Prof Nhonoli afariki - kimya! Wasomi hawathaminiwi

Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,192
1,500
Daktari bingwa na nguli katika tasnia ya afya amefariki na kuzikwa Arusha, ni katika madaktari wa mwanzo baada ya uhuru, na alifundisha madaktari wengi nchini. Pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Afrika Mashariki na kusini kwa muda mrefu sana kabla ya kustaafu.

Alikuwa mkuu wa kwanza Mtanzania wa kitivo cha udaktari, mkurugenzi mkuu wa kwanza wa hospitali ya Muhimbili, Rais wa kwanza wa MAT etc etc ( ongeza unavyovijua)

Tanzania tuwajali na kuwaenzi wasomi wetu, R.I.P Professor
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
Wasomi wanajiharibia wenyewe hii nchi inashindwa kupiga hatua kwasababu yao,wao wanadhani kuwa PhD holder ndo baasi na wakati wanatakiwa kudevote muda wao kutoa elimu huko vijijini kama huyu Prof alitakiwa akasaidie watu kujua nini mabaya ya sera za afya kwa wazee,vijana n.k na nini watu wafanye ila tatizo lao wakishapata hizo titles wanahamia Obey na kusahau haraiki ya wanyonge wa nchi hii

R.I.P Prof.
 

Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,192
1,500
Hatumuheshim na kumuenzi mtu kwa elimu alionayo au position alionayo bali ni nini amefanya kwa taifa cha kukumbukwa kupitia elimu aliyonayo au position aliokuwa nayo.
RIP Dr.

Soma maelezo yangu utaona mchango wake kwa taifa ni nini
 

Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,192
1,500
Wasomi wanajiharibia wenyewe hii nchi inashindwa kupiga hatua kwasababu yao,wao wanadhani kuwa PhD holder ndo baasi na wakati wanatakiwa kudevote muda wao kutoa elimu huko vijijini kama huyu Prof alitakiwa akasaidie watu kujua nini mabaya ya sera za afya kwa wazee,vijana n.k na nini watu wafanye ila tatizo lao wakishapata hizo titles wanahamia Obey na kusahau haraiki ya wanyonge wa nchi hii

R.I.P Prof.

Huyu alisoma makerere na uk, ulimbukeni uliokuwepo kwa wasomi wa wakati ule, kama angeamua angebaki ughaibuni. Lakini alirudi kuja kuwatumikia watanzania. Amefundisha madaktari wengi hapa Tanzania, na hakuwa oysterbay, baada ya kutoka muhimbili alihamia arusha na ndiko alikofia na kuzikwa
 

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
Hivi yule bingwa wa upasuaji wa moyo ilikuwaje akafilisiwaaa?
out of context
 

MissM4C

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,341
2,000
Tatizo hawa maprof wetu haawachagi hata documenyaries ama vitabu tungekuwa tunawatambua na tunawaenz kuptia maandko yao, sasa mi ukurugenz wake mhimbl ungenisaidia nini??? Wasomi wa tz badilikeni andiken kwa faida ya vizaz vijavyo, mi ndo namsikia hapa, anyway wacha niende wikipedia,

apepe!!
 

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,053
2,000
Rest In Peace Prof. Nhonoli! Mungu Awape faraja wanafamilia na wote walioguswa.
 

DAWA YA SIKIO

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
979
195
daktari bingwa na nguli katika tasnia ya afya amefariki na kuzikwa arusha, ni katika madaktari wa mwanzo baada ya uhuru, na alifundisha madaktari wengi nchini. Pia alikuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi ya afya ya afrika mashariki na kusini kwa muda mrefu sana kabla ya kustaafu.

Alikuwa mkuu wa kwanza mtanzania wa kitivo cha udaktari, mkurugenzi mkuu wa kwanza wa hospitali ya muhimbili, rais wa kwanza wa mat etc etc ( ongeza unavyovijua)

tanzania tuwajali na kuwaenzi wasomi wetu, r.i.p professor

r.i.p Prof Nhonoli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom