Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Mtowa mada naona hata yy kajengeka kwa imani ya kidini zaidi japo naona kapindisha pindisha tu kutaka tumuone yeye hayupo kwenye udini
Mm kwangu rais ata awe mcristu awamu 10 kama ni muwadilofu huyo anafaaa kabisa
Awe anajali watu wake bila upendeleo awe mcristo muislam mpagani hote hawa ni wa tz

Mimi muislam unakuta nimezaa na mwanamke mcristu hapo watu hote ni sawa

Ninaimani nchi yetu inaharibiwa na viongozi wa dini za wacristo na waislam unakuta viongozi wa dini wanatowa matamshi ya siasa wakiwa kwenye nyumba zao za ibada tena matamshi yanyolenga taifa la watu ambao si hte wa mazeebu na imani hio wabadilike viongozi wetu wa dini
Tumeona kwenye kampeni za mwaka 2010 watu walikuwa wanambiwa na viongozi wa dini zao live tumpigie wa dhehebu letu hapo tunajenga nini

Nchi ya rwanda mauwaji mengi yalihalalishwa na viongozi wa dini japo wao hunyoosheya wanasiaaa
Kwangu mm viongozi wa dini ndio huwa chanzo cha kuwaminisha waumini wao kumchaguwa muumini mwenzao
Na nyie wanasiasa acheni kuongelea
Maswala ya kitaifa kwenye nyumba za ibada
Pale Moshi miaka ya nyuma kulikuwepo na mama mmoja aliyekuwa maarufu sana akiitwa mama Daruweshi, alikuwa mtu safi.Alikuwz pia akifuga farasi!

Tukirudi kwenye hoja hapa, naona umejitahidi kwa nguvu kutafuta udini, ukakosa, lakini bado ukaina uchangie tu kuonyesha hisia zako.

Kama nilivyosema hapo awali, hii ndo nchi yetu, tunaishi kiimani imani na pia tunaongozwa na imanimkwa kiasi kikubwa!

Hata mara pengi tumekuwa tukisema tunamwachia Mungu ama Mungu atuepushie na hili ama lile bila hata kuchukuwa hatua.

Kwahiyo imani kwa jamii yetu si jambo la kupuuzwa.Nadhani rais aliyepita angekuwa mkristo ndo ungeelewa zaidi!

Madhali umegunduwa kwamba hii issue iliibuka sana uchaguzi uliopita kwa ccm kutumia udini, hiyo tayari ni hatua nzuri!

Lets say hili ni tatizo, ok, limeonekana kuwepo kwenye siasa za kichama, unadhani kwenye siasa za kitaifa halipo?
 
Sijaongelea ishu ya kuchagua mwanamke na wala sijaandika neno mwanamke, suali langu tunaposema raisi awe mkristo, je hapo itakua ni democrasy?
Ulizungumzia uwepo wa issue hii kwenye katiba, ndiyo maana nikakupa mfano wa mgombea mwanamke, kijana nk.

Tulia pitia mabandiko yaliyopita kwa upole na utulivu.
 
Sie tunataka rais wa nchi,sio kiongozi wa kanisa wala msikiti. dini ni kwa faida yako wewe na mkeo.
Mkuu huyo rais unayemtaka watu na wake zao pia wanampigia kurankwa faida ya Taifa!tumia akili na usome mada kwa utulivu!

Tulia na uje na hoja na usijitie upofu kwasababu tu huna cha kaundika kwenye hii mada kuhusu chadema au Dr Slaa!
 
Mkuu vipi za mida?

Mkuu unwritten rules are mostly universal! Ok tuseme hizi za kwetu ni national! Kwa maana ya kwamba ni unwritten rules zinazo trump tofauti zetu za kisiasa(kumbuka ni national).

Maslahi ya Taifa ni muhimu zaidi hapa!

Hata tukiwaondoa ccm, haina maana kuwa na wananchi nao ni wapya! No! Wananchi ni wale wale wenye matatizo yale yale!

Binafsi naamini ni bora tufuate tamaduni zilizodumisha amani na umoja! Kwa maana kwamba kwa wengine kumchagua kiongozi mwenye Imani hiyohiyo kama aliyepita kwasababu tunataka upinzani ushike nchi haina mantiki!

Tunauwezo wa kupata viongozi wenye vigezo muhimu na hapohapo tukadumisha uhusiano wetu wa kidugu!
Wala mimi siko huko isipokuwa hizi habari za kumchagua rais kwa sababu ni Kijana/Mzee au Mkristu/Muislaam inanipa mashaka sana na akili zetu.

Kiongozi kama rais ana sifa zake. Ni kiongozi ambaye anatambua tofauti zetu na umuhimu wa nila na tamaduni ambazo zimetuweka sisi kuwa wamoja kwa miaka 50 na Taifa gani tunataka kulijenga. Sasa unapopongeza utukufu unaotazama mtengano wa kiimani hizo tamaduni kuwa kigezo hapo ndipo naposhindwa kuelewa. Na ujue fika kwamba kuna tofauti baina ya Leadership na Management iwe kwa sifa ama malengo.

Hakuna adui mkubwa wa umoja wa watu kama kuendeleza tofauti zao na ndiomaana Nyerere alisisitiza kufuta Ukabila. Na pengine niseme tukitoka katika Ukristu kesho Hao hao wakristu watadai tunahitaji rais Lutherani au Protestant kwa sababu kila rais aliyepita alikuwa Mkatoliki, Na Shia nao watakuja na lao kuhusu Sunni, Bniani na kadhalika. Yanayotokea Iraq na nchi za Kiarabu leo sii ya bahati mbaya, hawa watu kabila zao sina define Imani zao, ni watu waloshindwa kuelewa mila na tamaduni zilizowaweka pamoja badala yake wakaweka imani zao kuwa msingi wa jamii.

Hata huko India vile vile kabila ndizo zinajenga imani zao za dini na ndio maana wameishi kwa matabaka miaka yote. Pakistan, India na Bangladesh kugawanyika ilitokana na ubaguzi wa Kikabila = Dini. Hivyo nasi kuiga vitu kama hivi wakati tunaona athari zake ni kuonyesha wazi kwamba tunashindwa kusoma wakati. Kwa wenzetu wazungu Uislaam na dini nyinginezo ni wageni kwao hivyo mgeni analazimika kufuata mila na tamaduni zao japo wao ni wa makabila tofauti na imani tofauti ndani ya Ukristu.

ndio maana sisi wengine tunamwona Nyerere kama Genius kwa sababu alijaribu kuondoa Ukabila na Udini kutokana na mifano aloiona Ulaya. Mrusi aliyehamia Marekani leo anajisikia ni Mmarekani kuliko Mwafrika alozaliwa Marekani. Na ajabu Mrusi huyo huyo siku kuna mashindano baina ya Urusi na Marekani utamwona akibeba bendera vya Urusi. Tazama World cup hii jinsi Waamerika wenyewe walivyokuwa nyuma ya timu yao japo ikicheza na nchi ya asili yake anarudi kwao. Hakuna mtu alomshikia bango mwenzake wala uadui kwa sababu wanaelewa nini maana na haki za Uraia pamoja na fursa zake.

maendeleo ya watu hawa hayakuja kwa bahati mbaya bali ni kuelewa ruksa na fursa za Uraia. Kuelewa kwamba hakuna Ukabila ndani ya Marekani ila kuna taifa jipya lenye mkusanyiko wa Mataifa yote duniani na wenye vipaji na fursa ya kufikia ndoto ulokuwa nayo. Na tuseme ukweli bila woga Ujio wa Obama (sii mweusi tu bali ana asili ya Kenya, Afrika) ni ishara tosha ya Taifa waloweza kulijenga maana katoka ktk kundi la watu wachache na wanaodharauliwa kuliko mataifa yote.

Tuachane na fikra hizi za Ujana na Udini zitatupeleka pabaya zaidi..
 
Haijalishi rais ajaye atakuwa mkristo,mwislam,hindu au mpagani cha msingi atakuwa anatoka CCM...!!!
 
Jamani hebu acheni udini...mmejengwa kwa misingi ya ukabila na udini .sasa kila kitu mnaweka udini na ukabila mbele...
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amani kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.

Jmushi, naunga mkono hoja kwa asilimia fulani, huu ndio ukweli ambao watu wanaujua lakini wanogopa kuusema. Na kuwajuza zaidi si mkristo tu lakini ni lazima awe mkatoliki, nasisitiza "MKATOLIKI" hapa ndio utakumbuka vita ya Mrema(mlutheri) na Mkapa(mkatoliki).

2015 mamvi(mlutheri) hana nafasi na CCM wakimsimamisha mkrito mkatoliki ndio utakuwa mwisho wa Chadema na Dk Slaa(mkatoliki) atapotea kiana kumsafishia njia mgombea mkatoliki wa CCM.
Wekeni maneno haya katika kumbukumbu zetu.
 
Ulizungumzia uwepo wa issue hii kwenye katiba, ndiyo maana nikakupa mfano wa mgombea mwanamke, kijana nk.

Tulia pitia mabandiko yaliyopita kwa upole na utulivu.

Mimi nipo kwenye kiongozi kutoka dini fulani umeitoa wapi?
 
kama walivyoungana 2010 bahati nzuri Mungu si wa upande wao

ndo manake lazima awe mkristo ..tumechoka kugeuza Ikulu kuwa sehemu ya kulia mafutari na kufanya mahitima january to december.. vile vile hatutaki rais anayenyoa upara

Kwahiyo unataka ikulu zikabandikwe picha za yesu na misalaba ee???poor thinking capacity
 
Wala mimi siko huko isipokuwa hizi habari za kumchagua rais kwa sababu ni Kijana/Mzee au Mkristu/Muislaam inanipa mashaka sana na akili zetu.

Kiongozi kama rais ana sifa zake. Ni kiongozi ambaye anatambua tofauti zetu na umuhimu wa nila na tamaduni ambazo zimetuweka sisi kuwa wamoja kwa miaka 50 na Taifa gani tunataka kulijenga. Sasa unapopongeza utukufu unaotazama mtengano wa kiimani hizo tamaduni kuwa kigezo hapo ndipo naposhindwa kuelewa. Na ujue fika kwamba kuna tofauti baina ya Leadership na Management iwe kwa sifa ama malengo.

Hakuna adui mkubwa wa umoja wa watu kama kuendeleza tofauti zao na ndiomaana Nyerere alisisitiza kufuta Ukabila. Na pengine niseme tukitoka katika Ukristu kesho Hao hao wakristu watadai tunahitaji rais Lutherani au Protestant kwa sababu kila rais aliyepita alikuwa Mkatoliki, Na Shia nao watakuja na lao kuhusu Sunni, Bniani na kadhalika. Yanayotokea Iraq na nchi za Kiarabu leo sii ya bahati mbaya, hawa watu kabila zao sina define Imani zao, ni watu waloshindwa kuelewa mila na tamaduni zilizowaweka pamoja badala yake wakaweka imani zao kuwa msingi wa jamii.

Hata huko India vile vile kabila ndizo zinajenga imani zao za dini na ndio maana wameishi kwa matabaka miaka yote. Pakistan, India na Bangladesh kugawanyika ilitokana na ubaguzi wa Kikabila = Dini. Hivyo nasi kuiga vitu kama hivi wakati tunaona athari zake ni kuonyesha wazi kwamba tunashindwa kusoma wakati. Kwa wenzetu wazungu Uislaam na dini nyinginezo ni wageni kwao hivyo mgeni analazimika kufuata mila na tamaduni zao japo wao ni wa makabila tofauti na imani tofauti ndani ya Ukristu.

ndio maana sisi wengine tunamwona Nyerere kama Genius kwa sababu alijaribu kuondoa Ukabila na Udini kutokana na mifano aloiona Ulaya. Mrusi aliyehamia Marekani leo anajisikia ni Mmarekani kuliko Mwafrika alozaliwa Marekani. Na ajabu Mrusi huyo huyo siku kuna mashindano baina ya Urusi na Marekani utamwona akibeba bendera vya Urusi. Tazama World cup hii jinsi Waamerika wenyewe walivyokuwa nyuma ya timu yao japo ikicheza na nchi ya asili yake anarudi kwao. Hakuna mtu alomshikia bango mwenzake wala uadui kwa sababu wanaelewa nini maana na haki za Uraia pamoja na fursa zake.

maendeleo ya watu hawa hayakuja kwa bahati mbaya bali ni kuelewa ruksa na fursa za Uraia. Kuelewa kwamba hakuna Ukabila ndani ya Marekani ila kuna taifa jipya lenye mkusanyiko wa Mataifa yote duniani na wenye vipaji na fursa ya kufikia ndoto ulokuwa nayo. Na tuseme ukweli bila woga Ujio wa Obama (sii mweusi tu bali ana asili ya Kenya, Afrika) ni ishara tosha ya Taifa waloweza kulijenga maana katoka ktk kundi la watu wachache na wanaodharauliwa kuliko mataifa yote.

Tuachane na fikra hizi za Ujana na Udini zitatupeleka pabaya zaidi..
Mkuu mabadiliko tuliyonayo kama Taifa, mabaya ama mazuri, utakuwa huyatendei haki kwa utaratibu huu!

Mkuu hata hayo mataifa makubwa hizi discussions zipo.

Ninaamini kabisa kuwa hatukupata viongozi wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya!

Mkuu tena hili ninalolizungumzia tumekuwa tukilifanya, na siyo kama hizi hoja mpya za vijana, wanawake nk!

Utamaduni huu tumetoka nao mbali sana.Na hivyo hatuwezi kusema eti tutasabaisha udini! Pengine tukiacha kufuata taratibu hizo basi ndo tunaukaribisha huo udini kwa mikono yote na kwa moyo wote!

Nina amini kwa dhati kabisa kwamba utaratibu huu ni mojawapo ya taratibu ama tamaduni zilizosaidia kuitunza amani yetu pamoja na mshikamano.

Kilichobaki ni kupata kiongozi anayeuchukia ufisadi kiukweli!

Kuna mtu hapo nyuma nimempa mfano wa ulinzi, walinzi na makofuli.

Kofuli inaweza kuwa ni ulinzi ama ndo utaratibu tuliojiwekea sisi wenyewe ambao hauko kwenye mkataba(katiba)kama ilivyo shughuli ya mlinzi ambaye ameajiriwa(mkataba/katiba/sheria), na analinda mali pamoja na makofuli hayo yasiyokuwa na mkataba!

Hatuwezi kuacha taratibu za kupiga kofuli kwasababu eti tuna mlinzi ambaye tuna mkataba naye!

Hatuwezi kusema tusiwe makini na wakati tunafahamu hata viongozi wametoka kwenye jamii zetu!

ni utaratibu unaojenga heshima na mshikamano miongoni mwetu!

Wengi wetu tunadhani amani tuliyonayo Ipo kwa bahati mbaya!?
 
ndo manake lazima awe mkristo ..tumechoka kugeuza Ikulu kuwa sehemu ya kulia mafutari na kufanya mahitima january to december.. vile vile hatutaki rais anayenyoa upara

Heeee...yamekuwa hayo??
 
For me,awe Christian,Budha,Islam or Pagan i don't give a sh..t coz maisha yangu nahangaika mwenyewe nikilala njaa nalala mwenyewe,mimi kama Mkristo atanisaidia nini huyo rais siku nikikwama ktk maisha yangu???binafsi sijawahi'ona msaada wa rais/bunge maishani mwangu,wote wanafki kodi yangu wanagawana hovyo kwenye semina zao nikienda hospital huduma mbovu,dawa hakuna,ma-Doc wanalalamikia mishahara,elimu mbovu Walimu nao wanalalamika..barabara nazo mbovu maji ya shida uchumi nao mbovu then anatokea kima mmoja anasema eti uchumi umekua kwa 7.5%,uchumi umekua wakati mfukoni watu hela hatuna!!!!!!?labda ungetuhamasisha kupiga kura kuchagua viongozi bora wanaokataa rushwa na kuongoza vyema but sio kwa eti imani hii iongoze miaka fulani then iachie imani nyingine,kwa hivi,hata asipokuwapo huyo rais sitapata hasara wala faida.
 
Mkuu mabadiliko tuliyonayo kama Taifa, utakuwa huyatendei haki kwa utaratibu huu!

Mkuu hata hayo mataifa makubwa hizi discussions zipo.

Ninaamini kabisa kuwa hatukupata viongozi wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya!

Mkuu tena hiki ninalolizungumzia tumekuwa tukilifanya, na siyo kama hizi hoja mpya za vijana, wanawake nk!

Utamaduni huu tumetoka nao mbali sana.

Nina amini kwa dhati kabisa kwamba utaratibu huu ni mojawapo ya taratibu ama tamaduni zilizosaidia kuitunza amani yetu pamoja na mshikamano.

Kilichobaki ni kupata kiongozi anayeuchukia ufisadi kiukweli!

Kuna mtu hapo nyuma nimempa mfano wa ulinzi, walinzi na makofuli.

Kofuli inaweza kuwa ni ulinzi ama ndo utaratibu tuliojiwekea sisi wenyewe ambao hauko kwenye mkataba(katiba)kama ilivyo shghulimya mlinzi ambaye analinda mali pamoja na makofuli hayo!

Hatuwezi kuacha taratibu za kupiga kofuli kwasababu eti tuna mlinzi ambaye tuna mkataba naye!

Hatuwezi kusema tusiwe makini na wakati tunafahamu hata viongozi wametoka kwenhr jamii zetu!

ni utaratibu unaoje ga heshima na mshikamano miongoni mwetu!

Wengi wetu tunadhani amani tuliyonayo Ipo kwa bahati mbaya!
Dah kwa haya uloandika sijui hata nitakusaidia vipi.. yaani mwili wote umenisisimka kwa dhana ulokuwa nayo na sikulaumu kwa sababu Watu wengi wameanza kufikiria hivyo na wanapanda mbegu kila kukicha. hakika tutakuja vuna tulichopanda kama walotutanguliamaana hakujifunza kwa mabaya yalowahi kutokea ama tunavyopanda mbegu juu ya miamba.
 
Hahahahahahahaha,kile kibabu cjui kimekupa nn mpaka unakihusudu.Nchi hii haiendi kwa wachagga mkuu

Wachaga wamekufanya nn wewe mtu? Kama bwana wako wa kichaga kakuacha vumilia tu tafuta wa kikwe-re akuliwaze.
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amani kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
Ni zamu ya mlutherani sasa maana wao hawajawahi kuwa na rais
 
Ni zamu ya mlutherani sasa maana wao hawajawahi kuwa na rais
Ondoa wasiwasi mkuu, mlutherani ni mkristo!

Na hilo tatizo halipo kwenye jamii yetu!Hakutakuja kutokea hiyo issue ya catholic vs lutheran etc!

Kwani wasiokuwa wakristo wanawalalamikia wakristo ama wanachagua kati ya madhebu ya kikristo ie pentecoste, lutheran nk?!

Haina haja ya kucomplicate as If hii ni issue mpya.

Hilo halitakaa litokee baina ya wakristo, ni kuover think!

Issue hiyo Ingekuwa tatizo endapo taifa letu lingekuwa la kikristo!

Maana yanatokea kwenye mataifa ya kiislam(sunni vs shia), tumeyaona.Na hayo yametokana na tamaduni zao za kutokuheshimiana!

Cc Mkandara
 
Katiba ya zamani haijaandika kubadilishana wala hatutapitisha hata kwenye rasimu haipo. Mwaka 2015 sio wa hija za kikirsto hata tutake rais mkristo.

Haya ni maoni ya kutaka upendeleo wa namna fulani ndo umetufikisha hapa. Mara Nyerere alipendelea wakristo, mara Kikwete anapendelea waislamu. Kwetu muhimu ni kiongozi atakayeongoza kwa msingi wa katiba na utaratibu. Wakiongozana waislam kumi wasio mafisadi na wenye kujali mahitaji ya wananchi bila kujali imani zao itakuwa vyema, hivyo hivyo hata kwa wakristo. Hizi kelele ni ombwe la usawa ndo maana wadini hufikiri akija wa namna yao watapata ahueni kwa kuwapendelea.

Na utu uzima wangu huu sijaona rais bora kwa mkristo wala muislam. Tupanuke kifikra nje ya macho ya upendeleo, utu wEema, uadilifu ni haiba ambazo wanazo hata wasioingia makanisani na msikitini wakiwa heri kuliko mashekh na makasisi wanaotusalisha.
tunataka kuondoa dhana ya udini
 
Dah kwa haya uloandika sijui hata nitakusaidia vipi.. yaani mwili wote umenisisimka kwa dIana ulokuwa nayo na sikulaumu kwa sababu Watu wengi wameanza kufikiria hivyo na wanapanda mbegu kila kukicha. hakika tutakuja vuna tulichopanda kama walotutanguliamaana hakujifunza kwa mabaya yalowahi kutokea ama tunavyopanda mbegu juu ya miamba.
Mkuu rejea bandiko lilopita, nadhani pengine hukunipata pale niliposema kuhusu kutokuyatendea haki "mabadiliko yetu", whether mabaya au mazuri! Mengine yameletwa wakati wa uchaguzi uliopita! Na ndiyo maana nikasema mazuri kwa mabaya!

Mkuu kunawatu ambao wanachukuwa muda kubadilika na wakati na wengine ni fasta!

Nimekuja kugunduwa kuwa mojawapo ya mambo yaliyotuweka pamoja kwa muda mrefu kama taifa lenye mshikamano, basi ni utamaduni huu tuliojiwekea ambao hauko kisheria wala kwenye katiba, bali kwa utashi wetu sisi wenyewe!

Tumekuwa tukijigamba kuhusu amani yetu pasipokujuwa chachu za amani hiyo ni zipi?

Mkuu utakuja kuniambia, sishangazwi na wewe kushindwa namna ya kunisaidia! Isipokuwa nitashangazwa kama utamaduni huu utapuuzwa!
 
......Naombea kama kungekuwa na uthibitisho wa kisayansi/kihisabati ni rais gani tunamuhitaji watanzania ingekuwa raha sana.............ndiyo tabu ya siasa.........mwenye sauti ndio husikilizwa......hasa akiwa na kundi kubwa inalo muunga mkono....hata kama hana hoja za maana sana...... Ni mawazo yangu ya kizushi tu
 
Back
Top Bottom