Q & A ya Mhe. Rais & Mhe. Abdallah Possi

Q & A ya Mhe. Rais & Mhe. Abdallah Possi

Mkuu Chige, hii ni number nyingine, ila ingekuwa issue ni realization ya kuchemsha, angetengua uteuzi wa mmoja wa hao wateule wapya kabla hajaapishwa.

Ni kweli Dr. Posi atamwandikia Spika barua ya kujiuzulu, hivyo wabunge wanaume wa kuteuliwa wabakie 5, ila watu msianze kushangilia kwa kudhania atateua wabunge wanawake 3 ili watimie watano, anaweza kuteua au anaweza asiteue simply kwa sababu Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo vya kuteuliwa.

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! .

Paskali
paskali kwani bulembo ana sifa zipi kuzidi mke wako?

au kuzidi juliana shonza
 
Mkuu Chige, hii ni number nyingine, ila ingekuwa issue ni realization ya kuchemsha, angetengua uteuzi wa mmoja wa hao wateule wapya kabla hajaapishwa.

Ni kweli Dr. Posi atamwandikia Spika barua ya kujiuzulu, hivyo wabunge wanaume wa kuteuliwa wabakie 5, ila watu msianze kushangilia kwa kudhania atateua wabunge wanawake 3 ili watimie watano, anaweza kuteua au anaweza asiteue simply kwa sababu Tanzania hatuna wanawake wa kutosha wenye sifa na vigezo vya kuteuliwa.

Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa! .

Paskali
Kwa mkuu anayemuhitaji ni Dr Tulia Ackson pekee?
 
halafu toka mwanzo wakati ule wa kuunda baraza la mawaziri watu walihoji kweli kuhusu uteuzi wa wabunge wengi walisema huyu inakuwaje anateua mara moja wengi hivi huko mbele akipatwa na shida atapata wapi hizi nafasi tena? Da maskini Possi bora angebaki UDOM kufundisha ubalozi hauna kitu, atapoteza muda wake tu badala ya kujenga carrer yake awe Prof. Retirees ndo wanatakiwa wawe mabalozi....Du so sorry
 
Kwa aibu kama hii lazima mawaziri, makatibu wakuu na watumishi waandamizi wa serikali wabaki midomo wazi. Hivi huyu Rais ana washauri?

Anao ila nasikia akikutana nao badala ya wao kumshauri yeye ndo anawashauri..cha kusikitisha ushauri anaowapa ndo kama tunavoona..
 
Pascal Mayalla unawadhalilisha wanawake japo sijasoma hiyo link ya Uzi uliouweka. Hiyo ni tuhuma Kali sana lusema hakuna wanawake wenye sifa za kuteuliwa ubunge.

Sasa kama wanaume tu ndio wenye sifa za kuteuliwa ubunge, kwanini amteue mbunge wa kuteuliwa kuwa balozi? Ikumbukwe anapinga MTU mmoja kuhodhi vyeo.

Bottom line, kuna makosa ya kikatiba yalifanyika kwenye hizi teuzi za wabunge. Nnachosikitika bado makosa mengine yanaweza kufanyika kwa lengo la kurekebisha kosa la awali.

Great thinkers tuwe na uzoefu wa kusoma miandiko (hati) ya wachangiaji humu. Kwa kumlaumu Paskali ni wazi kuwa hadi leo hujaelewa 'mwandiko' wa huyu mchangiaji maarufu. Ikibidi rudia rudia maandishi yake, utamwelewa. Anaandikaga mlazo wa kinyume nyume sana.Ni hayo tu.
 
Naomba kusaidiwa majina 6 ya wateule wa wakiume wa rais bungeni
 
Nadhani, kwa busara tu, akishapangiwa kituo cha kazi anakuwa amejivua ubunge.....mfano Dr migiro alipokwenda UN

Sikumbuki vzuri hv Dr Migiro alipoenda UN nafasi yake ya ubunge wa kuteuliwa ilijazwa??
 
Kwani nani kasema huyu mtu ni muumini wa kinachosemwa kwenye katiba? "Katiba siyo kipaumbele changu". Kama ingekuwa huyu mtu ni muumini wa katiba angemshauri Possi ajiuzulu kwanza kabla ya kuteua mwanaume mwingine. kwa hiyo hadi sasa kuna wabunge 6 wanaume wa kuteuliwa. Hivi ni kweli washauri wa huyu mtu wanatimiza kazi yao ambayo sisi wote tunawalipa? Mbona wanaitilia aibu nchi? Kwanini lakini?
 
Hivi mtu wa level ya udaktari wa sheria analazimika kumpisha bulembo?

Kweli ccm janga la taifa
Hawa wanataaluma waliokubali kuja kusujudia siasa wameamua kwa makusudi kuja kudhalilishwa na taaluma zao🙁🙁
 
Nimejitendea haki mkuu, lakini hapa tunaongelea ukiukwaji wa katiba. Hiyo ya sifa za wanawake tuiweke pembeni kwanza. Hoja ni wabunge zaidi ya watano kiume wameteuliwa, ikiacha nafasi mbili tukiongeza na mbili zilizopo zinakua NNE kwa wanawake. Contrary to the current katiba iwe ya kiswahili au ya kiingereza.

Na kuonyesha kwamba kuna tatizo, ndio imekuja hii ya uteuzi wa mbunge mteule kuwa balozi.

Katiba kwa nchi za kiafrika ni utata mtupu.
Mkuu, huwa unamsoma vizuri pasco? Huyu anaweza kuweka heading kama ya magazeti ya shigongo vile lakini utakachokuta humo ndani utashangaa.
 
Great thinkers tuwe na uzoefu wa kusoma miandiko (hati) ya wachangiaji humu. Kwa kumlaumu Paskali ni wazi kuwa hadi leo hujaelewa 'mwandiko' wa huyu mchangiaji maarufu. Ikibidi rudia rudia maandishi yake, utamwelewa. Anaandikaga mlazo wa kinyume nyume sana.Ni hayo tu.

Endelea kufuatilia Uzi, huko mbele nimesoma na nikatoa maoni yangu.
 
Possible polite grounds
1.Kujihuzuru
2.Kutohudhuria vikao 3 kwa mfululizo bila taarifa kwa Spika.

Kujihuzuru! Naamini ni uwezo wa akili na sio typo au ni typo na si uwezo wa akili. Mojawapo kati ya haya mawili linawezekana.
 
Aisee hii kweli siasa naomba niulize tu,kwa mfano Dr. Possy akagoma kujiuzulu vipi hatma ya mkulu??
Akigoma kujiuzulu Ibara hiyo hiyo ya ukomo wa Ubunge inaweza kumhusu kwa njia nyengine..... Labda ya "kifo cha mapema zaidi"
 
Back
Top Bottom