Rafiki wa mume wangu ananitaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rafiki wa mume wangu ananitaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by anily, Apr 8, 2012.

 1. a

  anily Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman, hebu nisaidieni ktk hili, mimi nimeolewa na nnampenda sn mume wangu, sijawahi kumsaliti tokea nimekutana naye.

  Hivi keribuni amenitambulisha kwa rafiki yk ambaye alionekana mstaarabu kumbe mnafiki. Rafiki yake huyo ameoa ila cha kushangaza ananitaka mimi wakati mi ni mke wa mtu. Amekuwa akinishawishi kwa kw mme wangu ni mtu wa safari na yeye mke wake anafanya kazi mkoani. Mi nimemgomea kabisaa.

  Asa nisaidieni, je nimweleze mume wangu, ila naogopa kuharibu mahhusiano yao, na vlvl naogopa siku mume wangu akijua km jamaa ananitokea! Naombeni ushauri!
   
 2. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Unaogopa kuharibu uhusiano gani na umesha sema mwenyewe kua ni rafiki mnafiki?
  Unataka waendelee kua marafiki ili iweje? Mwambie mume wako and get him out of your life.
   
 3. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  with friends like him who needs an enemy
   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa hayo anayoyafanya huyo sio rafiki tena, wahi kuchukua hatua kabla hujawahiwa!!!.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  keshakulegeza magoti???
  Ukiona unashindwa mkataa mtu hadi usaidiwe, jua kuna tatizo mahali.
   
 6. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Yawezekana!!
   
 7. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  unamaanisha yawezekana alishamdondokea shemeji?
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Usimwambie mumeo kama huyo jamaa aliyekutongoza hakubughudhi sana maana kuna wanaume akikutongoza inakuwa kero.

  Kama ikizidi na ukalazimika umwambie mumeo basi jitahidi kutumia indirect method, mfano tu unaweza tu kumwambia mumeo. Hivi mume wangu fulani ulijuana nae vipi? Ni lazima atakuuliza kwa nini? Unamjibu, mimi ninavyomuona kama hajatulia vile yaani macho yake yapo juu juu.

  Akikuambia amekutongoza nini? Hapana ila naona kwa jinsi anavyoniangalia ni kama anataka kusema kitu ila anashindwa.

  Akija jamaa unamwambia ukiendelea kunisumbua nitamwambia mume wangu maana nimeshakwambia sitaki.

  Jambo lingine kama ushauri kwako,
  Usimpe nafasi akushike hata kiungo chako kimoja hata kwa kukusifia kisha akajitia anataka kukugusa. Akifanya hivyo kuwa mkali na uonyeshe haupendi ujinga wake huo kabisa.

  Pili kama akipiga simu usimchekee kama unongea na mpenzi wako, just be straight, hallow hallow, vipi safi. Eeeh nikusaidie nini au una shida gani? Ajue huna matani na wala haitakaa uitokee umsaliti mumeo kwa ajili yake.

  Ni hayo tu.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  anily!!

  Ushauri toka kwa Mzee wa Rula hakika inaweza ikawa bomba kbs!!


  Ila kwangu nina cha nyongeza kidogo ktk usemi huu ya kwmb "KIMLACHO MWENZIE HAKIKA KINA NJAA" tafakari kabla ya kumfikisha malalamiko meza kuu!

  Halafu ujue huyo ana tamaa tu kwn hata ukimpa atakacho atafanya nini?

  Dunia imejaa tamaa fluu!!
  Tafakari na chukua hatua anily!!
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  shemeji ni shemeji tu..................hawezi kuzima taa labda umkaribishe kwenye moyo wako.....................
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Challenge hyo!
   
 12. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Unauliza Majibu? Mwambie, huyo Hana adabu wala usimuonee Huruma.


   
 13. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  We unaonekana ushaelekezwa kibra wewe inasubiri kuchinjwa tu! Yaani hapo kuna la kuomba ushauri kweli?
   
 14. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,329
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Zingatia hapo kwa mzee wa rula.
   
 15. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inaonekana na wewe unajiachia sana manake mwanaume simjinga hadi aanze kukutongoza ni kwamba tayari kaona kamwanya cha kufanikiwa maombi yake.Cha kufanya kwanza embu kaa kidini kwanza la sivyo yatakushinda
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....anakutaka? ...wewe wajua anakutaka ili iweje? Uwe mpenzi wake 'wa pembeni'....au uwe mkewe?
  Yeah, mwambie mumeo ajue...hakuna ubaya wowote, wao ni marafiki watajuana mbele ya safari.
   
 17. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hapa kuna walakn, naamin had hapo ulipo ulishatongozwa sana na kuna ambao walifanikiwa na kuna ambao hawakufanikiwa. cdhan kama kuna jipya had uombe ushaur ktk maamuz. cdhan pia kama kuna ulazma wa maelezo zaid kwa vile inaonyesha umempa shem wako nafas na yawezekana mlishayamaliza kikubwa ila unatafuta justification cha kilichotokea.
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Ukimuambia mumeo atakuwa insecure sana na marafiki zake wote. Mshushue na kumuambia kwa macho makavu. Maneno kama 'ngoja nimuage mume wangu kuwa natoka na wewe basi' yatamuweka mbali. Lakini mponde kwa mumeo kama ulivyoshauriwa hapo juu.
   
 19. p

  poto Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nooooma!
   
 20. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Pole sana...nadhani wewe ni mnafiki zaidi. Nikuulize ni ushauri gani unaotegemea hapa? Kwa taarifa yako tu ni kuwa kama kweli unampenda mume wako ungeshamshirikisha mapema kabisa...nisema umechelewa sana. Pili kama si tabia yako kutoka nje ya ndoa yako basi huyo rafiki ya mume wako amekuona wewe ni cheap tu. Samahahi...nahisi kama umeshatembea na huyo family friend at least in your mind.

  Niseme kitendo cha wewe kushiriki ktk maongezi ya kutakana kimapenzi na kuja hapa jukwaani kutuambia kwamba "umemgomea kabisa" si sahihi hata kidogo. If I may ask huwa mnaongeleaga wapi...ni kwa simu au mume wako akiwa yupo safari? Nakushauri utubu haraka sana kwani kama ni kweli unachosema basi njia sahihi unaifahamu.
   
Loading...