Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Twende pound for pound unionyeshe huo udini, unatapatapa tu na wakati huna proof zaidi ya kujidai unajuwa watu.You don't know me like dat man! And if you think you do, weka hayo mabandiko niliyoonyesha udini badala ya unafiki unaounyesha hapa!

Wewe ndo wale ambao kama rais angekuwa mkristo awamu zote pengine ungejilipuwa wewe!

Acha hisia za kipuuzi baki kwenye mjadala usianze kujadili watu, as If hujawahi kuona matusi humu kuhusu mifumo na imani za viongozi wasio waislam kama wewe?

Watu wengine bana! Ukitaka za uso utapata mkuu! Lakini hakuna anayetaka kuweka ladha mbaya kwenye mahusiano yanayogusa maslahi ya Taifa.Mimi ni mtanzania kwanza kabla hata ya dini yangu, wewe je?

Kwani nani asiyejuwa udini wako? Sasa ndo unataka kuona kila mtu ni kama wewe!?

Acha chuki wewe!
Naona umeanza matusi baada ya kuishiwa hoja... wewe mdini tu huna lolote mwehu!! Tafuta thread yangu humu uone ni nani nilipendekeza anafaa kuongoza nchi hii kisha uone kama ni Mwislamu!!! Kama huwezi kuwafahamu wote kupitia maandiko yao basi hiyo juu yako lakini mimi nakufahamu kupitia maandiko yako mengi yenye hisia za kidini! Kama ungekuwa unataka usawa, kwanini usi-propose Rais awe Zanzibar ambao kwa misimu miwili hawajatoa Rais na wanalalamika??

Mwisho usijipe status ya kwamba naweza kukujadili kwavile huna hadhi ya kujadiliwa na mimi bali najadili tabia zako za kuendekeza udini... ni ujinga kukataa kwamba sio mdini wakati hoja yako hapa unataka Rais Mkristo huku ukijitahidi kuipaka rangi ili usionekane mdini....
 
No working!, no goal ! just observation and jf comments tuu!

Kwa hiyo Mkuu J.Mushi unashauri sasa tuipreserve hii pattern, badala ya kuiacha ijitokee tuu coincidentally na badala yake sasa tuirasimishe iwe rasmi kwamba wabadilishane Mkristo na Muislam, na akiwa Mkristo wawe wale wale tuu?.
Pasco
Ni ushauri tu kwa vyama vya siasa! Wao ndo wanatuletea wagombea na sisi tunapiga kura kuwachagua!chochote watakacholeta, hatuna cha kufanya zaidi ya kuchagua kati ya watakaoletwa na vyama hivyo vya siasa!

Sasa unavyosema kuipreserve hiyo pattern sijui una maana gani? Ama pengine hujunielewa vyema?ama umemix niliposema kuipreserve amani yetu, umoja na mshikamano?

Maana hapa sasa si ni ushauri tu kwa vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla?!
 
Kwani Wachawi na Waganga wa mambo haya wanasemaje kuhusu rais ajaye katika nchi yetu ?
 
Sasa unavyosema kuipreserve hiyo pattern sijui una maana gani? Ama pengine hujunielewa vyema?ama umemix niliposema kuipreserve amani yetu, umoja na mshikamano?!
Labda mimi ndio nikuulize, uliposema hivi ulikuwa unamaanisha nini
Hiyo pattern ni sawa tu endapo itakuwa broken bila ya madhara yoyote kuwepo!

Badala ya kuona kwamba hii pattern ni coincidence ama some sort of a miracle! Tunatakiwa tutambuwe kuwa we can work on it to preserve it and come out with something positive for our nation badala ya kusema tu hili ni jambo baya na huku tukikubali kuwa no mojawapo ya mambo ama patterns zilizodumisha amani yetu?.
My catchline is
we can work on it to preserve it and come out with something positive for our nation
 
Naona umeanza matusi baada ya kuishiwa hoja... wewe mdini tu huna lolote mwehu!! Tafuta thread yangu humu uone ni nani nilipendekeza anafaa kuongoza nchi hii kisha uone kama ni Mwislamu!!! Kama huwezi kuwafahamu wote kupitia maandiko yao basi hiyo juu yako lakini mimi nakufahamu kupitia maandiko yako mengi yenye hisia za kidini! Kama ungekuwa unataka usawa, kwanini usi-propose Rais awe Zanzibar ambao kwa misimu miwili hawajatoa Rais na wanalalamika??

Mwisho usijipe status ya kwamba naweza kukujadili kwavile huna hadhi ya kujadiliwa na mimi bali najadili tabia zako za kuendekeza udini... ni ujinga kukataa kwamba sio mdini wakati hoja yako hapa unataka Rais Mkristo huku ukijitahidi kuipaka rangi ili usionekane mdini....
Wewe ndo mwehu kabisa! Naona umewehuka, nimekwambia weka hayo mabandiko yangu yanayoonyesha udini! Halafu na mimi nikuletee mabandiko yako yenye kuonyesha upofu wako na ujinga wa kidini! We ni ---- tu! Changanya makalio kama unaona ni too hot!
 
labda mimi ndio nikuulize, uliposema hivi ulikuwa unamaanisha nini

My catchline is
Kuipreserve amani was a word!

As far as the pattern Is concerned! Kama pattern ndo utamaduni wenyewe ni sawa tu!

As long as siyo ishu ya kuweka kwenye katiba, then we'll be fine!
 
Wewe ndo mwehu kabisa! Naona umewehuka, nimekwambia weka hayo mabandiko yangu yanayoonyesha udini! Halafu na mimi nikuletee mabandiko yako yenye kuonyesha upofu wako na ujinga wa kidini! We ni ---- tu! Changanya makalio kama unaona ni too hot!
Can I tell you something?! Even if your smartness triples, you'd still be stupid, dumbass ever. Niweke mabandiko gani tena wakati nimeshasema hilo nalo ni full udini? You ain't nothing fartnocker, you're just the product from the abused use of condoms...
 
Sifa ya kuwa expadre ikiwa ni upungufu machoni kwako, huo siyo udini?!

Maana hapo si unajaribu kuwa please wale wananchi wanaoona ukristo ama uexpadre ni jambo baya?

Sasa hao ukiwawekea rais mkristo mihula yote kutakuwa na amani?

Hivi kwanini hauwezi kabisa kuiona issue hii in many different dimensions?

Ama mnakuwa fixated kutokana na feelings?

Kiukweli ninatoa pendekezo na pia ni mada ya kuchokoza maoni for as there Is a question mark on the heading!

Ni baada ya kuona jinsi udini ulivyoongezeka, nikasema basi ni vyema tuangalie yale ambayo hayata endelea kuchochea huo moto ama cheche za udini!

Hili ni tatizo tena limekuwa sugu zaidi chini ya utawala huu wa ccm!

Mbali nakwamba ni vyema kuzingatia huo utamaduni kwa maoni yangu, pia ni vyema kuwapima wagombea hao kuhakikisha hawana sifa zitakazoleta malalimishi!

Wanapimwa kwa utendaji wao na si kihisia hisia kama ilivyotokea kwa Dr Slaa uchaguzi uliopita!

Tunadai hatuna hisia za kidini na wakati kuna viongozi waliokataliwa kwa hisia za kidini eti mukiita sifa mbaya yenye mapungufu?!

Na kama hujui mkuu, hisia za kidini ni rahisi sana kupofusha na kutokuona vilivyo wazi kabisa, just kwasababu havinasibiani na hisia zako za kiimani na machaguo yao!
Mkuu wangu unajua tupo ktk dunia mpya na utamaduni mwingine wa kupofusha watu lazima ufukiwe hasa baada ya kuwa na itikadi na mirengo ya vyama. Ule utamaduni wa kwamba rais akiwa Mtanganyika basi lazima makamu wake awe Mzanzibar ama kupokezana utawala hii inatia shaka zaidi na demokrasia gani tunayoichukua.

Leo hii sii rahisi mtu kusema huyu ni Mtanganyika ama Mzanzibar kwa uraia ama asili maana sisi sote tumeungana kwa lengo la kuunda Taifa moja na sii Imani ya dini wala Uzawa. Na ifahamike tu ya kwamba haya yalifanyika wakati ule wa chama kimoja na itikadi moja, hapakuwa na vyama vingi hivyo hapakuwa na kupokezana isipokuwa dhana tu maana Nyerere alitawala miaka mingapi? na hata ukichukua toka mwaka 1964 baada ya Muungano, aliitawala miaka 20 kufikia mwaka 1984 Je, alipokezana na nani na ikiwa ilitokana na Ukristu na Uislaam Nyerere alikuwa mwenyekiti wa TANU toka mwaka 1954 na kuachia mwaka 1990 kama sikosei. Je, huo utamaduni wa kupokezana uko wapi? Hii dhana ya kupokezana mmeitoa wapi?

Ni rahisi sana kusema Salim A. Salim ni Mzanzibar, wakati huyu mtu kisha hamia Bara karibu miaka 40 ilopita na wala sii peke yake wapo wengi sana walohamia bara. Na wapo pia watu walozaliwa bara ambao wanaishi Zanzibar kwa zaidi ya miaka 60 kabla ya Uhuru, sijui hao tutawaita Wazanzibar ama Wabara. Na kibaya zaidi ni kwamba wapo watu wa Mataifa mengine walohamia Zanzibar na bara ambao ni raia wa nchi hii sijui wao tutawaita Wazanzibar, wabara au walowezi maadam asili yao sio hapa. Kwa mfano Wangazija na Wamalawi hawa wapo Znz na bara tena ktk ngazi ya uongozi.

Vivyo hivyo ukienda ktk Dini, sielewi Muislaam ni nani na pengine nikujulishe tu ya kwamba Uislaam sio kabila, jina wala uzawa na wala haikomei ktk IMANI. Hivyo huwezi kumuita mtu Muislaam kwa tafsiri ya ufuasi kwa sababu Muislaam sii mfuasi wa Muhammad bali Muislaam ni yule anayeishi ktk Uislaam, Muhammad mwenyewe alikuwa Muislaam. Islaam is the way of life na inasisitiza - Total submission to God - kama mnavyowaita Walokole na sii wa kuunga unga kwa jina. Hivyo wewe unaweza kuniita mimi Muislaam kwa sababu ya jina langu lakini kiukweli navyoishi sii ktk Uislaam na sistahili kuitwa japo baina yangu na wewe haturuhusiwi kumhukumu mtu.

Labda nikupe mfano wa Kisiasa ambao huwezi kumwita mtu ama serikali ya Kijamaa ikiwa serikali hiyo haifuati misingi ya Kijamaa. Ukisoma katiba yetu utafikiri sisi ni Wajamaa na tunaweza kujiita wajamaa ama jamii inayotaka kujenga Ujamaa na Kujitegemea, lakini je kweli sisi Wajamaa? kweli tunataka kujenga Ujamaa na Kujitegemea au dhana tupu. Je, tunachagua viongozi wetu kwa sifa hizo (kikatiba) ama tunawachagua kwa sifa zao wenyewe na propaganda za vyama vya siasa ktk kutazama mgombea gani anauzika?. hakuna hata moja linalohusiana na Ujamaa ila katiba inasema wazi sisi tunataka kujenga taifa gani. Hiyo China yenyewe leo hii sii Wajamaa wa miaka ya 60 na huwezi kusema China leo itafute kiongozi Mjamaa wakakuelewa maana Ujamaa wao wameutafsiri wapendavyo na pengine haupo tena.

Hii pia ipo ktk dini zetu tuna viongozi wa madhehebu yanayotafsiri Biblia ama Kuruan wapendavyo na kujiita Waislaam au Wakristu na hakuna kati yetu anayejua mkweli ni nani isipokuwa tunachagua dini na madhehebu na sio viongozi wa dini. Usije nambia wewe ni dini fulani kwa sababu ya mchungaji fulani! Licha ya hivyo majina ya watu ni utamaduni wa asili na makabila, hivyo ukisikia mtu akiitwa Salim hili ni neno la jina kwa Kiarabu, sio jina la kiislaam ila lina maana nzuri inayosisitizwa ktk Uislaam, hivyo haina tofauti na mtu huyo akiitwa Peace au Amani kwa kiswahili haibadilishi maana. Uislaam unasisitiza tu tupeane majina mazuri, lakini sisi mbururazz tumechagua kutumia lugha za wageni kupeana majina - Huu ni Ujinga mwingine!

Swali la kujiuliza sisi na haswa nyie Ma great thinker ni kwa nini tuwe na utaratibu wa kupokezana Urais kutokana na Imani ya dini ikiwa dini hizi zinapingana na katiba yetu. Kwa nini tumpe nafasi kiongozi Urais kutokana na imani yake ilihali katiba Inakataza na kukemea ushirika wa serikali na taasisi za kidini. Hivyo kwa nini sisi tusikemee kiongozi yeyote ambaye navunja misingi hii kwa kutumia dini kujitangaza ama kupatia ushindi wake. Kwa nini ikiatikana ushahidi kwamba mgombea Urais katumia imani za dini kufanya propaganda zake na hivyo kuondolewa ktk wagombea?...

Mimi nadhani mambo yote tunayoyaona ama kuyabeba ni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji ktk SHERIA zetu wenyewe. Tunasema Rushwa mwiko lakini kila kiongozi na wananchi wanapokea na kutoa Rushwa! Hivyo mifano yako yote ni sawa na kusema maadam tumeshindwa kusimamia sheria basi hata RUSHWA iwe halali kama wale wanaotaka bangi na Cocaine iwe ruksa kama Uholanzi kwa sababu sheria imeshindikana na kuna Uhuru wa watu kuchagua hata kufa kwao iwe ruksa kujimaliza (commit suicide). Huu Uhuru wa watu unapopitiliza ndipo sheria inapokuwa dhaifu..
 
Mkuu sema ukweli wako toka moyoni,ikitokea marais wote wanaochaguliwa now onwards coincidentaly wakawa wakristo,je utaridhika?

Unadhani usalama utakuwepo hata kama inatokea tu bila kupangwa tukawa na marais wakristo peke yake kuanzia uchaguzi ujao?

Just be honest on your answer!
 
Hainisumbui wala haijalishi kitu kwangu kwa sababu Mwinyi akiwa rais ndiye alopiga vita Waislaam walopingana na Bakwata, ndiye aloweka Elimu na Afya ktk Mkataba na makanisa na ikaundwa taasisi kusimamia Elimu na Afya nchini, ndiye alofungua mahusiano yetu ya kibalozi na Israel. Wakati Nyerere alipingana na kila uonevu unaomdhalilisha mwananchi hata akafuta mahusiano yetu na Israel na hakuyafanya hayo kwa sababu ni Mkristu - Mkatoliki. Kama nilivyosema Uislaam ni ibada, ni vitendo na maisha yako unavyoishi na sio jina la mtu. Am not proud of JK either, kwa sababu muislaam na wala simhukumu Mkapa kwa sababu ni mkristu.They are who they are politically!

Hii habari ya labeling watu imetokana na hisia zenu wenyewe kiasi kwamba wale wanaojiita Waislaam wakajipa nao majina kujitofautisha sawa na Mzungu alipojiita White basi nasi tukakubali kuitwa Weusi ili mradi tuwe tofauti nao. You can call Africa Europe, it won't change a thing! Swala la usalama haliwezi kuwepo hata kama akichaguliwa Muislaam/Mkristu kwa muhula mmoja au miwili pale udini umeshamiri. Leo JK na Dr.Slaa wanahukumiwa kwa dini zao wakati haikuwepo zamani. Mbona wakati wa Nyerere alitawala miaka 23 na salama hatukusikia Ukristu wake hadi alipoingia Mwinyi, na kwa umaskini wetu ndio ikiwa deal?

Yes, naweza kutokubali rais awe Mkristu ikiwa rais huyo atachaguliwa kwa Ukristu wake lakini sintothubutu kumkana rais kwa jina lake au ubatizo wake ikiwa anafuata katiba inayokataza Udini na pia misingi bora ya chama ktk ujenzi wa Taifa hili. Na maadam tumeshindwa kukomesha Udini kutokana na udini uliopo, nitapinga kiongozi yeyote awe Muislaam au Mkristu atakaye chaguliwa kutokana na mfumo wa kupokezana ama kuendeleza kile mnacho amini.
 
Dini ni non-issue..awe na dini au asiwe nayo muhimu afahamu watanzania wanataka aende Ikulu kufanya nini na awe tayari kutekeleza!!
 
Mkuu umeongea vyema sana tu!Mfumo wa kupokezana siyo official!Unaweza kuita coincidence kama wengi wenu mnavyotaka kusema!Lakini ninaamini kabisa kuwa hilo ni mojawapo ya sababu za uwepo wa amani nchini especially btn religions!

Hivi sasa inaonekana kwa wengi wenu(sijui kama ni ukweli),kuwa coicidentally,tumeweza ku alternate marais BILA KUPANGA!Lakini bado kuna malamiko pande zote!Ama mkuu unataka kuniambia haufahamu hilo?

Mkuu umeongea vyema sana hadi nimefurahi,lakini unfortunately,mambo hayako hivyo!Tena si afadhali wakati wa Nyerere tulikuwa kama ndugu?Hiyo issue ya wapalestina na waisrael hata mimi nikiwa mmojawapo wa kuwapinga waisrael.lakini waislam wa nchini,wameharibu ule udugu.So as of now,i don't really care about the middle east shit!

Kama reflection ya wengi wa waislam ndo hiyo kama ya wapalestina,hilo linanifanya kutokurukia tu na kuwasapoti hao wapalestina dhidi ya Israel!

Hilo lazima litawa bite wabongo!Ule udugu haupo tena kihiivyo,ndo maana unaona hata humu kuna ubishani wa palestine vs isarael kwa misingi ya dini!Matusi kedekede na disrespect kwakila imani za wenzao!

Sasa ndo maana naelewa kuwa,kwa utaratibu huu,itafika pahala tunaweza kutaka hayo mambo yawe officially recognised.

Mark ma words and this thread,Mungu atupe uzima uje kuniambia mkuu!

It is a safer way since kwa maoni yangu,there is no a way to return!HOW?
 
Mkuu umeongea vyema sana hadi nimefurahi,lakini unfortunately,mambo hayako hivyo!Tena si afadhali wakati wa Nyerere tulikuwa kama ndugu?Hiyo issue ya wapalestina na waisrael hata mimi nikiwa mmojawapo wa kuwapinga waisrael.lakini waislam wa nchini,wameharibu ule udugu.So as of now,i don't really care about the middle east shit!
(bold) This explain a lot! unaendeshwa na emotions na ndio Udini huo!
 
Pouwa tu mkuu,tushafika hakuna njia tena,na kama nilivyosema,mark my words,tutakuja kuwekeana haya masharti,subiri uone.Mark this thread too kama nilivyokambia!

Unaweza kujipendekeza kwa watu wasiokupenda?Utaratibu huu,mwishowe mtaufanya official ili unafiki uishe mujuwe kuwa kuheshimiana hakuji kinafki!

Mwalimu tutamkumbuka kwa hilo,na wengi wa waislam wameharibu kwasababu wanamtukana mtu aliyekuwa akiweka ubinadamu mbele kwenye ishu hizo!

Inanifanya kujiuliza mara mbili mbili kuhusu hao wapalestina!

Sikuwahi kufahamu kama kuna chuki za kidini kiasi hiki nchini mwetu,slowly but surely,tutageuka na kuwa kama mataifa mengine tu,tofauti na misingi aliyoweka Nyerere!Misingi mizuri sana licha ya madhaifu yake mengine!

Misingi hiyo ishaharibika,ndo ukweli huo!Na sisi kwa upofu wetu,tunaiita coincidence kwasababu mwalimu tayari si alikuwa adui wa usilam kwa waislam walo wengi?Ama hujui kuhusu hilo?
 
Tatizo lako unasumbuliwa na Udini mkuu wangu hakuna lolote.

Kama kumtukana mwalimu tumewasikia toka kina Kambona, Marreale, Mtikila, na hata mchungaji Munisi. Majuzi tu ktk bunge la katiba wapo wengi wakristu wamezionyesha sura zao kamili. Ukweli ni kwamba hawa wote hawakubaliana na siasa za mwalimu iwe kwa sababu ya dini, Ukabila ama maslahi yao binafsi kwa sababu Nyerere alifunga mirija yao. Hizi ni sababu tu za kumtafuta mchawi lakini sii swala la waislaam, wachagga au wahindi. Kila mtu ana historia yake ya kumpenda mwalimu ama kumchukia.

Na Hata Wazanzibar wachahce wanaoendesha siasa za udini imetokana na ukweli hawaupendi Muungano wetu na hawa watu hawampendi hata Karume kwa chuki ile ile sawa na Nyerere isipokuwa wanajificha nyuma ya pazia la Uzanzibar na Uislaam wasionekane wahaini wa Mapinduzi. Tena naweza sema wanamchukia Karume kuliko Nyerere maana wapo wanaofurahia kifo chake (Assassinated) wakati Nyerere akienda Unguja na kupokelewa kwa shangwe na baba zao. Mkuu huu uhuru tulopewa ni pamoja na kufikiri kwa kina kisha unatoa mawazo yako na sio kudakia na kuparaza ya wengine kuwa ndio ukweli.

Mpambe mkubwa wa Ubaguzi duniani ni Marekani aliyafanya haya toka wakati wa Ukombozi wa Afrika tukaitwa ngedele na trend ya kumrushia mtu mweusi ndizi ikaanza. Leo hawa ndio marafiki wetu wakubwa kwa sababu mnakubali siasa zao za kugawa watu ili wawatawale kiuchumi na wanafanikiwa sana maana hata Iraq, Somalia wamefikishwa ktk ujinga ule ule. Ama kweli kipofu haachi fimbo yake maana mtu alozoea Utumwa hawezi kuacha asili yake.

Congo ambako hakuna Waislaam, Rwanda, Ivory Coast, Ukraine, Zimbabwe, Nicaragua na kadhalika hayasemwi isipokuwa kule kwenye Uislaam na nina hakika kama nchi hizo zingekuwa za kiislaam sijui mngesema nini! mmekuwa programed kiasi kwamba mnashindwa kuingia ndani ya visa hivi na kujua who is behind all this! na What do they have in common? - Utajiri wao wa Maliasili na rasilimali zao na western world need them at lowest cost! na solution yao ni Wagombanishe!

Mkuu watu wanapigania Uhuru, haki na usawa lakini lazima marekani ajiingize kwa kumpamba nyapala the whip master kwa hila na visa vya Udini, Ukabila ama tofauti za jamii hiyo ili wafanikiwe wao kuchota utajiri wa nchi hizo. Na inashangaza sana kuona kuna watu kama nyie mnaotaka kutumia siasa hizo hizo kwa maana ya Utamaduni sijui Utamaduni gani zaidi ya kuwa watumwa wa hawa washenzi. Samahani sana mkuu mimi sipo nawe na nakomea hapa...
 
Kama wewe unaona mimi ni mdini na wewe ni nini?

Ina maana wewe Mkandara ni neutral?

Ama unataka kuita wengine wadini kwasababu hawaendani na msimamo wako wa kidini?

Wewe hapa unapigania upagani?

Ebu nieleze neutrality yako hapa inayokufanya kusema wewe si mdini!

Si afadhali mpagani anaweza sema hivyo?

Ofcourse tuko wote humu toka kitambo, so hilo halinipi shida hata chembe!

Utautafuta udini sana kwenye thread!

Hapa ni hoja sometimes zenye utelezi, utashangaa huwezi kushikilia moja!
 
Kama wewe unaona mimi ni mdini na wewe ni nini?

Ina maana wewe Mkandara ni neutral?

Ama unataka kuita wengine wadini kwasababu hawaendani na msimamo wako wa kidini?

Wewe hapa unapigania upagani?

Ebu nieleze neutralit yako hapa inayokufanya kusema wewe si mdini!

Ofcourse tuko wote humu toka kitambo, so hilo halinipi shida hata chembe!

Utautafuta udini sana kwenye thread!

Hapa ni hoja sometimes zenye utelezi, utashangaa huwezi kushikilia moja!
Niite unavyotaka lakini kinachonieleza mimi ni ktk maandishi yangu. Kama ningekuwa mdini ningeenda kuishi Saudia ambako sina haja ya kuomba rais au waziri mkuu atoke dini gani lakijni naishi nchi ya Wakristu na naridhika na maisha. Fikra zako za KUAFIKI mapokezano ya udini ndio Udini wenyewe, kwa sababu umefikiria what if the next President akiwa Muislaam? ina maana hukukubaliana nalo! kwa hiyo haijalishi wewe unataka kusema nini. What comes out of your mouth ndicho kinacho kutambulisha. Samahani sana kama nimekukwaza lakini ukweli lazima usemwe na wewe mwenyewe ndio umeyaweka hapa kuonyesha fikra zako huru. Hukatazwi wala hakuna aliyekushika mkono, you said what was supposed to be said and you stand by your word! - MDINI..
 
Next president kuwa the same dini kwa maoni yangu binafsi haifai!(kutokana na hali hali halisi ya sasa nchini mwetu)

Tena ninadhani udini ulikuwepo toka awamu ya kwanza sema mwalimu alijitahidi kufunika na kusawazisha!(BADO MNAITA COINCIDENCE AMA BAHATI MBAYA)

Lakini pia ni ukweli kuwa lazima kuwepo na makubaliano yatakayo weka msisitizo kwenye mutual respect baina ya watazania...Kwasababu pia siamini it was a coincidence kuwa na marais wa tofaut kidini!

Una haki ya kuendelea kufikiri kuwa imetokea kwa bahati kama unavyodai!

Maajabu, ni kwamba, eti unajidai kuwa hakutakuwa na maneno endapo marais watatokea kuwa wakristo kwa bahati mabaya kama unavyoona!?

However within the freedom of speech...Na mawazo ama ideas zangu siyo sheria!

Hatuwezi kufanana wote kwa maoni, however, ndo maana tunakuwa na mijadala!

We can disccuss instead of arguing, it healthier that way!

Kwasababu discussions ni kufind solution, where as argument ni kufind nani mshindi!

So we better discuss!

Having said that, kusema kwamba kwenda kuishi Saudi ndo kuonyesha kwamba wewe si mdini, huo ni upotoshaji mkubwa kabisa!

Kuna magaidi kibao kwenye nchi za West, sema tu wengi hawapati nafasi! Tena kuna wengine huwa wanajitolea kwenda kupigana vita vya jihad kuanzia Afghanistan, Yemen, Syria, Pakistan etc!

Hapo UK tu wako kibao, achilia mbali Canada and USA!

Halafu mkuu wangu haujanikwaza wala nini! Si mara yangu ya kwanza ku engage kwenye such discussion with you, i bet you remember!

I never harbor those kinda feelings mkuu!

Nimejifunza mengi sana duniani, na nikikutana na watu, inategemea na interactions, huwa nikipenda kujifunza zaidi na huwa nikipenda watu wenye mawazo huru na walioko tayari kujifunza na kuthink outside the box!

Hilo limekuwa shida sana inapokuja kwenye mijadala inayohusu imani za watu!

A lot of people wears religion on their sleeves, so wanakuwa very sensitive kwenye such topics na inakuwa extremely hard kwa wao kuthink outside the box!

Nimeshajifunza sana kuhusu hilo! Na michango yangu kwenye such topics iko accordingly!

Na ninakwambia mkuu, ningekuwa mdini si ningesema hatuna haja ya kuwa na waislam kama marais?

Maana si ninaweza pia kusema ugaidi umezidi nchini baada ya rais muislam kuyafungia macho matendo na chuki za kidini!

Mkuu kwa wanaoweza kuruka, wakiwa juu kabisa, wanaonekana wadogo sana machoni pa wale wasioweza kuruka! (#FoodForThought)
 
Ebu kaa na soma maandishi yako mwenyewe halafu nambie una discuss au una argue?..
Na rudi kunisoma miye halafu unambie kama na discuss ama nina argue maana mimi nakueleza hadi chimbuko la kila hoja unayo raise, na nakupa mifano wewe umekazania kuwalaumu waislaam kila msitari ni waislaam hivi waislaam vile. Ni wapi katika mazungumzo haya, mimi nimewalaumu wakristu hata mara moja kama sio wewe mdini?.

Mkuu hata hayo ya waislaam kujiandikisha kupigana vita ni fikra zako za Udni tu, kwa sababu huwezi kunieleza sababu gani Watanzania walikwenda kupigana vita ya South Afrika, Angola, Msumbiji na kadhalika kama ilikuwa Ubaguzi ama kusaidia nchi hizo zipate Uhuru wao. Hivi Kwani hao hayo Mataifa makubwa mengine hawaendi kupigana vita nje baada ya kujiandikisha? Juzi tu wamekufa Wamarekani wawili ktk vita ya Gaza hawasemwi na wengine waliandikishwa wengi kupigana vita ya Bosnia.

Na ajabu ni kwamba huhesabu Waamerika na mataifa makubwa wanaokwenda nchi ya wengine iwe Iraq, Misri, Syria au Libya kwamba ni wadini kujiandikisha kupigana huko isipokuwa wakosa ni wale tu wanaojiandikisha kuwalinda wenyeji wa nchi hizo. wakenya na Ethipia wameingia vipi Somalia nchi isokuwa yao kupigana vita kama sio ushenzi halafu mashambulizi upande toka wa pili ni Ugaidi.

Mimi ni natinaolist, napingana na Wazanzibar na napingana na utawala huu wa CCM bila kujali rais ni Kikwete au Mkapa. That's me!
 
Back
Top Bottom