Q & A ya Mhe. Rais & Mhe. Abdallah Possi

Q & A ya Mhe. Rais & Mhe. Abdallah Possi

Q: Je, Abdallah Possi kuteuliwa kuwa Balozi ina maana na ubunge wake umeshakoma?

A: HAPANA, bado ni mbunge kwa sababu, uteuzi ambao ungemwondolea sifa ya ya ubunge ni endapo angeteuliwa kuwa Rais au Makamu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(b) & (f) au angetenda jambo ambalo lingempotezea sifa ya ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 71(1) (d) & (g)

Q: Je, Rais ana mamlaka ya kumvua mtu ubunge?

A: HAPANA! Hana mamlaka hayo, iwe ni mbunge wa kuchaguliwa au aliyemteua yeye mwenyewe!!

Q: Ni kwanini basi Mheshimiwa amemteua Mheshimiwa Possi kuwa Balozi?

A: Hiyo ni namna nyingine ya Rais kusema nimechemka kuteua Wabunge 6 wanaume kati ya Wabunge 10 manake huo ni uvunjwaji wa katiba ulio wazi!!!

Q: Kwahiyo hivi sasa tunaweza kumzodoa baada ya kukiri amechemka?

A: Hapana, sio vizuri hivyo! Lakini kubwa kuliko yote, hukumu ya faini hivi sasa imelazimishwa kwenda likizo, kwahiyo hata kama una milioni 7 za kuchezea; hazitakusaidia ndugu!

Q: Basi sawa yaishe... lakini si ulisema kumteua mtu ubalozi hakumuondolei sifa yake ya ubunge! Basi tunamuonea Mheshimiwa Rais tunapohusisha uteuzi wa Abdallah Possi kuwa Balozi na lile la kuteua wabunge 6 wanaume!

A: Sikiliza wewe, kusoma hujui hata picha ukutani huzioni? Kwanza nasisitiza! Uteuzi huu HAUMUONDELEI sifa ya kuwa mbunge lakini huu ni mwanzo wa next episode ya this political drama!

Muda mfupi ujao, Mheshimiwa Possi atalazimika kutangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge kwa madai kwamba, mosi, ili apate nafasi ya kutosha kuitumikia nchi yake kama balozi lakini pili; kwa madai ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mtu mmoja kutorundikiwa cheo zaidi ya kimoja!

Q: Alaa!! Kwa mbaaaaaaali, nimeelewa lakini hilo la Mbunge kujiuzuru ni jipya kwangu!
A: Hamna namna, soma aya ya mwisho kabisa hapo chini!!!

KATIBA:

71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -

(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;

(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;

(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;

(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;

(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge,

lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
Katiba inasemaje kuhusu sifa za waziri mkuu? Mbunge wa kuchaguliwa tu au hata wakuteuliwa?
 
Katiba inasemaje kuhusu sifa za waziri mkuu? Mbunge wa kuchaguliwa tu au hata wakuteuliwa?
Lazima awe mbunge wa kuchaguliwa kutoka jimbo la uchaguzi.
 
Mkuu Chige, hii ni number nyingine, ila ingekuwa issue ni realization ya kuchemsha, angetengua uteuzi wa mmoja wa hao wateule wapya kabla hajaapishwa.

Ni kweli Dr. Posi atamwandikia Spika barua ya kujiuzulu, hivyo wabunge wanaume wa kuteuliwa wabakie 5, ila watu msianze kushangilia kwa kudhania atateua wabunge wanawake 3 ili watimie watano, anaweza kuteua au anaweza asiteue simply kwa sababu Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo vya kuteuliwa.

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! .

Paskali
Awamu zote zilizopita hasa awamu ya nne wanawake walikua wengi na waliteuliwa kulingana na nafasi kikatiba!
Imekuaje awamu hii wanawake wawe wachache washindwe kuziba nafasi hizo?

Awamu hii na wanawake kunakitu tu hapo
 
U are being so unfair Paskalli!!! Unless una maelezo mengine ya ziada haujayaweka kwenye haya maandiko yako
Mkuu you are real mamii the best, kwa sababu kabla ya kulaumu umehoji kama nina maelezo mengine, ili ku justfy hoja yangu, na ikiwa sina au yasipojitosheleza, ndipo ninakuwa so unfair.

Nimetumia simpo logic, kuwa mkuu anateua watu wenye sifa fulani anazotaka ili kuwa wabunge wa kuteuliwa, katiba inamtaka kama atateua wote 10, anapaswa ateua angalau wanawake 5!. Kitendo cha rais kuteua wanaume 6 na wanawake wawili tuu, ni uthibitisho, kwenye sifa na vigezo anavyovitaka, hakuna wanawake hao, ndio maana kateua wanaume 6!.

Ufafanuzi mzuri kabisa nimeuweka hapa,
Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! .

Karibu.

Paskali
 
Awamu zote zilizopita hasa awamu ya nne wanawake walikua wengi na waliteuliwa kulingana na nafasi kikatiba!
Imekuaje awamu hii wanawake wawe wachache washindwe kuziba nafasi hizo?

Awamu hii na wanawake kunakitu tu hapo
kila mtu na vigezo vyake, awamu iliyopita kiukweli aliwabeba sana hawa watu, hata wasio na vigezo waliteuliwa tuu!, awamu hii, hakuna kubeba, ni sifa na vigezo tuu!, wanawake wamekosekana, wanaume wameteuliwa!. Wangekuwepo wenye sifa na vigezo, si wangeteuliwa!.

Paskali
 
kila mtu na vigezo vyake, awamu iliyopita kiukweli aliwabeba sana hawa watu, hata wasio na vigezo waliteuliwa tuu!, awamu hii, hakuna kubeba, ni sifa na vigezo tuu!, wanawake wamekosekana, wanaume wameteuliwa!. Wangekuwepo wenye sifa na vigezo, si wangeteuliwa!.

Paskali
Nahisi kigezo awamu hii itakua Phd na kuendelea
 
Labda tujiulize kabla ya kulaumu au kuona rais kachemka,,je rais alikua hajui kua anapaswa kuteua watano?na je alimteua Mr posi bila kumpa taarifa?na je kama lengo lake ni kuoanisha idadi sawa na watano kila upande je hatuoni kua alishaona hali hyo ndio maana akamtoa posi ili idadi iwe kamili?je tunataka kuamini kua mitandao ya kijamii ndio imemkumbusha rais? Hapana alishaamua kabla ya lawama za kukosoa na ndio maana hali ikawa hii,mabalozi hawajateuliwa Leo hao waliopangiwa vituo Jana Ila tunaweza kusema kimoja kilitangazwa kabla ya kingine ambacho kilipaswa kutangazwa,so hakuna kosa LA kiufundi vyote vimezingatia utaratibu
Maelezo yako karibu yote ni assumptions lakini itoshe tu kusema, kwa kuzingatia hapo kwenye RED, huwezi kuvunja sheria kwavile tu unafahamu utakuja kurekebisha uvunjaji huo baadae! Lililo wazi ni kwamba, kwa mujibu wa barua ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Dr. Abdallah Possi ameteuliwa ubalozi tarehe 19.01.2017 yaani jana wakati uteuzi wa akina Bulembo ulifanyika kabla ya hapo!
 
Kwa possy kwa kujivuaa ubunge kwa kusema anahama chama hapo kuna ulakini maana possy kwa alivyoingiaa bungeni anaonekana ni neutral hana chama ila najua ni ccm
 
Wasioamini kwamba kuna wanawake wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi ni wale waliolelewa na wa jinsi hiyo.vicevrsa vivo hivyo
 
Mkuu Chige, hii ni number nyingine, ila ingekuwa issue ni realization ya kuchemsha, angetengua uteuzi wa mmoja wa hao wateule wapya kabla hajaapishwa.

Ni kweli Dr. Posi atamwandikia Spika barua ya kujiuzulu, hivyo wabunge wanaume wa kuteuliwa wabakie 5, ila watu msianze kushangilia kwa kudhania atateua wabunge wanawake 3 ili watimie watano, anaweza kuteua au anaweza asiteue simply kwa sababu Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo vya kuteuliwa.

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! .

Paskali
Pascal, nawaza kwa tu kwa kuandika haya:

1) Wakati kuna wasomi wachache waliobobea nchini kwenye Sheria ya Kikatiba (Constituional Law), humu jamvini tuna nguli kibao wa sheria na tena wa Sheria hiyo! Hakija nchi hii imebahatika. Lakini najiuliza, kwa nini hawajitokezi wazi hadharani kulipeleka swala mahamakani badala ya kujificha nyuma ya ID!

2) Humu jamvini tuna watu wenye vipaji sana kiasi kuwa wana na uwezo wa kumsoma Rais na kuashiria atakachofanya. Kateua wabunge wawili, kelele ati kavunja Katiba! Kateua Mbunge aliyemteua kuwa Balozi, ehe, anarekebisha makosa! Hivi Taasisi yake na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuna asiyejua Katiba! Kama ni kweli basi ofisi hiyo ivunjwe!"

3) Au ni nafasi iliyopo ya usiri mitandaoni, kila kukicha tunaandika kinachoingia kichwani!

Siamini na sintoamini kwamba Ikulu na Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali kuna vilaza wa Sheria, iwapo ni kweli, uteuzi wa sasa wa Rais umevunja Katiba!
 
Hivi mtu wa level ya udaktari wa sheria analazimika kumpisha bulembo?

Kweli ccm janga la taifa

Ndiyo. Kwani huoni hao kina Mpango na usomi wao wanakotupeleka?? Huoni hao kina Masaju na ubobevu wao wa Sharia wanakompeleka Mkulu?? Hao wasomi wako ni janga. Heri mtaalam wa ARV faki abaki
 
Pascal Mayalla unawadhalilisha wanawake japo sijasoma hiyo link ya Uzi uliouweka. Hiyo ni tuhuma Kali sana lusema hakuna wanawake wenye sifa za kuteuliwa ubunge.

Sasa kama wanaume tu ndio wenye sifa za kuteuliwa ubunge, kwanini amteue mbunge wa kuteuliwa kuwa balozi? Ikumbukwe anapinga MTU mmoja kuhodhi vyeo.

Bottom line, kuna makosa ya kikatiba yalifanyika kwenye hizi teuzi za wabunge. Nnachosikitika bado makosa mengine yanaweza kufanyika kwa lengo la kurekebisha kosa la awali.
Makosa hayo ni heri, yatufanya tuisome katiba na kujua madhaifu yake. Makosa yanatufanya tujue uwezo wa mwanasheria mkuu ktk taaluma ya sheria.
 
Back
Top Bottom