Rafiki yangu wa karibu anatakwa kimapenzi na mpwa wake

Smart AJ

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
5,533
5,751
Salaam enyi watu wa Mungu, bwana weeh mi nna mshikaji wangu mmoja,ni rafiki haswa tangu huko shule ya sekondari miaka takribani miaka kumi,hivyo tunaelezana mambo mengi tu binafsi.

Sasa siku ya siku bwana,nilikuwa nae jamaa pamoja na kaka yake,ambaye kimsingi naye ni rafiki yangu ila baada ya kuunganishwa na huyu jamaa yangu.

Hiyo siku zilipigwa stories za kawaida ila katikati wakaingizia kupata ugeni ambao ni wa mtoto wa dada yao,(mama yao alishakuwa na mtoto mkubwa kabla akutane na baba yao)ila anaishi mkoani yeye na familia yake.

Siku kadhaa ni kweli kale kabinti kalifika,siku naenda kwa wanangu nakuta ugeni,na baadae nakua kutambulishwa kuwa ndio yule mgeni,ni kadada tu ka umri wa miaka pengine 17 au 18.

Kwanini hakuwa shule kwa umri huo,!?nkauliza nkajibiwa kalifeli drs la saba hivyo kalitaftiwa mume huko huko kwao(kanda ya ziwa,ila ndo ilikashinda kakasepa nakwenda mjini dar kufanya kazi za ndani,ambazo nazo kwa muda flani kalishindwa baada ya kupokea kaliyoyaita manyanyaso kutoka kwa waajiri wake wenye asili ya arabuni.

Story inaanza wana wako watatu yaani jamaa kaka yake na mdogo wao wote ni wanaume,na ni over 20yrs,mama yao sio mtu wa kushinda home ni mjasiriamali,so ka anko kalikuja wakati sahihi sana hasa kwenye usaidizi wa kazi,kwani hapo kabla jamaa walikuwa wanasimamia shoo zote wenyewe.

Na jamaa ni watu wa utani mwingi sana, hivyo walika treat ka anko with all the love and humility,kumbe ka anko ule kakadhani ule upendo una maana pana tofauti na undugu,si ndo kakamfungukia mwanangu kuwa kanamuelewa na kapo radhi hata kumtunuku vinono kwa mara ya kwanza,kwani kalikuwa bikira(kwa mujibu wake lakini,binafsi hata siamini)

Siku niko kwa mwana ananiambia kuhusu sakata hilo nikabaki nimeshika mdomo kwa kushangaa sana,INAWEZEKANAJE MPWA AMTAMANI MJOMBA YAKE??

Jamaa nilivyomsoma ana ile sitaki nataka nyingi sana ...

Ila akaniomba ushauri juu ya sakata lile,kama ambavyo huwa ananiomba na ananipa ushauri juu ya masuala mengineyo.

USHAURI WANGU NILIOMPA ULIJIKITA KWENYE MASUALA KADHAA AMBAYO YALITUKIA SIKU KADHAA NYUMA.

(i)SIKU KADHAA NYUMA,kabinti kalikuwa kanalalamika kuwa bibi yake,ambaye ni mama wa rafiki yangu kukakemea juu ya masuala kadhaa likiwemo suala la mazoea na wajomba zake.

Kuna siku nilikaskia kanalalama sana kuwa bibi anasema yake anakashutumu kuwa huenda kanamtaka jamaa kimapenzi kwani kamezidisha sana ukarimu kuliko kwa wengine,(kimsingi jamaa ni mtu mkarimu sana na ni wale watu wa kumpenda kila mtu ).

Sasa pengine nawaza mama alishaona kuna ishara za hatari zinaendela kwa haka kabinti juu ya mwanae!?

Kwa kuzingatia kigezo hiki nikamwambia jamaa,achana nako na ukaambie wazi kuwa huo haukuwa ni mpango mzuri.

(ii)SIKU KADHAA NYUMA,bahati nzuri hiyo siku sikuwa hata na wazo la kwenda kukutana na hao jamaa ila nkajikuta mguu mosi,mguu pili mpaka kwao,ilikiwa siku ya jumapili mida ya saa tisa mchana hivi.

Kufika pale kama kawaida tulisalimiana na kujadili mambo kadhaa ikiwemo kuhusu biashara ya forex,(wote sie ni traders).

Baada ya muda kadhaa kaka ake akainuka na kuelekea ndani,tukawa tunamsikia anaongea na ka anko kuhusu kwenda hospitali kwani kalionekana kuwa kanaumwa.

Dakika kadhaa jamaa alirudi na akamwambia mwanangu,”oya hebu nenda kamcheki huyu dogo naona kama anaumwa ila hataki kusema anaumwa nini”.

Jamaa aliinuka na kuelekea ndani,nikabaki peke angu kwani kaka ake alimfuata baada ya dakika mbili hivi.

Kule ndani nikawa nasikia sauti fulani za ajabu,ghafla kaka ake akaja haraka na kuchukua kikopo cha kinywaji aina ya energy,akaniambia kwa kifupi “NJOO”.

Nikainuka na kumfuata nyuma ila nikaona anaelekea chumbani kwa ka anko,nikasita kuingia nikakomea dining tu,pale dining na chumbani kwa anko hakukuwa mbali hivyo nikawa naskia kwa ukaribu sana kilichokuwa kinaendelea.

Nikawa namskia jamaa yangu anakemea mapepo,kumbe kale ka anko kalikuwa na mapepo buana.

Siku hiyo kalipandisha sana mapepo na ile chupa ya energy ndani yake ilkuwa na maji ya baraka,ambayo wana walienda kuyapata kwa baadhi ya watumishi kwa minajilibya kuwasaidia kwenye changamoto zao.

(kumbe na mama yao huwa anapandishaga mapepo tena mara kibao sana,na jamaa yangu ndo huwa anayatuliza kwani ni mlokole flani wa mchongo.....by the way mimi pia ni wale wana ambao wameokoka ila ndio hvyo tena kama mnavyojua ujana NAJUA MSHAELEWA)


HAPA NISEME JAMBO MOJA KUWA KWENYE SAFARI YA MAISHA YANGU KUNA STORY PIA NTAKUJA KUWALETEA NIKIPATA WASAHA JUU YA SAFARI YANGUBYA KIROHO NA CHANGAMOTO ZAKE)


TUENDELEE NA KISA,baada ya kuskia hivyo yule kaka yake,akachungulia mlangoni akaniita.

Nikaingia ndani na kukuta yule binti yuko chini sakafuni,huku ameshikilia kooni,(HAPA NI SUALA LA IMANI SO SIO LAZIMA UAMINI KILICHOTOKEA,ILA NI UKWELI MTUPU)

Binti alikuwa ameshikilia sehemu ya shingoni huku akilalamika,ila kwa muda ule ni wazi hakuwa yeye anayeongea......


Kuna roho zilikuwa zinaongea kupitia yeye,(she was possesed)by the so called demons.

jamaa yangu alivyoniona akanambia”dogo ameshapandisha demon mwanangu,tunafanyaje”??

Hapo washamwagia sana yale maji ya baraka kinoma dogo amelowa mpaka sio poa.

Nikamwambia ngoja tujaribu kuuliza hili pepo linataka nini!

Nikamsogelea yule binti na kumuuliza,”we ni nani na unataka nini kwa binti huyu!!!”?

Likajibu bila kupepesa maneno,”TUMEKUJA KUMUUA”

Weeeh Tukaangaliana huku jamaa anazidi kuomba sana tu,nikahoji tena we ni nani likajibu tena “MALKIA”

DUH! Hii ya leo kali sana,hapo sijawahi hata siku moja kukutana na mtu mwenye mapepp na nikamuombea,sikuwa na imani kuwa yatanitii kama wale wachungaji wakubwa,labda kutkana na imani haba.

Nikaendela kuliambia huyu hatakufa bali ataishi kushuhudia wema wa Mungu maishani mwake,nikaona ngoja niombe na mimi basi tukalikemea sana pale,yule binti akawa anagusa sana vidole vyake Kichwani kuna kitu kikanambia ombea pia pete vidoleni mwake,tujafanya hivyo na kweli bwana lile demon likawa linalia na kupiga kelele NIRUDISHIENI PETE ZANGU NA TAJIBLANGU LA MALKIA!!!

Mhhhh’!!!!nikajua kumbe hapa ishu ni very serious tukazidisha sana maombi,kuna muda yule anki akawa anarudi kwenye ufahamu wake na tunaongea naye na kumuuliza kuhusu hali yake,akajibu anaendelea vizuri kuna kitu kilikuwa kinamkaa na sasa kimeachia kwa kiasi flani.

NIKAMHOJI KUHUSU PETE AKAWA ANASEMA VIDOLE VINAWASHA KAMA VINAWAKA MOTO HIVI.

Kwa kifupi tuliomba mpaka saa 12 hivi,na yale mapepo yalisema yalikuwa 15,ila mwisho wa siku alikuja kutulia na baadaye alitoka nje na kupunga upepo kwani alikuwa na hali mbaya hata kwa kumtazama alionekana kuchoka sana,

Tulimhoji suala lile liliwahi kumtokea hapo awali,akasema ndio mnamo akiwa darasa la sita.

Nikagundua ilikuwa ni mission ya kumchukua tena baada ya mwaka huo kushindikana kwani alisema aliombewa pia.

Nikamhoji huwa anaota nini pindi akiwa amelala,yaani ndoto ambayo huwa inajirudia rudia mara nyingi,akajibu huwa anaota yuko baharini,na mara nyingi huwa anaota atakuja kuwa mtu kubwa sana kimafanikio.

Nikakumbuka wakati wa maombezi yale kuna muda tulilihoji pepo lile kwanini huyu binti na sio mwingine,LIKAJIBU KWA KUWA ANA NYOTA KALI SANA.

NISKILIZE KWA MAKINI HAPA,....IKO HIVI
WATOTO WENGI AMBAO TUNAWALEA SIO WATOTO WETU,ILA NI MIILI YAO TU WAO WAMEKUWA POSSESED NA MAPEPO, AMBAYO YANAWAFANYA WAWE NA TABIA TOFAUTI KABISA NA WAZAZI WAO(MFANO KIBURI CHA HALI YA JUU, WIZI NA UKOROFI)

HUYU BINTI PIA KWA MUJIBU WA ANKO ZAKE ALIKUWA NI MKOROFI SANA,NDIO MAANA BIBI YAKE AKAWA HATAKI KABUSA AWE NA UKARIBU NA ANKO ZAKE.

KINACHOFANYIKA HAPA NI KUWA MTOTO WAKO HUWA ANAKUA ANATUMIKA KAMA AGENT WA KUKULETEA MAJANGA,KAMA HASARA KWANI HUWA KANAIBA IBA SANA HELA HATA UKIFICHA WAPI KATAZIONA TU

ASILIMIA 90 YA WATOTO WETU WANATUMIKA NA NGUVU ZA KIZA UWE UNAPENDA AU HUPENDI,JARIBU SANA KUCHUNGUZA UTAGUNDUA KUNA VITABIA VYA UKOROFI,UJEURI,KIBURI NA WIZI KWA MWANAO.

SABABU ZIKO NYINGI SANA ZINAZOPELEKEA HAYA KUTOKEA....Kwa leo sina uwezo wa kueleza hayo ila next time nitakuja na uzi kwa wenye imani sawa na yangu watanielewa na kuchukua hatua.

Basi bwana kale kabinti kakawa kameenda kupumzika ila kabla hakajaenda nikona kanajikuna sana vidole vyake,hasa hiki cha pete((HAPA NIKAGUNDUA KITU,HAKA KABITNI KALIOLEWA NA ROHO MBAYA yaani jini kwenye ulimwengu wa kiroho.

Angalia yaani kalikuwa na SPIRIT HUSBAND AMBAYE ASILIMIA KUBWA YA MABINTI WANAKUWA NAO:KAMA USHAOTA ANAVALISHWA PETE USINGINI NA MTU USIYEMJUA NARUDIA USIYEMJUA BASI UNA MUME WA KIPEPO.NAJUA WADADA WENGI MSHAWAHI HAMNA HAJA YA KUFICHA HILI.

Dalili nyingine kuwa una huyo mume wa kipepo ni kwamba,unakuwa huna mahusiano ya kudumu....

Kuna wengine huwa wanajikuta wanagombana tu na wenzi wao bila sababu,sababu ni kwamba huyu pepo huwa anakuwa na wivu wa hali ya juu sana na wengine huwa wanawaua kabisa wenzi wenu...

MFANO KWA HUYU BINTI BAADA YA TUKIO HILI ALISHAWAHI KUTUSIMULIA KUWA ENDAPO ATAJARIBU KUINGIA TU KWENYE MAHUSIANO BASI,WATU WALE HUTOKEA KUMPENDA SANA NA KUMJALI ILA BAHATI MBAYA HUFA GHAFLA TU,NA MPAKA MUDA HUO ALISHAPOTEZA MA BOY FRIEND WAWILI AMBAO WOTE WALIKUFA VIFO VYA AJABU IKIWEMO AJALI.(kifo cha ajali ni dalili ya kafara za majini)

TUISHIE HAPA KWENYE BINTI KUPUMZIKA KWANI ALIKUWA SAWA KABISA KUTIKEA HAPO**********************************SASA RUDI KWENYE KICHWA CHA MKASA NA ZAIDI PALE KWENYE POINT NAMBA (ii)

KWANINI NILITUMIA KISA HIKI KUMSHAURI ASIKUBALI KUZINI NA ANKO WAKE!????

JIBU:NADHANI NA NINA UHAKIKA KWA 95% KUWA.....mpango wa kuzimu na lile pepo kutaka kumuua yule binti haukuwa umeishia pale yalipokubali kutoka,(MAPEPO NA WACHAWI HUWA HAWAKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI,MARA ZOTE HUJA NA MBINU MBADALA)

Basi hii nayo ilikuwa mbinu mbadala,mapepo yale yale ili kukamilisha lengo lao yakaja na mpango huu,....yakamwingia tena binti,KUMBUKA BINTI HAKUOKOKA SIKU ILE ILA ILKUWA NI KUOKOA UHAI WAKE TU,ILA BIBI YAKE ALIAHIDI KUMPELEKA KANISANI AKAOKOKE KITU AMBACHO HAKUFANYA,NA HILO LILIKUWA NI KOSA KUBWA SANA.

Binti alishawishiwa na mapepo yale amtongoze anko wake,yule yule ambaye huwa anaomba sana kama mama na anko wakiwa wamepandisha mapepo...JIULIZE KWANINI ASIWE MWINGINE ILI HALI WOTE WALIKUWA WANAMJALI SANA ..

HIVYO kama jamaa angekubali kuzini na binti yule next time yangekuja na kutaka kumuua,kama jamaa angenza kuombea na kuyakemea yangemwambia wazi ....

“HATA WEWE TUMESHAKAMATA NAFSI YAKO HIVYO HUNA MAMLAKA YA KUTUTOA SISI”

HIVYO KULIKUWA NA UWEZEKANO MKUBWA SANA WA KUMUUA BINTI YULE.

KUMBUKA UNAPOZINI NA MTU,YAFUATAYO HUTOKEA KWENYE ULIMWENGU WA KIROHO

i)Nafsi yako na ya mtu huyo huungana ma kiwa kitu kimoja,hivyo kama huyo mtu ana roho wachafu basi huikamata pia nafsi yako.

ii)Huwa mnagawana mikosi na mabalaa yote ambayo yapo kwa mmoja wenu

NDIO MAANA TUNAPASWA KUFANGA NGONO PINDI TUNAPOOA TU,NA MKE NA MUME WANATAKIWA WAWE NA USAFI WA ROHO ILI WASIAMBUKIZANE UCHAFU WA ROHONI KUPITIA TENDO LA NDO.(JAPO KWA HILI HATA MIMI NISHAKILI KUWA SIWEZI)

BAADA YA KUMSHAURI HIVI JAMAA ANAGUTUKA NA KUSEMA DUH KWELI ASEE BROH...

SIKU KADHAA BAADAYE NILIENDA KWAO BAADA YA MUDA MREFU NA AKANIPA MREJESHO UFUATAO.


NIKAMHOJI KILICHONDELA JUU YA MKASA ULE,akanijibu alifanya kumwambia kuwa lile halikuwa jambo la busara na ni la aibu kwa kuwa wao ni ndugu wa damu kabisa.

Ila nilishangaa kwa sababu ambazo sikuzielewa kwangu basi baada ya kama wiki hivi mama ya ke jamaa yangu akaamua kumtaftia kazi binti maeno ya mikumi huko...

Tena alilazimsiaha sana binti aondoke nakumbuka ilikuwa saa tisa au kumi hivi jioni,binti alipakizwa kwenye gari kutoka mkoa x na kuelekea mikumi morogoro tayari kwa kuanza kazi za ndani.

Jamaa zangu wote watatu HAWAKUFURAHIA KITENDO KILE NA WAKAWA WANAMLAUMU WAZI WAZI MAMA YAO.

Walimshutumu kwa kumtelekeza binti mdogo wa miaka 17-18 kwa kumpeleka kufanya kazi za ndani mahali pa mbali,wao walionelea ingekuwa sawa kama angeleelwa pale kama dada mdogo wao

KWENYE HILI SIKUWA NA UPANDE WA KUCHAGUA NILIAMUA KUWA AFRICA KUKAA KIMYA KWENYE MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE,LICHA YA EU KUSEMA AFRICA IAMUE UPANDE WA KUUNGA MKONO....

INGAWA ROHONI NAWIWA SANA KUMUOMBEA BINTI YULE KWANI NAJUA HUKO ALIKO BADO ANA VITA SANA NA ULIMWENGU WA GIZA.

NISAMEHENI KWA KUWACHOSHA KWA KUSOMA KISA HIKI.

Nawasilisha.
 
Hongera aisee. Unaweza ukaandika kwa aya zisizozidi mbili ishu hasa ni nini?

Hongera aisee. Unaweza ukaandika kwa aya zisizozidi mbili ishu hasa ni nini?
Ni hiv, huyu mdau ana washkaji zake wawili.wote hawataki kazi kutwa kucha kushinda maghetoni kucheza cheza forex. Jamaa zake wawil wote ni domo zege hawana madem ila wana act ni walokole full maji ya upako kumbe tu wameshindwa kumilik pisi.

Sasa ikatokea jamaa zake hao wawil walipata mgeni mtoto wa kike wa dada yao wakamtani.binti ni bikra ila alishaolewa before.Mixer wana ugwadu na sound hawana ila ndio wameanza kutamaniana hawa ndugu zikaanza sarakasi humo ndani mara bint kapandisha mapepo mara nin sijui kimsng mama yao akagundua akamuondoa huyu bint kampeleka mikumi kufanya kazi.Wadau waka mind huku wao kazi wanayofanya ni kucheza forex af wanataka mama yao awalee wao akalee na kadem kao kana kwamba maisha ni rahis.
Ila jamaa hawakufanikiwa kukatafuna hako katoto
 
Hongera aisee. Unaweza ukaandika kwa aya zisizozidi mbili ishu hasa ni nini?
Ni hiv, huyu mdau ana washkaji zake wawili.wote hawataki kazi kutwa kucha kushinda maghetoni kucheza cheza forex. Jamaa zake wawil wote ni domo zege hawana madem ila wana act ni walokole full maji ya upako kumbe tu wameshindwa kumilik pisi.

Sasa ikatokea jamaa zake hao wawil walipata mgeni mtoto wa kike wa dada yao wakamtani.binti ni bikra ila alishaolewa before.Mixer wana ugwadu na sound hawana ila ndio wameanza kutamaniana hawa ndugu zikaanza sarakasi humo ndani mara bint kapandisha mapepo mara nin sijui kimsng mama yao akagundua akamuondoa huyu bint kampeleka mikumi kufanya kazi.Wadau waka mind huku wao kazi wanayofanya ni kucheza forex af wanataka mama yao awalee wao akalee na kadem kao kana kwamba maisha ni rahis.
Ila jamaa hawakufanikiwa kukatafuna hako katoto
 
Back
Top Bottom