Aisee hii kweli siasa naomba niulize tu,kwa mfano Dr. Possy akagoma kujiuzulu vipi hatma ya mkulu??
Hata Mimi nilitaka kumwambia kuwa tiyari Dr Abdallah Posi kwa kuteuliwa kuwa balozi inamuondolea sifa ya kuwa mbunge kwa kuwa balozi Ni Executive officerKuhusiana na mada yako kuhusu sifa za mbunge kutokuwa mbunge tena soma hii ibara ya Katiba;
71(1)(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Sasa swali la kujiuliza, ni jambo gani ambalo linamfanya mtu asiwe na sifa ya kuwa mbunge?
Soma ibara hii ya Katiba;
67(2)(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
Je, Balozi ni afisa mwandamizi katika utumishi wa serikali ya Tanzania?
Kama balozi ni afisa mwandamizi wa serikali basi kuteuliwa kwa Possi kuwa balozi na kukubali uteuzi huo kunamfanya automatically kukosa sifa ya kuwa mbunge bila hata ya kuandika barua ya kujiudhuru.
Hii ni haina tofauti na mbunge akihukumiwa kwenda gerezani kwa miezi zaidi ya sita kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu. Huyu anakuwa amekosa sifa ya ubunge na kwa maana hiyo, barua ya kujiudhuru ni non-essential.
Absolutely correct. Kitendo cha kukubali kuwa BALOZI kinafuta ubunge wake. Spika atatakiwa kutangaza mbunge huyo amepoteza ubunge wake kwa kukubali kuwa balozi. Option 2, ni Possi kuandika barua ya kujihuzulu ubunge. Hii iko wazi zaidi.Tuendelee kuijadili katiba yetu.
Ni ukweli mtupu rais hana uwezo wa kumtumbua mbunge baada ya kumteua na kuapishwa. Ana uwezo wa kuteua lakini sio kutengua.
Lakini kifungu 67 (2)a kinasema
Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge-
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
Sasa nenda kwenye kifungu 71 (1)a
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake
katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au
apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au
kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii
Kwa vifungu hivyo viwili, bwana Possi aakikubali tu kuapishwa kama Balozi, automatically ubunge wake unapotea.
Tujadili.
Nilishaongea jambo sawa na hili kwenye post #34!!!Tuendelee kuijadili katiba yetu.
Ni ukweli mtupu rais hana uwezo wa kumtumbua mbunge baada ya kumteua na kuapishwa. Ana uwezo wa kuteua lakini sio kutengua.
Lakini kifungu 67 (2)a kinasema
Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge-
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
Sasa nenda kwenye kifungu 71 (1)a
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake
katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au
apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au
kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii
Kwa vifungu hivyo viwili, bwana Possi aakikubali tu kuapishwa kama Balozi, automatically ubunge wake unapotea.
Tujadili.
lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
Lazima ajiuzulu vinginevyo ataendelea kuwa mbunge!!Absolutely correct. Kitendo cha kukubali kuwa BALOZI kinafuta ubunge wake. Spika atatakiwa kutangaza mbunge huyo amepoteza ubunge wake kwa kukubali kuwa balozi. Option 2, ni Possi kuandika barua ya kujihuzulu ubunge. Hii iko wazi zaidi.
Kwani kuwa Mbunge inalazimu kuwa Daktari wa Sheria? Then, Bulembo siyo mtu wa kumdharau, ana mafanikio katika maisha yake inawezekana kuliko baba yako. Wewe mpaka umemjua hapo alipo hakufika hivihivi, kuna watu wazito ndani ya chama chake wanamjua uwezo wake na kumwamini. Acha ku underestimate mtu usiomjua vizuri.Hivi mtu wa level ya udaktari wa sheria analazimika kumpisha bulembo?
Kweli ccm janga la taifa
Dah hapa hakuna namna lazima atangaze kujiuzuru dah aibu. Jamaa Pole Mkuu Kaingia chaka BAYA.Q: Je, Abdallah Possi kuteuliwa kuwa Balozi ina maana na ubunge wake umeshakoma?
A: HAPANA, bado ni mbunge kwa sababu, uteuzi ambao ungemwondolea sifa ya ya ubunge ni endapo angeteuliwa kuwa Rais au Makamu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(b) & (f) au angetenda jambo ambalo lingempotezea sifa ya ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 71(1) (d) & (g)
Q: Je, Rais ana mamlaka ya kumvua mtu ubunge?
A: HAPANA! Hana mamlaka hayo, iwe ni mbunge wa kuchaguliwa au aliyemteua yeye mwenyewe!!
Q: Ni kwanini basi Mheshimiwa amemteua Mheshimiwa Possi kuwa Balozi?
A: Hiyo ni namna nyingine ya Rais kusema nimechemka kuteua Wabunge 6 wanaume kati ya Wabunge 10 manake huo ni uvunjwaji wa katiba ulio wazi!!!
Q: Kwahiyo hivi sasa tunaweza kumzodoa baada ya kukiri amechemka?
A: Hapana, sio vizuri hivyo! Lakini kubwa kuliko yote, hukumu ya faini kwenye haya mambo hivi sasa imelazimishwa kwenda likizo, kwahiyo hata kama una milioni 7 za kuchezea; hazitakusaidia ndugu!
Q: Basi sawa yaishe... lakini si ulisema kumteua mtu ubalozi hakumuondolei sifa yake ya ubunge?! Kama ndivyo, basi tunamuonea Mheshimiwa Rais tunapohusisha uteuzi wa Abdallah Possi kuwa Balozi na lile la kuteua wabunge 6 wanaume!
A: Sikiliza wewe, kusoma hujui hata picha ukutani huzioni? Kwanza nasisitiza! Uteuzi huu HAUMUONDELEI sifa ya kuwa mbunge lakini huu ni mwanzo wa next episode ya this political drama!
Muda mfupi ujao, Mheshimiwa Possi atalazimika kutangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge kwa madai kwamba, mosi, ili apate nafasi ya kutosha kuitumikia nchi yake kama balozi lakini pili; kwa madai ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mtu mmoja kutorundikiwa cheo zaidi ya kimoja!
Q: Alaa!! Kwa mbaaaaaaali, nimeelewa lakini hilo la Mbunge kujiuzuru ni jipya kwangu!
A: Hamna namna, soma aya ya mwisho kabisa ya Katiba Ibara ya 71(1) hapo chini!!!
KATIBA:
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;
(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge,
lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.
Pascal Mayalla unawadhalilisha wanawake japo sijasoma hiyo link ya Uzi uliouweka. Hiyo ni tuhuma Kali sana lusema hakuna wanawake wenye sifa za kuteuliwa ubunge.
Sasa kama wanaume tu ndio wenye sifa za kuteuliwa ubunge, kwanini amteue mbunge wa kuteuliwa kuwa balozi? Ikumbukwe anapinga MTU mmoja kuhodhi vyeo.
Bottom line, kuna makosa ya kikatiba yalifanyika kwenye hizi teuzi za wabunge. Nnachosikitika bado makosa mengine yanaweza kufanyika kwa lengo la kurekebisha kosa la awali.
Nakushauri usubiri ugombee Urais 2020 kwa kuwa unaijua Katiba vizuri na madaraka ya Rais.Kinacho sikitisha ni kuona kijana msomi na msafi akifanywa ndo kondoo wa msiba. Bora angetengua uteuzi wa buhemba kwani bado hajawa mbunge kwani hajaapishwa.
Posi kijana huyu ingekua hazina kuu ya baadae ya ccm na taifa. Badala ya kumwacha kupata usoefu zaidi wizarani tunampa ubalozi akapotee kitaalam na ki elimu.
Ushauri wangu kwa bwana Posi ukipelekwa ubalozi tumia muda huo kujisomea zaidi huko nje.
Umekua mpole ghaflaYaliyopita si ndwele tugange yajayo