote kuwepo!

Unajuwa mkuu sisi waafrika ni watu wa imani imani sana! Tunapenda miujiza miujiza na mambo ya kiimani imani zaidi?

Kwa mfano mwafrika aliona maji yanazunguka na ukiweka kitu hapo kinazama na kinapotea kabisa!

Yani hata binadamu huwa wakiogelea maeneo hayo huwa wanazama na kupotea! Guess what! Tukaja na imani kuwa ni chunusi ndo anabeba hao watu na mitambiko kibao ikafanyika huku watu haswa watoto wakiambiwa wawe makini wasiogelee sehemu zenye chunusi!

Wenzetu wazungu wao waliona ni opportunity! Wakasema maji haya yanaweza kuzungusha mashine kabisa yanapozunguka!

So wakagundua HEP(hydro electric power), na leo hii tunanufaika nayo!

Mimi nimetizama tu nikaona hakuna muujiza hapa! Bali tunaweza kuhakikisha kuwa tunaitumia opportunity hii ya utamaduni huu ili kiweza kudumisha amani!

Haya hayakutokea kwabahati mbaya ama kimiujiza!

Badala ya kuona kwamba hii pattern ni coincidence ama some sort of a miracle! Tunatakiwa tutambuwe kuwa we can work on it to preserve it and come out with something positive for our nation badala ya kusema tu hili ni jambo baya na huku tukikubali kuwa no mojawapo ya mambo ama patterns zilizodumisha amani yetu?

Ama tunataka kujitia ulufundi kwa mambo serious?
 
nchi yetu haiongozwi kwa misingi ya dini. Wanaotakiwa ni viongozi wenye moyo na mapenzi mema na TanZan-ia.
 
Ilikuwa Kijana sasa linakuja suala la dini. Rais atachaguliwa kwa mujibu wa katiba, full stop. Vigezo havitaangalia, ujana, uzee, dini, jinsi na mambo kama hayo.

Rais fisadi hata awe wa dini gani au mpagani, hanufaishi watu wa dini yake. Ufisadi unaadhiri watu wote bila kujali dini, jinsi au umri wao. Mimi mkristo lakini bora aje Rais muislamu muadilifu kuliko mkristo fisadi!
Wote tunajua uhalisia hauko hivyo. Kuna sehemu kwenye katiba inaruhusu ufisadi? Ukishajijibu hilo swali jiulize ufisadi upo au haupo?
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Wenzetu wamarekani wanakiita kitendo cha ku alternate hizi dini kwa viongozi wetu kama unwritten constitution! Yote kwa yote nimepkupata vyema.
Unachanganya mambo aisee. Wamarekani katiba yao haijaandikwa ndio maana inaitwa "unwritten constituation" lakini bado ni rasmi (official). Hii ni tofauti na unwritten rules. Sisi katiba yetu imeandikwa ila kuna mambo yanafanyika kama vile ni taratibu rasmi wakati si rasmi na hayajaandikwa popote na ndiyo tunaita "unwritten rules".
 
Asante kwa pole mkuu!

Umezungumzia jambo la msingi kabisa bila kuingiza hisia.Ni mchango wa muhimu kabisa!

Sasa tizama humu wengi wetu tunavypenda kujitia upofu! Mara ooh! Dini si kigezo, mara ooh unaleta udini! Badala ya kujadili wanaleta hisia!

Ni vyema tukajidhatiti mapema! Wala sioni sioni big Issue yoyote kujadili mustakabali wa taifa letu!

Ndo wale watu kwa akili za kibongo wanadhani vitu vinatokea kama miujiza tu vyenyewe vyenyewe, na wandhani hatuhitaji kuvifikri wala kuvijadili! Mazoea ya uvivu wa kufikiri!

So wanadhani ni muujiza ama just a coincidence kwamba tuna rais mwenye Imani ya tofauti kila muhula unaofuata!
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kuwa ukiwauliza wengi wanaotoa tahadhari kuhusu udini kwamba udini ni nini/kufanya kitu gani na ni nani wanaoleta udini. basi huenda wengi wao wanaweza kushindwa kujibu swali hili. Kimsingi tumekifikia mahali udini umenasibishwa na yeyote anayetamka neno dini. Yaani imefikia mahali tunataka kuaminishwa kuwa kutamka neno dini ni dhambi.
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuwa dini flani ndo kigezo cha urais kama vile wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita, bado tuna nafasi ya kuuenzi umoja wetu na mshikamano uliopeleka amani tuliyonayo!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amini kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.

Tanzania kama tutaweka dini kama kigezo tuendako si kuzuri, mimi nafikiri uwezo wa mtu ndo kiwe kigezo cha kwanza, uadilifu, uwazi na upendo viwe vigezo vingine.
 
Kwani katiba ya sasa hairuhusu mwanamke kuwa raisi?
Inaruhusu lakini ishu ni culuture!

Ndiyo maana hapa na pale, issue hiyo hupewa kipaumbele.Mfano kwenye uchaguzi wa spika ambapo uamuzi ulikuwa kumchaguwa spika mwanamke! Anna Makinda akachaguliwa.Katiba haikusema kwamba sasa tumchaguwe mwanamke!

Kuna aliyeniuliza kama point ama hoja yangu inalenga kutaka kuwepo na sheria ama kama ninamaanisha kuwa katiba iseme tuwe na marais wa dini za tofauti kila muhula! Na mimi ndo nikamuuliza kwani katiba inasema lazima tuweke kiongozi mwanamke ama ni utashi wetu tu wa kuamuwa?
 
Mkapa,kikwete wote kutoka tanganyika sasa ni zamu ya wazanzibar,muungano ni wa nchi mbili.

Wewe umerogwa ama vipi, tangu lini mtu kutoka ujerumani akatawale ufaransa eti kwa kuwa wote wameungana kwenye umoja wa ulaya. Zanzibar ni nchi na Tanganyika ni nchi. Futilia mbali zile enzi za ujinga, kwanza mwinyi sio mzanzibar.
 
Wala mimi siko huko isipokuwa hizi habari za kumchagua rais kwa sababu ni Kijana/Mzee au Mkristu/Muislaam inanipa mashaka sana na akili zetu.

Kiongozi kama rais ana sifa zake. Ni kiongozi ambaye anatambua tofauti zetu na umuhimu wa nila na tamaduni ambazo zimetuweka sisi kuwa wamoja kwa miaka 50 na Taifa gani tunataka kulijenga. Sasa unapopongeza utukufu unaotazama mtengano wa kiimani hizo tamaduni kuwa kigezo hapo ndipo naposhindwa kuelewa. Na ujue fika kwamba kuna tofauti baina ya Leadership na Management iwe kwa sifa ama malengo.

Hakuna adui mkubwa wa umoja wa watu kama kuendeleza tofauti zao na ndiomaana Nyerere alisisitiza kufuta Ukabila. Na pengine niseme tukitoka katika Ukristu kesho Hao hao wakristu watadai tunahitaji rais Lutherani au Protestant kwa sababu kila rais aliyepita alikuwa Mkatoliki, Na Shia nao watakuja na lao kuhusu Sunni, Bniani na kadhalika. Yanayotokea Iraq na nchi za Kiarabu leo sii ya bahati mbaya, hawa watu kabila zao sina define Imani zao, ni watu waloshindwa kuelewa mila na tamaduni zilizowaweka pamoja badala yake wakaweka imani zao kuwa msingi wa jamii.

Hata huko India vile vile kabila ndizo zinajenga imani zao za dini na ndio maana wameishi kwa matabaka miaka yote. Pakistan, India na Bangladesh kugawanyika ilitokana na ubaguzi wa Kikabila = Dini. Hivyo nasi kuiga vitu kama hivi wakati tunaona athari zake ni kuonyesha wazi kwamba tunashindwa kusoma wakati. Kwa wenzetu wazungu Uislaam na dini nyinginezo ni wageni kwao hivyo mgeni analazimika kufuata mila na tamaduni zao japo wao ni wa makabila tofauti na imani tofauti ndani ya Ukristu.

ndio maana sisi wengine tunamwona Nyerere kama Genius kwa sababu alijaribu kuondoa Ukabila na Udini kutokana na mifano aloiona Ulaya. Mrusi aliyehamia Marekani leo anajisikia ni Mmarekani kuliko Mwafrika alozaliwa Marekani. Na ajabu Mrusi huyo huyo siku kuna mashindano baina ya Urusi na Marekani utamwona akibeba bendera vya Urusi. Tazama World cup hii jinsi Waamerika wenyewe walivyokuwa nyuma ya timu yao japo ikicheza na nchi ya asili yake anarudi kwao. Hakuna mtu alomshikia bango mwenzake wala uadui kwa sababu wanaelewa nini maana na haki za Uraia pamoja na fursa zake.

maendeleo ya watu hawa hayakuja kwa bahati mbaya bali ni kuelewa ruksa na fursa za Uraia. Kuelewa kwamba hakuna Ukabila ndani ya Marekani ila kuna taifa jipya lenye mkusanyiko wa Mataifa yote duniani na wenye vipaji na fursa ya kufikia ndoto ulokuwa nayo. Na tuseme ukweli bila woga Ujio wa Obama (sii mweusi tu bali ana asili ya Kenya, Afrika) ni ishara tosha ya Taifa waloweza kulijenga maana katoka ktk kundi la watu wachache na wanaodharauliwa kuliko mataifa yote.

Tuachane na fikra hizi za Ujana na Udini zitatupeleka pabaya zaidi..
Unafikiri ni kwa nini imewezekana kwa Marekani kuwa taifa la aina yake? Kimsingi yaliyowezekana Marekani japokuwa yamepiganiwa kwa nguvu na juhudi lakini yaliwezekana kwa sababu kiasili wamarekani tangu mwanzo walikuwa mchanganyiko wa jamii nyingi. Ni kweli kuwa waingereza ndio walikuwa watawala kule lakini hadi Marekani inapata uhuru (usahihi zaidi kujitangazia) wake kulikuwa na mchanganyiko mkubwa kiasi chake, hali iliyopelekea kutafuta njia bora zaidi ya kuishi pamoja kwa amani. Na ndipo wakaja na siasa ya kuwakubali watu wote. Lakini pamoja na yote hayo leo hii ni vigumu sana kwa Mmarekani muislamu kuwa raisi kwa kuwa pamoja na kusema kuwa wao hawangalii dini/rangi/jinsia na makorokoro mengine lakini bado binadamu kiasili hatuko hivyo kwa hiyo linapokuja suala la uchaguzi haya mambo yanaangaliwa. Na ndio maana suala la uwezekano wa Obama kuwa muislamu lilikuwa ni ishu kipindi cha kampeni.

Kwa hiyo mkuu suala la kutamani kuwa na ideal society ni kitu kimoja na hali halisi ni kitu kingine. Leo hapa tunataka tudanganyane kuwa watu hawangalii masuala ya dini katika chaguzi, ni kujidanganya kwa huwa hali halisi haioneshi hivyo. Busara zaidi ni kukubaliana na hali halisi na kukabiliana nayo kuliko kujifanya mbuni kuficha kichwa katika mchanga.
 
Inaruhusu lakini ishu ni culuture!

Ndiyo maana hapa na pale, issue hiyo hupewa kipaumbele.Mfano kwenye uchaguzi wa spika ambapo uamuzi ulikuwa kumchaguwa spika mwanamke! Anna Makinda akachaguliwa.Katiba haikusema kwamba sasa tumchaguwe mwanamke!

Kuna aliyeniuliza kama point ama hoja yangu inalenga kutaka kuwepo na sheria ama kama ninamaanisha kuwa katiba iseme tuwe na marais wa dini za tofauti kila muhula! Na mimi ndo nikamuuliza kwani katiba inasema lazima tuweke kiongozi mwanamke ama ni utashi wetu tu wa kuamuwa?
Ile ya spika mwanamke karibia kila mtu anajua suala lilikuwa kumwadhibu bwana Samwel
 
Daah! Mkuu nakubali you are working extremely hard towards your goal!
No working!, no goal ! just observation and jf comments tuu!
Badala ya kuona kwamba hii pattern ni coincidence ama some sort of a miracle! Tunatakiwa tutambuwe kuwa we can work on it to preserve it and come out with something positive for our nation badala ya kusema tu hili ni jambo baya na huku tukikubali kuwa no mojawapo ya mambo ama patterns zilizodumisha amani yetu?

Ama tunataka kujitia ulufundi kwa mambo serious?
Kwa hiyo Mkuu J.Mushi unashauri sasa tuipreserve hii pattern, badala ya kuiacha ijitokee tuu coincidentally na badala yake sasa tuirasimishe iwe rasmi kwamba wabadilishane Mkristo na Muislam, na akiwa Mkristo wawe wale wale tuu?.
Pasco
 
Back
Top Bottom