Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 446
- 1,140
Kuna Stendi ya mwendokasi pale (Jangwani), mwendokasi ile imejengwa kwenye mkondo wa maji halafu maji yakijaa pale wanaanza kulia kwamba maji yameingia kwenye magari sio kweli bali magari yameingia kwenye maji na wale wote waliotengeneza ile Stendi akili hawakuwa nazo na nitashangaa kama bado wanapumua mpaka sasa, kwa sababu hawakuangalia mabadiliko ya tabia nchi, wameleta hasara magari yale, maji yameingia kwenye yale magari lakini ukweli usiopingika ni kwamba magari ndio yaliyofuata maji, kwa hiyo ninapozungumzia watu waliofuata maji ni pamoja na vituo vya mwendokasi baadhi hufuata maji sasa kama kuna hasara wale watapaswa wapelekwe Mahakamani kwa sababu wamesababisha magari kuharibika pasipo sababu" -Chalamila
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo Februari 19.2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Temeke
Pia soma
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo Februari 19.2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Temeke
Pia soma
- Prof. Tibaijuka: Mimi nilikataa Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi kujengwa Jangwani, Sikuwa na Madaraka ya Kuzuia
- Kwanini Rais anashindwa kuwachukulia hatua waliojenga stendi ya mwendokasi Jangwani?
- Hivi ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi jangwani ulifanyiwa "environmental impact assesment(e.i.a)"?