BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Prof. Anna Tibaijuka amesema wakati akiwa Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hakutoa Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi katika eneo hilo lakini ulifanyika kwa maamuzi yasiyo sahihi
Tibaijuka amesema "Jangwani haina kibali changu kuwa pale. Mimi nilikataa lakini sikuwa na madaraka kuzuia na hivyo pakajengwa, nilikataa kabisa Serikali yote inajua. Nilisema mimi kama mtaalamu wa Mipango Miji hamuwezi kuweka Kituo cha Mabasi kwenye eneo la Bwawa. Pale panajulikana ni Bwawa patafurika"
Ameongeza kuwa suala Upangaji Miji ni uamuzi wa Rais si Utaalamu, ujenzi wa eneo la Jangwani ulikuwa na mvutano kwasababu hakukuwa na Utashi wa Kisiasa (Political Will) ambapo kama pangetolewa uamuzi wa juu pasingejengwa Kituo cha Mabasi.