Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,737
- 76,365
Mnaongelea mifumo tofauti hapo, tanzania ipo wazi katika miaka ya kustaafu na ndio maana hata mtu akipanda cheo mapema sawa ila inapokuja umri wa kustaafu anaondoka. Sasa sijui nyie mnaongelea kupanda cheo badala ya miaka ya kustaafu?!Hii point siyo kweli sana kma unavyoamini kuwa lazima ukae na cheo fulani cha ujeneral kwa miaka mitatu ndipo upande, in fact wao mambo ni kinyume kabisa kuwa lazima upande ndani ya hiyo miaka mitatu ama sivyo utatakiwa kustaafu. Yaani iwapo utakuwa Brigedia General (1-star), ikipiata miaka mitatu kabla hujapanda tena kuwa Major General (2-star) basi unastaafu jeshi; vile vuile ukiwa Major General (2-star)ikapita miaka mitatu hujapanda kuwa Luteni General (3-star)basi na wewe unastaafu utumishi wa jeshi; ni vivyo hivyo ukiwa Luteni General (3-star) ikapipita miaka mitatu kabla hujapanda kuwa General (4-star), pia unastaafu. Utaratibu huu unatokana na kuwa kwenye kupanda kutoka 2d LT mpaka Colonel ni lazima uwe umeshatumikia jeshi kwa zaidi ya miaka 22 ikiwa ulikuwa unapata promotions za haraka haraka kila baada ya miaka mitatu au minne. Lakini kwe vile unaweza kuwaa visiki hapo jini, inawezekana kuwa utakuwa umetumikia jeshi kwa miaka 25; ambapo kwa kawaida utakuwa na umri kama miaka 47 au 48 hivi. kwa vile Umri wa kustaafu ni miaka 62; na hawataki mtu anafikia miaka hiyo 62 bado akiwa hajawa 4-star General nasi ndiyo maana wana utaratibu huo. In fact limit ya kukaa cheo kimoja ni mpaka miaka mitano, ila ukishapitisha miaka mitatu bila kupanda, basi unaaza kujiandaa kustaafu.
Mifano yake ipo mingi sana kwenye jeshi la marekani: Lt Gen Ricardo Sanchez aliyekuwa anaongoza vita Iraq, baada ya skendo ya Abu Ghraib alishindwa kupanda kuwa 4-star General na hivyo kustaafu baada ya miaka mitatu tangu awe Lt. Gen. Halafu Maj. Gen Antonio Taguba aliyetoa taarifa ya jeshi kutesa wafungwa huko Abu Ghraib na Guantanamo, hakupandisha cheo kuwa Lt Gen na baada ya miaka mitatu naye aalistaafu. Vile vile General Michael Flyinn, alikuwa Lt General, lakini alipovurga kwenye handling ya Classified information hakupandishwa kuwa 4-start General na baada ya miaka mitatu naye akastaafu. List ipo ndefu sana ila hao ni wale maarufu wanaojulikana.
MASAMILA
ᵃʳᵉᵉᵐ 
