Prof Nhonoli afariki - kimya! Wasomi hawathaminiwi

huu uzi uko jukwaa ambalo si mahala pake. Hii habari ipelekwe jukwaa la jf doctor maana marehemu hakuwa mwanasiasa

Haipo kwenye siasa, ipo kwenye hoja na habari mbalimbali
 
RIP Prof. jamani namuunga mkono Bijou, kama huna data fulani tafuta kwanza kabla ya ku-comment na kama inabidi anyway.
 
Daktari bingwa na nguli katika tasnia ya afya amefariki na kuzikwa Arusha, ni katika madaktari wa mwanzo baada ya uhuru, na alifundisha madaktari wengi nchini. Pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Afrika Mashariki na kusini kwa muda mrefu sana kabla ya kustaafu.

Alikuwa mkuu wa kwanza Mtanzania wa kitivo cha udaktari, mkurugenzi mkuu wa kwanza wa hospitali ya Muhimbili, Rais wa kwanza wa MAT etc etc ( ongeza unavyovijua)

Tanzania tuwajali na kuwaenzi wasomi wetu, R.I.P Professor

Upumzike kwa amani mwana mwema wa Tanganyika!
 
Kwa kweli hata mimi..Kwani hawana Umoja wa Madaktari bigwa?may be ingesaidia ktk kumtangaza.
R.I.P PROF

Inashangaza Maana hata M.A.T kimya! KWA Rais WAO wa kwanza wa Chama chao cha Madaktari
 
Daktari bingwa na nguli katika tasnia ya afya amefariki na kuzikwa Arusha, ni katika madaktari wa mwanzo baada ya uhuru, na alifundisha madaktari wengi nchini. Pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Afrika Mashariki na kusini kwa muda mrefu sana kabla ya kustaafu.

Alikuwa mkuu wa kwanza Mtanzania wa kitivo cha udaktari, mkurugenzi mkuu wa kwanza wa hospitali ya Muhimbili, Rais wa kwanza wa MAT etc etc ( ongeza unavyovijua)

Tanzania tuwajali na kuwaenzi wasomi wetu, R.I.P Professor

RIP Prof Nhonoli............

Prof alikuwa ni "mtu wa kawaida".........Mabina, Ditopile......"hawakuwa watu wa kawaida"......
 
Tanzania ina maprofesser wengi sana ukitaka anaefariki taifa limmshikie bango je tutawashikia wangapi?
Mungu amuweke anapostahili.
 
Pro. Makene
pro. Mwaluko
Pro.Salungi
Pro.Karashani
Pro.Kimati
Pro. Shaba
Pro.Masawe
Wote hawa ni Rank moja
 
Pro. Makene
pro. Mwaluko
Pro.Salungi
Pro.Karashani
Pro.Kimati
Pro. Shaba
Pro.Masawe
Wote hawa ni Rank moja

Hao uliowataja hawakuwahi kuwa dean wa kwanza mtanzania, rais wa kwanza wa MAT, mkurugenzi mkuu wa kwanza wa muhimbili etc etc
 
Pia ndie mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya wakurugenzi ya National institute of Medical research
 
Back
Top Bottom