Waliotunukiwa zawadi ya Nobel Peace Prize ya mwaka 2007 ni Al Gore na IPCC. IPCC ilitunikiwa kwa kazi ilizozifanya tangu ilipoanzishwa mwaka 1988. IPCC imekuwa likitoa ripoti kuhusu climate change uhai wake wote. Profesa Pius Yanda ni mmoja ( wako wengi sana) wa contributors katika Working Group II ( ziko WG tatu) Fourth Assessment report. Humo katika WG kuna reviewers wengi tuu ambao nao wanachangia katika hii ripoti. Unaweza kuona majina yao hapa:
http://www.ipcc.ch/pdf/assessment-report/ar4/wg2/ar4-wg2-app.pdf
Mkuu wa IPCC ni Bw. Rajendra Cheuri kutoka India ambaye ni kiongozi wa tatu kuongoza Panel hii. Wote hawa kwa namna moja au nyingine wamechangia katika mafanikio ya IPCC lakini hatuwezi kuwaita 'joint recipients' wa Nobel Peace Prize.
Profesa Yanda anastahili kuheshimiwa na pengine hata kutunukiwa nishani na taifa lake maana aliyoyafanya hata nje ya Panel hii ni makubwa. Tulibidi sisi kama taifa tumuenzi badala ya kujificha nyuma ya hii zawadi. Bila sisi kumvisha hiki kilemba cha ukoka, Profesa Yanda anaweza kutembea kifua mbele kwa yale aliyoishayafanya. Ndio maana nikaweka CV yake humu kuthibitisha hilo.
Fundi Mchundo,
Hilo la kwamba yeye hajashinda hiyo noble prize linajulikana, tatizo kwa watu wengine hapa ni hiyo kujaribu ku negate umuhimu wake kwenye hiyo IPCC kushiinda hiyo prize.
Taifa litamtunikia vipi kama hakuna publicity yoyote anayopata hata anapofanya jambo la maana au kupata fanikio kama alilopata kwa kushiriki kwenye kuandaa reports ambazo zimeifanya IPCC ishinde prize?
Vyombo vya habari havikutakiwa kumtangaza prof. kama mshindi wa nobel peace prize lakini pia vilitakiwa kuongelea contribution yake kwenye hizo reports.