Q: Je, Abdallah Possi kuteuliwa kuwa Balozi ina maana na ubunge wake umeshakoma?
A: HAPANA, bado ni mbunge kwa sababu, uteuzi ambao ungemwondolea sifa ya ya ubunge ni endapo angeteuliwa kuwa Rais au Makamu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(b) & (f) au angetenda jambo ambalo lingempotezea sifa ya ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 71(1) (d) & (g)
Q: Je, Rais ana mamlaka ya kumvua mtu ubunge?
A: HAPANA! Hana mamlaka hayo, iwe ni mbunge wa kuchaguliwa au aliyemteua yeye mwenyewe!!
Q: Ni kwanini basi Mheshimiwa amemteua Mheshimiwa Possi kuwa Balozi?
A: Hiyo ni namna nyingine ya Rais kusema nimechemka kuteua Wabunge 6 wanaume kati ya Wabunge 10 manake huo ni uvunjwaji wa katiba ulio wazi!!!
Q: Kwahiyo hivi sasa tunaweza kumzodoa baada ya kukiri amechemka?
A: Hapana, sio vizuri hivyo! Lakini kubwa kuliko yote, hukumu ya faini kwenye haya mambo hivi sasa imelazimishwa kwenda likizo, kwahiyo hata kama una milioni 7 za kuchezea; hazitakusaidia ndugu!
Q: Basi sawa yaishe... lakini si ulisema kumteua mtu ubalozi hakumuondolei sifa yake ya ubunge?! Kama ndivyo, basi tunamuonea Mheshimiwa Rais tunapohusisha uteuzi wa Abdallah Possi kuwa Balozi na lile la kuteua wabunge 6 wanaume!
A: Sikiliza wewe, kusoma hujui hata picha ukutani huzioni? Kwanza nasisitiza! Uteuzi huu HAUMUONDELEI sifa ya kuwa mbunge lakini huu ni mwanzo wa next episode ya this political drama!
Iko hivi, muda mfupi ujao, Mheshimiwa Possi atalazimika kutangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge kwa madai kwamba, mosi, ili apate nafasi ya kutosha kuitumikia nchi yake kama balozi lakini pili; kwa madai ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mtu mmoja kutorundikiwa cheo zaidi ya kimoja!
Q: Alaa!! Kwa mbaaaaaaali, nimeelewa lakini hilo la Mbunge kujiuzuru ni jipya kwangu!
A: Hamna namna, soma aya ya mwisho kabisa ya Katiba Ibara ya 71(1) hapo chini!!!
KATIBA:
71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;
(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;
(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge,
lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake.