Watanzania tulianza kupigania haki tangu enzi za mababu zetu akina Mkwawa, Isike, Chabruma, Mirambo, n.k. Wakati huo hakukuwa na mikataba ya kuheshimu haki ya kimataifa, hakukuwa na simu, hakukuwa na radio, internet wala TV lakini watu walijua wanatakiwa kuwa huru, hata kama uhuru huo haukuwa kwa tafsiri ya leo, lakini walijua kuwa walistahili uhuru na haki.
Akaja Mwalimu na wenzake, Mwinyi, Mkapa, na kisha Kikwete. Wakati wote huo tumeendelea kujenga Taifa ambalo tunataka liwe na huru kamili, demokrasia kamili, haki kamili, n.k. Hatujafika huko lakini tumekuwa tunapiga hatua. Kinashangaza sasa hivi badala ya kuzidi kupiga hatua kwenda mbele, tayari tunarudi nyuma.
Binadamu ni mtu huru ndiyo maana Mungu kamwumba kila mmoja na kichwa chake chenye ubongo unaojitegemea. Mtu yeyote anayetaka watu wote watumie ubongo wake kwa kila kitu, hawezi kufanikiwa, badala yake atasababisha matatizo makubwa.