UDART Jangwani ni mradi wa Mtu, kelele za chura hazizui Tembo kunywa maji!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411

DART.jpeg

Eneo la Jangwani ilipo Karakana ya Mwendokasi imekuwa ikipigiwa kelele muda mrefu na wadau wa mazingira kuwa ujenzi wake haukuzingiatia tathmini iliyofanywa na NEMC wala haukuzingatia sheria za mazingira.

Baadhi ya sheria zinazotajwa kukiukwa katika ujenzi wa karakana hiyo ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 kifungu cha Kifungu cha 57 (1). Kifungu hicho kinakataza shughuli za binadamu katika maeneo oevu.

“Kwa kuzingatia kifungu cha (2), ndani ya mita 60 hakutafanyika shughuli yoyote ya binadamu ya kudumu au ambayo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi wa mazingira au utunzaji wa bahari au kingo za mto, bwawa, au miambao ya asili ya ziwa,” ameeleza sheria hiyo.

Hata hivyo kifungu cha (2) kinampa mamlaka waziri anayehusika na mazingira kuweka miongozo ya kuendesha shughuli za binadamu ndani ya maeneo yaliyoelezwa kwa mujibu wa kifungu cha 1.

Pia uwepo wa karakana hiyo unakinzana na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya 2007, kifungu cha 25 na Sheria ya Ardhi Na.5 ya 1999 kifungu cha 7 (a-d), ambazo zinataka maeneo oevu yalindwe.

NEMC: Kituo cha mabasi ya mwendokasi Jangwani kina kibali cha Mazingira hakitahusishwa kwenye bomoabomoa.
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mabondeni kuhoji uhalali wa kituo cha mabasi ya mwendokasi (DART) katika eneo la Jangwani huku wananchi wakihamishwa eneo hilo, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeeleza kuwa mradi huo umepata kibali cha Mazingira.

"Kuna Stendi ya mwendokasi pale (Jangwani), mwendokasi ile imejengwa kwenye mkondo wa maji halafu maji yakijaa pale wanaanza kulia kwamba maji yameingia kwenye magari sio kweli bali magari yameingia kwenye maji na wale wote waliotengeneza ile Stendi akili hawakuwa nazo na nitashangaa kama bado wanapumua mpaka sasa, kwa sababu hawakuangalia mabadiliko ya tabia nchi, wameleta hasara magari yale, maji yameingia kwenye yale magari lakini ukweli usiopingika ni kwamba magari ndio yaliyofuata maji, kwa hiyo ninapozungumzia watu waliofuata maji ni pamoja na vituo vya mwendokasi baadhi hufuata maji sasa kama kuna hasara wale watapaswa wapelekwe Mahakamani kwa sababu wamesababisha magari kuharibika pasipo sababu" -Chalamila

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo Februari 19.2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Temeke.

Karakana utafikiri zizi la ng'ombe
Kweli tukisema kuna binadamu wana akili na wengine matope wala tusijilaumu
Wana vyeti na wanaitwa ma -engineer na walipo hojiwa walisema maji yanakuja mara moja kwa miaka 5.

Lakini yote tisa kumi, Yanga pale kwenye chakula walichoalikwa Ikulu wanamwambia Rais Samia wanataka kujenga uwanja hapo kwenye Ziwa JANGWANI. [eng Hersi ]

#Tatizo Vyuo vyetu.
#Ni zaidi ya matope.
 
Wana vyeti na wanaitwa ma -engineer na walipo hojiwa walisema maji yanakuja mara moja kwa miaka 5.

Lakini yote tisa kumi, Yanga pale kwenye chakula Ikulu wanamwambia Rais Samia wanataka kujenga uwanja hapo kwenye Ziwa JANGWANI.

#Ni zaidi ya matope.
Kuna nchi zingine utasema hakuna binadamu aisee
Sijui hata niseme nini hapa
Sasa hiyo miaka 4 kabla ya maji wamejiandaa vipi
Kweli matope 😄
 
Waende Nchi za Ulaya na Asia wakaone Jinsi Mito inavyodhibitiwa kwa kuchimbwa kina na kingo kuongezwa.

Kuudhibiti Mto Msimbazi sio kazi kubwa.

Mto kama Danube unaopititia Miji mingi umedhibitiwa wakati sisi huu Mto mdogo unatutoa kamasi.
 
View attachment 2910045

Eneo la Jangwani ilipo Karakana ya Mwendokasi imekuwa ikipigiwa kelele muda mrefu na wadau wa mazingira kuwa ujenzi wake haukuzingiatia tathmini iliyofanywa na NEMC wala haukuzingatia sheria za mazingira.

Baadhi ya sheria zinazotajwa kukiukwa katika ujenzi wa karakana hiyo ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 kifungu cha Kifungu cha 57 (1). Kifungu hicho kinakataza shughuli za binadamu katika maeneo oevu.

“Kwa kuzingatia kifungu cha (2), ndani ya mita 60 hakutafanyika shughuli yoyote ya binadamu ya kudumu au ambayo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi wa mazingira au utunzaji wa bahari au kingo za mto, bwawa, au miambao ya asili ya ziwa,” ameeleza sheria hiyo.

Hata hivyo kifungu cha (2) kinampa mamlaka waziri anayehusika na mazingira kuweka miongozo ya kuendesha shughuli za binadamu ndani ya maeneo yaliyoelezwa kwa mujibu wa kifungu cha 1.

Pia uwepo wa karakana hiyo unakinzana na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya 2007, kifungu cha 25 na Sheria ya Ardhi Na.5 ya 1999 kifungu cha 7 (a-d), ambazo zinataka maeneo oevu yalindwe.

NEMC: Kituo cha mabasi ya mwendokasi Jangwani kina kibali cha Mazingira hakitahusishwa kwenye bomoabomoa.
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mabondeni kuhoji uhalali wa kituo cha mabasi ya mwendokasi (DART) katika eneo la Jangwani huku wananchi wakihamishwa eneo hilo, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeeleza kuwa mradi huo umepata kibali cha Mazingira.

"Kuna Stendi ya mwendokasi pale (Jangwani), mwendokasi ile imejengwa kwenye mkondo wa maji halafu maji yakijaa pale wanaanza kulia kwamba maji yameingia kwenye magari sio kweli bali magari yameingia kwenye maji na wale wote waliotengeneza ile Stendi akili hawakuwa nazo na nitashangaa kama bado wanapumua mpaka sasa, kwa sababu hawakuangalia mabadiliko ya tabia nchi, wameleta hasara magari yale, maji yameingia kwenye yale magari lakini ukweli usiopingika ni kwamba magari ndio yaliyofuata maji, kwa hiyo ninapozungumzia watu waliofuata maji ni pamoja na vituo vya mwendokasi baadhi hufuata maji sasa kama kuna hasara wale watapaswa wapelekwe Mahakamani kwa sababu wamesababisha magari kuharibika pasipo sababu" -Chalamila

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo Februari 19.2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Temeke.

NEMC: Kituo cha mabasi ya mwendokasi Jangwani kina kibali cha Mazingira hakitahusishwa kwenye bomoabomoa.

Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mabondeni kuhoji uhalali wa kituo cha mabasi ya mwendokasi (DART) katika eneo la Jangwani huku wananchi wakihamishwa eneo hilo, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeeleza kuwa mradi huo umepata kibali cha Mazingira.
Niliwahi kumuonya mkuu DART siku nilibahatika kuonana naye wakati ujenzi unaendelea akabisha kwanba sio tatizo. Huenda msukumo ulikua kwa mkandarasi.. Kwake mradi amepata kandarasi washibe wao, mazingira watajuana wenyewe.
 
Niliwahi kumuonya mkuu DART siku nilibahatika kuonana naye wakati ujenzi unaendelea akabisha kwanba sio tstizo. Huenda msukumo ulikua kwa mkandarasi.. Kwake mradi amepata kandarasi washibe wao, mazingira watajuana wenyewe.
"Haambiliki" ndio alikuwa Waziri, huwezi kumbishia. NEMC waliona hilo na walijua, wangegoma kutoa vibali "mzee haambiliki" angefukuza wote.
 
Back
Top Bottom