Dkt. Philip Mpango: Jitihada zinahitajika kutoa elimu ya magonjwa yasioambukiza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Bohari ya Dawa (MSD) imeshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuwakutanisha Madaktari Bingwa, wataalam na wadau wa afya, wauguzi na watunga sera kutoka mataifa zaidi ya 40 Duniani kwa lengo la kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali yanayohusu magonjwa ya moyo Duniani, Februari 9, 2024.

Akifungua Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Airport – Unguja, Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema jitihada zinahitajika katika kutoa elimu ya magonjwa yasioambukiza pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha, mazoezi na kufanya vipimo vya afya mara kwa mara ili kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo.
IMG_20240210_134553_921.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai akipokea Tuzo Maalum kutoka Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, iliyotolewa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kutambua mchango wa MSD katika kuhakikisha bidhaa za afya zinazohusisha na huduma, dawa na vipimo vya magonjwa ya moyo, zinapatikana nchini.


Amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa moyo ni muhimu wananchi kufuata njia za kujikinga zaidi ikiwemo kuacha ulevi uliyopindukia, uvutaji sigara, tabia bwete pamoja na uzito uliyopindukia. Ametoa rai kwa watalaamu wa afya, wasomi, vyombo vya habari pamoja na watunga sera kushiriki katika utoaji elimu kuhusu masuala ya afya.
IMG-20240210-WA0007.jpg

IMG-20240210-WA0008.jpg

IMG-20240210-WA0010.jpg
Aidha, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa tafiti zinapaswa kufanyika kwa kina ili kubaini visababishi zaidi vya magonjwa ya moyo kwa kupata taarifa zaidi juu ya taratibu za kijamii na tabia za kiutamaduni katika mambo mbalimbali yaliyozoeleka kufanyika barani Afrika.

Mbàli na kushiriki mkutano huo, MSD imepokea tuzo maalum kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kufutia mchango wake katika kuhakikisha bidhaa za afya zinazohusisha na dawa na vipimo vya magonjwa ya moyo, zinapatikana nchini.
 
Back
Top Bottom