Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,665
- 15,554
Serikali imetoa ufafanuzi kwa umma kufuatia taarifa iliyoelezwa kuwa potofu iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuhusu uteuzi wa Mbunge uliofanywa na Rais Samia Aprili 2, 2026 chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba.
Katika ufafanuzi huo, Serikali imeeleza kuwa ni kweli kwamba kabla ya uteuzi huo, Angela Kizigha alikuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Hata hivyo, imefafanua kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 51(3)(c) ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mbunge wa EALA hukoma kushika nafasi hiyo pindi anapoteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la nchi mwanachama.
Soma: LHRC: Uteuzi wa Angela Kizigha kuwa Mbunge unavunja masharti ya mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kutokana na masharti hayo ya kisheria, Serikali imebainisha kuwa ubunge wa EALA kwa Mheshimiwa Angela Kizigha, pamoja na Waheshimiwa Dkt. Ngwaru Maghembe na James Milya, ulikoma mara baada ya kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Serikali imeeleza kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 50 ikisomwa pamoja na Ibara ya 52 ya Mkataba huo, Bunge la nchi mwanachama lina mamlaka ya kujaza nafasi zilizo wazi katika Bunge la Afrika Mashariki kulingana na ratiba zake na taratibu husika.
Tazama alivyoapishwa: Angela Kizigha na Dkt. Evaline Munisi waapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Tanzania, Aprili 9, 2026
Kwa msingi huo, Bunge la Tanzania linatarajiwa kujaza nafasi tatu zilizoachwa wazi, kwa kuzingatia ratiba ya shughuli za Bunge. Serikali imeongeza kuwa mchakato huo utaanzia katika vyama vya siasa ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 50(1) ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Serikali imesisitiza kuwa hakuna mgongano wowote kati ya uteuzi uliofanywa chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na masharti ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hivyo basi, wananchi wamehimizwa kupuuza taarifa iliyotolewa na LHRC kuhusu suala hilo, kwa kuwa si tafsiri sahihi ya masharti ya Mkataba huo.