BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Pia soma > Tanga: Mjamzito afariki kwa kukosa Tsh. 150,000
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Waziri Kindamba ametuma Timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha Madaktari bingwa wawili - Daktari Bingwa wa Wanawake na Uzazi na Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi - ili kufanya uchunguzi wa tukio hili.
Pili, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tayari amewasimamisha kazi watumishi watatu (3) walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hili baya na lisilopaswa kuvumiliwa!
Tatu, Tuhuma hizi pia tayari zimeshapokelewa na Mabaraza ya kitaaluma (Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC)) na vyombo vingine vya dola kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hivyo, ninaelekeza Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) ndani ya Siku 7 kuanzia leo kuniletea Taarifa ya Uchunguzi wa tukio hili na mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Nne, nataka niwahakikishie umma wa watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya Uchunguzi, kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua kali za kitaaluma, kiutumishi na kijinai ikiwemo kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika hivyo.
Nichukue fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya kote nchini wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Nawapa pole familia iliyoguswa na msiba huu na niahidi kuwa serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya ili kufikia matarajio ya wananchi.