Promotion za leo jeshini zimenistua

Promotion za leo jeshini zimenistua

Ninavyofahamu rank jeshini ni stahili ya mtu na sio favour

Anyway siku hizi naona hapa nchini tunaenda na mdundo tu maana chochote kitakachofanywa na jiwe watu wanasema ni sahihi
Rank za chini ndio stahili ya mtu, lakini kwa maafisa wakuu kuanzia brigadier general ni vile Amirijeshi mkuu itakavyompendeza. Are we together?

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Mnaongelea mifumo tofauti hapo, tanzania ipo wazi katika miaka ya kustaafu na ndio maana hata mtu akipanda cheo mapema sawa ila inapokuja umri wa kustaafu anaondoka. Sasa sijui nyie mnaongelea kupanda cheo badala ya miaka ya kustaafu?!
MASAMILA

ᵃʳᵉᵉᵐ
Nadhani hukuelewa post uliyokwoti. Ni kwamba system za Magharibi na hasa Marekani ukishakuwa General officer unatakiwa uwe 4-star wakati unafikisha umri wa kustaafu-yaani unazeeka. Sasa iwapo njia ya kelekea hizo 4-star itakwama hapo katikati basi unastaafishwa kabla ya kufikia umri wa kustaafu kwani hawawezi kuendelea kukuweka General officer hadi uzeeke wakati huna uwezekano wa kufikia 4-star. Ina maana kuwa unatakiwa uwe na promotion za haraka haraka, siyo zaidi ya miaka mitatu kwa kila rank. Kuna kustaafu kwa kufikisha umri wa kutumikia jeshi, na kuna kustaafu kwa kukwakama njia ya ya kufikia 4-star general na hiyo ni hutokea kbal hujafikisha umri wa kustaafu
 
Narudia tena kwako na wewe hata kama unaanzia kwa brigedia. Inachotakiwa useme brigedia jenerali na sio je jenerali tu, kwa maana hata kama unaanzia kwa brigedia ila upo kwa ngazi mbali mbali
Brigedia hadhi yake ni nyota 1 na ndio maana anaitwa (single star jeneral), meja generali hadhi yake ni nyota 2 (2star jeneral), luteni jenerali hadhi yake ni nyota 3 (3star general). Ukisema neno general peke yake basi ujue unamaanisha mwenye hadhi ya nyota 4 (4star general).

ᵃʳᵉᵉᵐ
Sawa kabsa mkuu......na watu waelewe kwamba, kwa wanajeshi wote ambao bado wanatumikia nchi ( hawajastaafu)... cheo cha jenerali ni kwa mwanajeshi mmoja tu, mfano kwa sasa Tanzania, Jenerali ni Mabeyo pekeyake hakuna mwingine, ukiskia mwingine ujue huyo ni CDF mstaafu.
 
Awamu hii tutashuhudia mambo mengi ya ajabu ambayo hayajawahi tokea tokea dunia iumbwe
 
Sawa kabsa mkuu......na watu waelewe kwamba, kwa wanajeshi wote ambao bado wanatumikia nchi ( hawajastaafu)... cheo cha jenerali ni kwa mwanajeshi mmoja tu, mfano kwa sasa Tanzania, Jenerali ni Mabeyo pekeyake hakuna mwingine, ukiskia mwingine ujue huyo ni CDF mstaafu.
Sahihi kabisa

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Nimecheki sana CV za majenerali wa UK wa zama hizi yaani wao licha ya kuwa na experience ya kufanya operesheni na formations kubwa kubwa kama Brigades, Divisions hawajaruka ranks kwa miezi aisee

Hapa nchini kituko huyo alietumia miezi kupanda hadi u'meja jenerali' hajawahi kuwa kamanda brigedi

Kichuguu anadai ni sahihi kutumia miezi kufika meja jenerali

Wewe unachukulia kuwa Jeshi la Tanzania lifuate system ya Jeshi la uingereza one-to-one, hapana, hiyo siyo kweli. Maafisa wa jeshi la Uingereza hawafanyi kazi za serikali; wakati Tanzania kuna magenerals na makanali wanafanya kazi za serikali. Uingereza kila general ana Command ya kijeshi, Tanzania siyo kila general officer ana command, kuna general officers wengi hawana command yoyote. Tuna brigadier general wengi kuliko idadi ya brigade zilizopo.

Mwisho elewa kuwa General officer yeyote katika TPDF anapandishwa na Amiri jeshi mkuu kwa kushauriana na watu wawili tu: CDF na Chief of Staff. Hakuna guideline yoyote ya kupandishwa inayotaka mtu akae na cheo kimoja muda mrefu au awe amecommand unit yoyote ya kijeshi; in fact mtu anaweza kupandishwa kutoka Kanali kuwa Major General bila kuwa Brigadier general. Kuna Twalipo alipanda kutoka Luteni kanali (mkuu wa mkoa wa Ziwa Magharibi wakati huo) hadi na kuwa Lt General Mkuu wa Majeshi. Na Sarakikya naye alipanda kutoka Captain hadi kuwa Brigadier; ndiyo system yetu hiyo na wala uslalamike. In fact kuna mageneral officers wengi waliopanda kwa utaratubu huo ila ni kwa vile huyu anajulikana kuwa alipandishwa kuwa Brigadier general hadharani mwaka mmoja ulioopita( siyo miezi bali ni mwaka umepita), lakini ukichokonoa ndani ya jeshi utakuta wapo wengine wengi.
 
Mwisho elewa kuwa General officer yeyote katika TPDF anapandishwa na Amiri jeshi mkuu kwa kushauriana na watu wawili tu: CDF na Chief of Staff. Hakuna guideline yoyote ya kupandishwa inayotaka mtu akae na cheo kimoja muda mrefu au awe amecommand unit yoyote ya kijeshi; in fact mtu anaweza kupandishwa kutoka Kanali kuwa Major General bila kuwa Brigadier general. Kuna Twalipo alipanda kutoka Luteni kanali (mkuu wa mkoa wa Ziwa Magharibi wakati huo) hadi na kuwa Lt General Mkuu wa Majeshi. Na Sarakikya naye alipanda kutoka Captain hadi kuwa Brigadier; ndiyo system yetu.
Kama hajaelewa hapa basi ana matatizo yake binafsi.

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Usishangae maana inawezekana tu wengine mara ya mwisho kupandishwa vyeo ilikuwa mwaka 2008 sasa sijui unasemaje kwa hawa maana hadi leo hawajapandishwa vyeo
Kupanda kwa mkubwa wa karanga karanga leo kutoka ubrigedia hadi meja jenerali ndani ya miezi aisee nimepigwa na bumbuazi

Anyway katika taaluma ya kijeshi cheo mtu hapandi haraka haraka au kurushwa kwa kigezo cha uwezo au umahiri peke yake bali kuna kitu experience (service)

Wanaohusika kushauri hilo sidhani kama wameshauri (CDF nadhani), ngazi za kijeshi (ranks) zina heshima na mantiki yake kwa kila ngazi

Makakala pamoja na umahiri wake na kipaji mpaka anastaafu hakurushwa rushwa kutoka rank moja kwenda nyingine kwa miezi

Kama mtu analijua jeshi basi atakubaliana nami kuwa katika Merit jeshini maafisa wanafanana tu hawajapigana gap na ndio maana promotion mpaka wakati wa JK zilikuwa zimebase kwenye seniority sababu kwenye merit maafisa hawajapigana gap bali wako wote sawa tu by majority
 
Nina matumaini unajua fika kuwa jeshi letu material ya uafisa na maafisa wote wa mwanzo walifunzwa academy za kijeshi katika mataifa yaliyopo chini ya British Royal crown

Muingereza ambae tunafuata utamaduni wake na sheria zake yeye kupanda ngazi moja hadi nyingine kijeshi ni muda wa miaka mitatu na pia angalia na mataifa mengine makongwe huwezi kupanda kutoka brigedia hadi meja jenerali ndani ya miezi

Rais amepewa mamlaka makubwa mno kwa vifungu vya sheria zetu kwa mfano Rais amepewa mamlaka ya kupindua seniority ya ndani ya rank ambayo utamaduni wa kijeshi mkubwa ni yule alietangulia kuvaa cheo sasa rais amepewa mamlaka ya kujiamulia mfano alietangulia akamfanya ni mdogo yaani vice versa ya utamaduni wa kijeshi

Busara ni muhimu, sio kufanya baadhi ya vitu kwa sababu tu uko na power ukaacha lawama watu wananung'unika (majenerali waliosotea, makanali wanaosota lazima wanung'unike )

Majenerali wengi tu wazuri wanastaafu na wamestaafu katika ubrigedia anakuja rushwa mtu ndani ya miezi
Acha uongo/usiongee usichokijua
 
Wewe unachukulia kuwa Jeshi la Tanzania lifuate system ya Jeshi la uingereza one-to-one, hapana, hiyo siyo kweli. Maafisa wa jeshi la Uingereza hawafanyi kazi za serikali; wakati Tanzania kuna magenerals na makanali wanafanya kazi za serikali. Uingereza kila general ana Command ya kijeshi, Tanzania siyo kila general officer ana command, kuna general officers wengi hawana command yoyote. Tuna brigadier general wengi kuliko idadi ya brigade zilizopo.

Mwisho elewa kuwa General officer yeyote katika TPDF anapandishwa na Amiri jeshi mkuu kwa kushauriana na watu wawili tu: CDF na Chief of Staff. Hakuna guideline yoyote ya kupandishwa inayotaka mtu akae na cheo kimoja muda mrefu au awe amecommand unit yoyote ya kijeshi; in fact mtu anaweza kupandishwa kutoka Kanali kuwa Major General bila kuwa Brigadier general. Kuna Twalipo alipanda kutoka Luteni kanali (mkuu wa mkoa wa Ziwa Magharibi wakati huo) hadi na kuwa Lt General Mkuu wa Majeshi. Na Sarakikya naye alipanda kutoka Captain hadi kuwa Brigadier; ndiyo system yetu hiyo na wala uslalamike. In fact kuna mageneral officers wengi waliopanda kwa utaratubu huo ila ni kwa vile huyu anajulikana kuwa alipandishwa kuwa Brigadier general hadharani mwaka mmoja ulioopita( siyo miezi bali ni mwaka umepita), lakini ukichokonoa ndani ya jeshi utakuta wapo wengine wengi.
Kipindi cha Nyerere kulikuwa na upendeleo sana imewahi lalamikiwa kuna mtu aliwahi panda vyeo viwili ndani ya wiki moja

Na nchi ilikuwa changa kipindi hicho Muingereza katika jeshi lake la kikoloni la KAR na wakoloni wote kiujumla hawakutaka muafrika awe Afisa Jeshini , Waafrika cheo wamejitahidi ilikuwa ni Sajenti and so JK Nyerere angalau alikuwa na pakushikia

Nasikitika mkuu wangu unapoona kuwa kuskip ranks ni jambo la kawaida

Nilikuwa nasoma handout ya mkufunzi mmoja wa Sandhurst Jeshini vyeo sio kichwa tu uzoefu baada ya kutumikia unamatter kuliko ndio inakuja mantiki ya hata kuwepo hizo ranks
 
Usishangae maana inawezekana tu wengine mara ya mwisho kupandishwa vyeo ilikuwa mwaka 2008 sasa sijui unasemaje kwa hawa maana hadi leo hawajapandishwa vyeo
Hii hatari

Au hao wapo kwenye rank visiki mfano u'meja' ?
 
Kipindi cha Nyerere kulikuwa na upendeleo sana imewahi lalamikiwa kuna mtu aliwahi panda vyeo viwili ndani ya wiki moja

Na nchi ilikuwa changa kipindi hicho Muingereza katika jeshi lake la kikoloni la KAR na wakoloni wote kiujumla hawakutaka muafrika awe Afisa Jeshini , Waafrika cheo wamejitahidi ilikuwa ni Sajenti and so JK Nyerere angalau alikuwa na pakushikia

Nasikitika mkuu wangu unapoona kuwa kuskip ranks ni jambo la kawaida

Nilikuwa nasoma handout ya mkufunzi mmoja wa Sandhurst Jeshini vyeo sio kichwa tu uzoefu baada ya kutumikia unamatter kuliko ndio inakuja mantiki ya hata kuwepo hizo ranks

Kuhusu maoni yako kwenye upendeleo wakati wa Nyerere, sina ushahidi na wala sitaliongelea sana kwa vile hata wewe hujaleta ushahidi wowote wa kujadliliwa ila ninataka kuengelea vyeo vya mejenerali tu. Niliwahi kujibu mada fulani hapa takriban miaka kumi iliyopita mtu aliposema kuwa Nyerere aikuwa anateua wakuu wa majeshi kutoka Mara tu nikampa data kuwa wakati wa Nyerere kulikuwa na wakuu wa majeshi watatu tu: Sarakikya (mmeru), Twalipo(Mrufiji), na mwishoni sana mwa utawala wake ndipo alipomteua Musuguri wa kabila lake tena kwa kufuata seniority ya kijeshi, na ambaye alimtumikia chini ya miaka mitatu tu kabla hajastaafu.

Kuhusu vyeo vya majenerali, unapokosea ni kuwa jeshini kuna vyeo vya aina nne: Non-Comissioned Oficers, Junior Officers , Senior Officers, Superior au General Officers. Sasa unapofikia kuwa General Officer unakuwa umeshaaminika sana na wala huhitaji mafunzo wala uzoefu tena. Nenda tena kwenye mitaala ya Sandhurst na utakuta kuwa hakuna kozi yoyote ya General officer, bali ni kwa hao Junior na Senior officers tu, na hataTanzania kwa kiasi kikubwa kwa hao junion na senior officers ndio utaratibu unaofanyika. Hiyo mannual uliyosoma ni ya hao maofisa wa chini, siyo kwa ajili ya general officers. Kumbuka kuwa chuoni pale huenda kuna general officers wawili au watatu tu, mmoja akiwa mkuu wa chuo na wengine wakiwa kwa shughuli za administration, sasa sijui ni nani atakuwa anawafundisha general officers tena. Ukisha kuwa general officer wewe ni General tu; haijalishi una nyota ngapi.

Tufauti yetu na Uingereza ni kuwa kwa wao General Officer lazima awe na Command kwa hiyo hawawezi kumpandisha mtu kuwa genral officer wakati hakuna command ambayo ni vacant, na sisi General officer anaweza kufanya kazi yoyote hata kuwa mkuu wa mkoa au katibu mkuu wa wizara au Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU. Nashindwa kuelewa malalamiko yako yanatokana na msingi gani ilhali kila kitu kiko wazi kabisa. Je unaweza kuniambia kuwa hao mameja jenerali wote takribani 30 waliopo TPDF leo wote kweli walikaa miaka mitatu kabla ya kupandishwa tena. Hata huyu Chief of Staff aliyeko leo madarakani hakukaa miaka mitatu mitatu kwenye cheo kimoja kama unavyosisitiza, alipotoka kuwa kanali alipanda harakaharaka hadi kuwa Luteni jenerali na Chief of Staff. Angekaa hiyo miaka mitatu unayotaka huenda Lt Gen Mohammed angeanza kufikiriwa kwa cheo hicho mwaka jana tu.
 
Hakunaga rank kisiki ambacho hakiwezi pandishwa cheo, mkataba wa Serikali ni kila baada ya Miaka 3 watu wanapandishwa vyeo ila kwa masharti ya uwe na nidhamu, mchapa kazi na usiwe na mshtaka mashtaka. ukishtakiwa miaka unaongezwa ya ww kupandishwa cheo. sasa huku wameanza kupandishana kama ushabiki, kuingiza siasa ili wasichukiwe kwenye madaraka na kuwafanyia kitu mbaya...
Hii hatari

Au hao wapo kwenye rank visiki mfano u'meja' ?
 
Genaral huanzia hata kwenye u brigedia mzee,mana hata brigedia nae ni general na gari yake ina nyota 2 ,meja genaral ni general nae pia
Generals wako Wanne
Brigadier General(1 star general)
Major General (2 stars general)
Lieutenant General (3 stars general)
General (4 stars general)

Lieutenant General Chief of Staff (CoS)
General Chief of Defense Forces (CDF)

Mara nyingi kuanzia rank ya Brigadier General mtu anaweza kurushwa rank yoyote kama itakavyompendeza Commander in Chief (CiC) ivo hao kina Major General Mbuge kuwa promoted ivo sioni shida as Team ya mkuu imejirizisha vya kutosha japo kwenye Millitary shortcut ni mbaya sana Tumetoa reference juu kuhusu Jeshi la Nigeria kusumbulia na Pirates na Vikundi vya kigaidi ambavyo unakuta viko well trained and very strategic kuzidi hata Top decision maker wa Jeshi lao kwahiyo experience within the battle field ina matter sana
 
Hii point siyo kweli sana kma unavyoamini kuwa lazima ukae na cheo fulani cha ujeneral kwa miaka mitatu ndipo upande, in fact wao mambo ni kinyume kabisa kuwa lazima upande ndani ya hiyo miaka mitatu ama sivyo utatakiwa kustaafu. Yaani iwapo utakuwa Brigedia General (1-star), ikipiata miaka mitatu kabla hujapanda tena kuwa Major General (2-star) basi unastaafu jeshi; vile vuile ukiwa Major General (2-star)ikapita miaka mitatu hujapanda kuwa Luteni General (3-star)basi na wewe unastaafu utumishi wa jeshi; ni vivyo hivyo ukiwa Luteni General (3-star) ikapipita miaka mitatu kabla hujapanda kuwa General (4-star), pia unastaafu. Utaratibu huu unatokana na kuwa kwenye kupanda kutoka 2d LT mpaka Colonel ni lazima uwe umeshatumikia jeshi kwa zaidi ya miaka 22 ikiwa ulikuwa unapata promotions za haraka haraka kila baada ya miaka mitatu au minne. Lakini kwe vile unaweza kuwaa visiki hapo jini, inawezekana kuwa utakuwa umetumikia jeshi kwa miaka 25; ambapo kwa kawaida utakuwa na umri kama miaka 47 au 48 hivi. kwa vile Umri wa kustaafu ni miaka 62; na hawataki mtu anafikia miaka hiyo 62 bado akiwa hajawa 4-star General nasi ndiyo maana wana utaratibu huo. In fact limit ya kukaa cheo kimoja ni mpaka miaka mitano, ila ukishapitisha miaka mitatu bila kupanda, basi unaaza kujiandaa kustaafu.

Mifano yake ipo mingi sana kwenye jeshi la marekani: Lt Gen Ricardo Sanchez aliyekuwa anaongoza vita Iraq, baada ya skendo ya Abu Ghraib alishindwa kupanda kuwa 4-star General na hivyo kustaafu baada ya miaka mitatu tangu awe Lt. Gen. Halafu Maj. Gen Antonio Taguba aliyetoa taarifa ya jeshi kutesa wafungwa huko Abu Ghraib na Guantanamo, hakupandisha cheo kuwa Lt Gen na baada ya miaka mitatu naye aalistaafu. Vile vile General Michael Flyinn, alikuwa Lt General, lakini alipovurga kwenye handling ya Classified information hakupandishwa kuwa 4-start General na baada ya miaka mitatu naye akastaafu. List ipo ndefu sana ila hao ni wale maarufu wanaojulikana.
Umeeleweka mkuu asante kwa ufafanuz uliotukuka

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Generals wako Wanne
Brigadier General(1 star general)
Major General (2 stars general)
Lieutenant General (3 stars general)
General (4 stars general)

Lieutenant General Chief of Staff (CoS)
General Chief of Defense Forces (CDF)

Mara nyingi kuanzia rank ya Brigadier General mtu anaweza kurushwa rank yoyote kama itakavyompendeza Commander in Chief (CiC) ivo hao kina Major General Mbuge kuwa promoted ivo sioni shida as Team ya mkuu imejirizisha vya kutosha japo kwenye Millitary shortcut ni mbaya sana Tumetoa reference juu kuhusu Jeshi la Nigeria kusumbulia na Pirates na Vikundi vya kigaidi ambavyo unakuta viko well trained and very strategic kuzidi hata Top decision maker wa Jeshi lao kwahiyo experience within the battle field ina matter sana
Sentensi yako ya kwanza ni sahihi kabisa ingawa unaimalizia vibaya kwa kutumia neno Military shortcut ambayo siyo hivyo; ni promosheni ya kawaida kulingana na majukumu mapya ambayo amepangiwa na amiri jeshi mkuu kwa mujibu wa katiba. Unajua hii kesi ya Mbuge watu wanaipigia kelele kwa sababu alipandishwa kuwa Brigadier General kwa mwembwe sana, lakini isingekuwa mwebwe zile huenda watu wasingekuwa wanapiga kelele hizi. Promotion za namna hiyo za kuwa Brigadier General na baada ya muda kidogo kuwa Major General hufanyika sana hasa kunapokuwa na Major Generals wanaokaribia kusataafu, na watu wanaoweza kurithi majukumu yao bado wana vyeo vya ukanali. Hata huyu CDF alipanda kuwa Lt Gen kwa mwaka mmoja tu akapandishwa tena kuwa Full General.

Kuhusu reference ya Nigeria, ni vizuri ukumbuke kuwa General Yakub Gowon aliruka toka Lt Col hadi Full General (4-star). Halafu mtu kuwa General Officer siyo lazima awe ni kwa ajili ya battlefield command tu; kuna general officers ambao ni administrators tu na kuna general officers ambo ni madaktari, wahandisi na shughuli kama hizo ambazo hazina uhusiano na kwenda kwenda vitani directly. Muundo wa jeshi unaruhusu kabisa kuwepo kwa wapiganaji na wasiokuwa wapiganaji, kuna kombania za kivita na kombania ambazo siyo za kivita; major anayeongoza kombania ya kivita anatakiwa nawe na ujuzi wa kuongoza mapamabano vitani, lakini major anayongoza HQ COY halazimiki kujua kuongoza vita. Ni vivyo hivyo hata kwa General Officers.
 
Ninavyofahamu rank jeshini ni stahili ya mtu na sio favour

Anyway siku hizi naona hapa nchini tunaenda na mdundo tu maana chochote kitakachofanywa na jiwe watu wanasema ni sahihi
sasa kama cheo ni stahiki ya mtu unadhani kuna watu wangapi wana sifa ya kuwa ma lut gen???

mkuu jeshi sio taasisi za katibu mkuu hizo kwamb ni lazima upande cheo,jeshi ni nidhamu wakati wote ndipo utapanda tofuti na wengine.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom