Huyu Prof Pius Yanda ameshinda zawadi ya Nobel. Ni zawadi kubwa hii duniani, na yeyote anayeipata huwa anapongezwa na kupokelewa kwa shangwe nchini kwake. Waafrika waliowahi kushinda zawadi hii ni pamoja na Askofu Desmond Tutu, Mzee Nelson Mandela, Prof Wangari Maathai wa Kenya, Prof Wole Soyinka wa Nigeria ambao wote walipongezwa sana na nchi zao kwa kupata kukubalika kiulimwengu. Lakini nashangaa sisi wabongo, huyu Prof wetu kashinda zawadi ya maana sana, kafanya kazi kubwa mno kitaaluma, lakini sisi huku tunangangania kuandika habari za Miss Tanzania, Big Brother nk! Nini kimetupata hata tukashindwa kuiona hii? Ni umbumbumbu wa waandishi wetu au ni pepo gani katukamata? Yaani mambo ya msingi hatuyaoni, siye tunangangania tu kutangaza uzinzi na upuuzi? Hivi ni elimu ndogo au ni nini? Zawadi ya Nobel, and nobody raises an eyebrow? This is ridiculous! Au ni hii tabia ya kupenda tu udaku, watu wanasubiri tu kusikia nani kafumaniwa nk? Sioni hata gazeti moja likiandika habari hii, sijasikia akipongezwa wala chochote? A Nobel laureate! It must be a terrible joke! Imagine hii zawadi kapewa pamoja na Al Gore, ambaye huko Marekani sasa wanampongeza na kuukubali mchango wake. Huyu wa kwetu karudi kimyakimya kama vile kaenda tu kutembea kivyake! Jamani, are we serious? Mbona sie ndo tunaojitapa na msemo "Mcheza kwao hutuzwa"? Huyu wa kwetu mbona tumemuacha tu kama vile hakuna alilolifanya? Ama waandishi wetu ni mambumbumbu hawaelewi hata uzito wa jambo kama hili? Na hata serikali haina habari, haielewi hata Nobel Peace Prize maana yake ni nini? Yaani inauma sana! Ama kweli "usiwatupie nguruwe lulu zako, wasije wakazitupa chini, wakakugeukia na kukurarua" (Mathayo 7:6).