Prof Pius Yanda ashinda zawadi ya Nobel

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
208
Huyu Prof Pius Yanda ameshinda zawadi ya Nobel. Ni zawadi kubwa hii duniani, na yeyote anayeipata huwa anapongezwa na kupokelewa kwa shangwe nchini kwake. Waafrika waliowahi kushinda zawadi hii ni pamoja na Askofu Desmond Tutu, Mzee Nelson Mandela, Prof Wangari Maathai wa Kenya, Prof Wole Soyinka wa Nigeria ambao wote walipongezwa sana na nchi zao kwa kupata kukubalika kiulimwengu. Lakini nashangaa sisi wabongo, huyu Prof wetu kashinda zawadi ya maana sana, kafanya kazi kubwa mno kitaaluma, lakini sisi huku tunangangania kuandika habari za Miss Tanzania, Big Brother nk! Nini kimetupata hata tukashindwa kuiona hii? Ni umbumbumbu wa waandishi wetu au ni pepo gani katukamata? Yaani mambo ya msingi hatuyaoni, siye tunangangania tu kutangaza uzinzi na upuuzi? Hivi ni elimu ndogo au ni nini? Zawadi ya Nobel, and nobody raises an eyebrow? This is ridiculous! Au ni hii tabia ya kupenda tu udaku, watu wanasubiri tu kusikia nani kafumaniwa nk? Sioni hata gazeti moja likiandika habari hii, sijasikia akipongezwa wala chochote? A Nobel laureate! It must be a terrible joke! Imagine hii zawadi kapewa pamoja na Al Gore, ambaye huko Marekani sasa wanampongeza na kuukubali mchango wake. Huyu wa kwetu karudi kimyakimya kama vile kaenda tu kutembea kivyake! Jamani, are we serious? Mbona sie ndo tunaojitapa na msemo "Mcheza kwao hutuzwa"? Huyu wa kwetu mbona tumemuacha tu kama vile hakuna alilolifanya? Ama waandishi wetu ni mambumbumbu hawaelewi hata uzito wa jambo kama hili? Na hata serikali haina habari, haielewi hata Nobel Peace Prize maana yake ni nini? Yaani inauma sana! Ama kweli "usiwatupie nguruwe lulu zako, wasije wakazitupa chini, wakakugeukia na kukurarua" (Mathayo 7:6).
 
  • Thanks
Reactions: ffn
...OK lakini ni vigumu kujua kwa sababu hatukusikia kama ameshinda,ni kweli alikuwemo katika ile timu ya umoja wa mataifa ilifonya kazi na wakashinda pamoja na Gore lakini humo kwenye timu kuna watu maelfu ujue ni Department kubwa sana hiyo ya UN,kwa hiyo ni vigumu kusema ameshinda ingawaje amefanyia kazi dept iliyoshinda....ni ngumu sana mjomba kumpa sifa sawa na Gore!
 
Mkuu hiii ni habari njema sana kweli mm mwenyewe hata sijaisikia. Nimekuwa nahudhuria seminar nyingi zinazoongozwa na Nobel prize winers hasa kwenye Development Economics kama Pro Yunis, Jeff Sachs etc ni watu wanaotukuka sana. Mama Mangare Wathai naye ukitembea sehemu kama Tokyo na Malysia unakuta mabango yenye picha zake na ujumbe wake wa mazingira. Hii ni zawadi kubwa sana sana siwezi kuelezea ila huwezi amini mimi imesoma hapa kwenye post yako wala sijawahi kusikia kama kuna Mtz nae katunukiwa hiyo zawadi ambayo watu wengi maarufu duniani huwa wanaota kuwa ipo siku watatunukiwa. Kwani huyo Prof yeye ni wa nini na kafanya nini? hebu tupe habari Kithuku.

Unajua bwana kama ni kweli basi Tz inachekesha sana Richard kashinda uzinzi hadi CCM wametoa pongezi zao na watu wameandamana kumpongeza, dada zetu wakionyesha vichupi basi ni shangwe kila mahala, siku Kithuku anarudi na PHD yake ili awe Waziri mkuu na Lowasa kupelekwa ubalozini Sudani hakuna watakaompokea aipot.
 
Mimi bado sijaamini namna hii event ilivyokuwa handled.Of course siku ile ya UD graduation,utawala wa chuo walilisema hili.Lakini cha ajabu ni kwamba the following day front page za magazeti yanasomwa zaidi waliweka event ya Hosea kutunukiwa PhD kama habari nzito and then issue ya Prof Yanda ikachomekwa kwenye para fulani ndani ya story ya Hosea.
Sijui kama hata aliapppear kwenye TV yoyote hapo bongo..sina uhakika.Lakini ukweli ni kwamba tunapanda mbegu mbaya kwa vizazi vijavyo kama mambo kama haya hatuyapi priority.Dunia imefikia maendeleo tunayoshuhudia leo kwa kuyapa uzito mkubwa masuala ya kitafiti.Tuna wabongo wengi tu wanaofanya vitu vyao (wonders) lakini wanaishia kimya kimya tu. Nadhani mindset yetu imeharibiwa na sasa inaelekea kuwa sumu mbaya katika mustakabali ya maendeleo yetu na dunia kwa ujumla.
 
Wakuu,
Kwenye ile kamati iliyo-share nobel peace prize na Al Gore kuna watanzania wengine watatu (jumla wanne pamoja na Prof Yanda). Wengine ni Dr. Willy Makundi wa UC Berkerly,Marekani, Prof. Mwandosya na Prof. Katima.
 
Nadhani ni vyema tukitofautisha, individual au duo wakishinda Nobel prize eg. Gore, Wole Soyinka, Wangari Maathai n.k. Akina prof Yanda wameshinda kama group, na hivyo hawawezi kutajwa mmoja mmoja. Tunachoweza kufanya ni kufurahi na kujivunia kwamba they were part of the team, but this was a team effort na tusim-single out one person only!
Hata hivyo I agree, the media haijatoa coverage nzuri, lkini ni kutokana na kwamba hata their win is collective and not publicized as individual by the Nobel committee.
Hongereni watafiti wa Bongo, don't give up!
 
Kwa bahati mbaya huyu Profesa hajashinda hiyo Nobel Prize. Walioshinda ni Gore na hiyo panel ya IIPC. Yeye kuwa alihusika katika kutayarisha ripoti ya panel hiyo hakumaanishi kuwa naye alishinda. Ni kama Kofi Annan aliposhinda pamoja na Umoja wa Mataifa miaka michache iliyopita. Mbona hatukuitafsiri kuwa watanzania lukuki waliokuwa wanafanyakazi U.M wakati ule kuwa nao walishinda.Nasikitika kusema hili lakini tukiendelea ku'trumpet' ushindi huu kwa namna hii tutamtia aibu huyo Profesa na sisi wenyewe kama jamii kuwa ni watu wa kupenda mijisifa ya dezo. Sidhani kama Profesa anaweza akasimama kwenye kadamnasi ya maprofesa wenzie akadai kuwa ati naye ni mshindi wa Nobel Peace Prize. Au kuweka kwenye CV yake kuwa aliwahi kuwa mshindi wa Nobel Peace Prize. Lakini hili suala si tuliisha lijadili?
 
Fundi Mchundo,
Hiyo report iliandikwa na kamati za watu mbalimbali. Kila aliyeshiriki kuandika hiyo report ana haki ya kusifiwa na pia hata kuweka kwenye CV yake. Hii ni tofauti na nobel prize ya UN. Hawa wataandika kwenye CV kwamba walishirika kuandaa report ambayo ilishinda noble prize.

Hii ni kamati ya watu wachache wasomi ambao walikaa chini na kutoa mchango kwenye hiyo report.

Ni sawa na Yanga wakishinda kombe, useme wachezaji hawana haki ya kujisifia na huo ushindi na hata kuweka kwenye CV zao. Wanachama sawa, wanaweza kushangilia lakini hawawezi kuweka kwenye CV. Wachezaji ni tofauti.

Kwa TZ hatuna mafanikio makubwa kwenye nyanja za sayansi, inabidi tuwaunge mkono hawa watanzania wenzetu ambao angalau wamejitihadi. Hakuna cha kuona aibu hapa, wamefanya kile ambacho wengi wetu tumeshindwa kufanya.

Hongera maprofesa na madaktari wetu.
 
Kwa bahati mbaya huyu Profesa hajashinda hiyo Nobel Prize. Walioshinda ni Gore na hiyo panel ya IIPC. Yeye kuwa alihusika katika kutayarisha ripoti ya panel hiyo hakumaanishi kuwa naye alishinda. Ni kama Kofi Annan aliposhinda pamoja na Umoja wa Mataifa miaka michache iliyopita. Mbona hatukuitafsiri kuwa watanzania lukuki waliokuwa wanafanyakazi U.M wakati ule kuwa nao walishinda.Nasikitika kusema hili lakini tukiendelea ku'trumpet' ushindi huu kwa namna hii tutamtia aibu huyo Profesa na sisi wenyewe kama jamii kuwa ni watu wa kupenda mijisifa ya dezo. Sidhani kama Profesa anaweza akasimama kwenye kadamnasi ya maprofesa wenzie akadai kuwa ati naye ni mshindi wa Nobel Peace Prize. Au kuweka kwenye CV yake kuwa aliwahi kuwa mshindi wa Nobel Peace Prize. Lakini hili suala si tuliisha lijadili?

FM
nadhani umekurupuka tu.Labda ufafanue hapo nilipo-highlight red.
Navyoelewa nafasi ya Gore ilikuwa kuzunguka duniani kupigia debe walichoandaa hawa "vichwa".

You better withdraw the statement because is not true and therefore misleading!

Nadhani hawa maprof watakuwa wanasoma JF, wanaweza kufafanua zaidi walichofanya kwenye hiyo project.
 
wabongo bwana! kuna siku nilitoa hotuba kwenye sherehe baada ya mlo. nilipomaliza, nikakumbushwa nimesahau kuwataja wapishi. mmhhh!
 
FM
nadhani umekurupuka tu.Labda ufafanue hapo nilipo-highlight red.
Navyoelewa nafasi ya Gore ilikuwa kuzunguka duniani kupigia debe walichoandaa hawa "vichwa".

You better withdraw the statement because is not true and therefore misleading!

Nadhani hawa maprof watakuwa wanasoma JF, wanaweza kufafanua zaidi walichofanya kwenye hiyo project.

Mkuu, sijakurupuka! Hebu soma hapo chini,

During its announcement, the Nobel committee cited the winners "for their efforts to build up and disseminate greater knowledge about man-made climate change, and to lay the foundations for the measures that are needed to counteract such change."

The award ceremony will be held December 10 in Oslo, Norway.

"Through the scientific reports it has issued over the past two decades, the IPCC has created an ever-broader informed consensus about the connection between human activities and global warming," Ole Danbolt Mjoes, chairman of the Nobel committee, said in making the announcement.

Utaona kuwa the Intergovernmental Panel On Climate Change (IIPC) imepewa kutokana na kazi zao na ripoti walizozitoa kwa zaidi ya miaka ishirini kuelimisha dunia kuhusu athari za climate change. sasa, ndugu zangu, mnataka kuniambia kuwa Profesa alihusika kuandika ripoti zote hizo? Zawadi ni kwa Panel(ambayo imeundwa na serikali tofauti) na si kwa watu binafsi ambao kwa njia moja au nyingine wamewahi kuhusika na Panel hiyo!
 
CV ya Profesa hii hapa:
[media]http://ncsp.va-network.org/UserFiles/File/PDFs/CVs/YANDA_Pius.pdf[/media]

Utaona anastahili kupongezwa tena sana kwa achievements zake bila ya hii tunayotaka kumvisha. Kama anasoma naamini kabisa yeye mwenyewe atajisikia vibaya kuona kuwa tunamtangaza kuwa mshindi wa Nobel Peace Prize!
 
Fundi Mchundo,

Nafikiria hapa uko upande wa pili wa hizi two extreme views kuhusu prof. Moja ni kwamba kashinda Nobel prize na nyingine kwamba hajashinda wala hata hastahili kuweka kwenye CV yake.

Ukweli uko katikakti, prof. ni mmoja wa panel la wasomi wazuri wa dunia walioandika hiyo report. Kwa maana hiyo inatakiwa apongezwe kwa kazi kubwa waliyofanya mpaka kuifanya IIPC washinde hiyo zawadi.

Ni mantiki hiyo ilitakiwa prof. na Watanzania wengine walioshiriki kuandaa hiyo report wapongezwe na serikali pamoja na sisi wananchi kama tunavyowapongeza hapa JF. Pia ilitakiwa vyombo vya habari hata viwahoji na kujifunza zaidi athari za global warming.

Prof. inatakiwa ajisikie wala hakuna haja ya kuweka kichwa chini, inatakiwa hata kwenye CV yake aweke bila wasiwasi kama mjumbe kwenye panel iliyoshinda nobel prize.
 
jeee hao wenzake wamepongezwa na nchi zao?????????
 
jeee hao wenzake wamepongezwa na nchi zao?????????

Mtu wa Pwani,

Usilinganishe mataifa makubwa na Tanzania. Mataifa makubwa hata ukishinda nobel prize, serikali hawakupongezi moja kwa moja. Sana sana unapongezwa na vyombo vya habari na makundi mengine.

Niliangaliwa wakati hiyo peace nobel price inatangazwa, baadhi ya waliohusika walikuwa wanahojiwa na kupongezwa na vyombo vya habari.

Kwa Tanzania ambao sana sana labda hawa ndio wakali wetu wachache lazima tupige debe zaidi ili iwe changamoto kwa vijana na watoto wetu.
 
FM

Nadhani hawa maprof watakuwa wanasoma JF, wanaweza kufafanua zaidi walichofanya kwenye hiyo project.

6toeosw.gif
 
Waliotunukiwa zawadi ya Nobel Peace Prize ya mwaka 2007 ni Al Gore na IPCC. IPCC ilitunikiwa kwa kazi ilizozifanya tangu ilipoanzishwa mwaka 1988. IPCC imekuwa likitoa ripoti kuhusu climate change uhai wake wote. Profesa Pius Yanda ni mmoja ( wako wengi sana) wa contributors katika Working Group II ( ziko WG tatu) Fourth Assessment report. Humo katika WG kuna reviewers wengi tuu ambao nao wanachangia katika hii ripoti. Unaweza kuona majina yao hapa:
http://www.ipcc.ch/pdf/assessment-report/ar4/wg2/ar4-wg2-app.pdf
Mkuu wa IPCC ni Bw. Rajendra Cheuri kutoka India ambaye ni kiongozi wa tatu kuongoza Panel hii. Wote hawa kwa namna moja au nyingine wamechangia katika mafanikio ya IPCC lakini hatuwezi kuwaita 'joint recipients' wa Nobel Peace Prize.
Profesa Yanda anastahili kuheshimiwa na pengine hata kutunukiwa nishani na taifa lake maana aliyoyafanya hata nje ya Panel hii ni makubwa. Tulibidi sisi kama taifa tumuenzi badala ya kujificha nyuma ya hii zawadi. Bila sisi kumvisha hiki kilemba cha ukoka, Profesa Yanda anaweza kutembea kifua mbele kwa yale aliyoishayafanya. Ndio maana nikaweka CV yake humu kuthibitisha hilo.
 
Fundi Mchundo,

Ukweli uko katikakti, prof. ni mmoja wa panel la wasomi wazuri wa dunia walioandika hiyo report. Kwa maana hiyo inatakiwa apongezwe kwa kazi kubwa waliyofanya mpaka kuifanya IIPC washinde hiyo zawadi.

So, sio kweli kwamba yeye binafsi ameshinda Nobel Peace Prize? Je, unakubali kwamba kuna tofauti kati ya ushindi wa an individual na panel? Otherwise, of course, tunampongeza kwa kuwa one of the authors of such a great report. But I think apewe sifa zinazostahiki na sio zisizostahiki!
 
Kitila,
Tofauti hiyo iko wazi na inatosha kutumia dakika kama kumi ku search kwenye google na kupata ukweli wote. Mimi ni mfuatiliaji wa washindi wa Nobel prize toka miaka ya 80 nikiwa secondary school, kwahiyo najua vizuri tofauti ya ushindi wa Gore na ushindi wa prof. wetu.

Ila pia naona ni mafanikio kwa reports ambazo prof wetu alishiriki kuzitayarisha kushinda hiyo nobel prize. Naamini hilo ni fanikio na ilitakiwa waandishi wetu kuitangaza hiyo habari na hata kumhoji ili aweze kutoa utaalamu wake kwenye mambo ya climate change.

Kuhusu CV yake, kama anataka inatakiwa aandike kwamba alikuwa mshiriki kwenye kuandika report juu ya climate change ambayo ilishinda noble prize. Watu kibao wameweka kwenye CV kushiriki kwao kwenye vikamati vya ajabu ajabu ndio iwe huyu prof?

Watu toeni CV zenu tuone mmeandika mafanikio gani (kwi kwi kwi!!!). Utafikiri kule bungeni ambako watu wanaweka hata seminars za siku moja moja kama wamepata certificates. Kama ni hivyo nafikiri kuna watu wanaweza kuwa na certificates hata 1000.
 
Back
Top Bottom