Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 15,859
- 20,714
UTARATIBU WA KIKATIBA RAIS ANAPOUGUA KIMWILI AU AKILI
Wakili Mwita ameandika maoni yake juu ya Kifo cha Hayati John Magufuli baada ya kauli ya CDF Mstaafu Mabeyo siku ya kuadhimisha miaka mitatu ya Rais Samia.
"Kikatiba, rais wa nchi anapougua na kushindwa kabisa kutekeleza majukumu yake, Baraza la Mawaziri linapaswa kupewa taarifa. #Fact 1
Baraza la Mawaziri limepewa uwezo Kikatiba chini ya Ibara 37 kupeleka AZIMIO kwa Jaji Mkuu ili aunde jopo la madaktari wasiopungua 3 wanaotambulika na sheria ya matabibu nchini ili kuchunguza afya ya rais ya AKILI au/na MWILI. Ripoti ya madaktari ikitoka, ikithibitisha rais ni mgonjwa na hawezi tekeleza majukumu kabisa & hakuna dalili ya yeye kupona, ripoti hiyo hupelekwa kwa Jaji Mkuu ambaye hutakiwa kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge kama AZIMIO la kumwondoa rais madarakani.
Jaji Mkuu asipofuta AZIMIO hilo ndani ya SIKU SABA, rais anahesabika amepoteza madaraka yake. Sheria inaelekeza taarifa za rais kuugua zipelekwe Bungeni kwa sababu rais ni mtumishi wa Umma & taarifa za kuugua kwake hazitakiwi kuwa siri. #Fact 2
Endapo ripoti itathibitisha kuwa rais ni mgonjwa na ameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake, sharti ya Kikatiba ni kwamba Makamu wa rais anatakiwa kuapishwa na kushika madaraka ya urais haraka iwezekanavyo & kumalizia kipindi kilichobaki kabla ya uchaguzi unaofuata. #Fact 3
Hivyo, kwa msimamo huu wa Kikatiba, Baraza la Mawaziri lilitakiwa kuwa na taarifa ya afya ya rais pale tu JPM alipoanza kuugua na kushindwa kutekeleza majukumu yake, hii ni kabla ya kuwa MAHUTUTI. Samia alitakiwa kuapishwa KABLA hata JPM hajafariki!
Pia, kutokana na alichokisema CDF mstaafu Mabeyo, ni wazi kwamba kuna kikundi cha watu KIMEVUNJA Katiba ya nchi kwa kutofuata taratibu zilizotajwa pale ambapo rais anaugua, taratibu ambazo zimewekwa ili kuepuka mambo ya UHAINI.
MASWALI
1. Kwanini utaratibu wa Kikatiba uvunjwe na hawa wavunja Katiba wako wapi na wanachukuliwa hatua gani & kuna uhakika gani hili halitajirudia?
Katika hili pia nakumbushia tu kumficha mtu mhaini ni kosa kubwa kisheria.
2. CDF Mabeyo ametuambia wakati rais JPM anafariki, akiwa MAHUTUTI sana, mbele yake alikuwa yeye (CDF), Mkurugenzi Mkuu TISS & IGP. Hawa ni wakuu wa vyombo vya ulinzi & usalama tu, ilikuwaje hakukuwa na kiongozi yeyote wa Kiserikali toka Baraza la Mawaziri akiwemo VP, PM au Waziri wa Afya?
3. Mnafahamu nguvu ya kisheria ya mwenza (mke) wa mgonjwa? Kwahiyo Mama Janet hakuwepo au mwanafamilia yeyote wakati mpendwa wao anaaga duniani?
4. Inakuwaje rais wa nchi ni mgonjwa halafu makamu wa rais afanye ziara Mkoa mwingine wa mbali huku rais yuko MAHUTUTI (fighting for his life), na ndiyo siku ambayo alifariki? Hiyo ziara ilikuwa na ulazima gani?
5. Kwanini Waziri Mkuu auambie umma kuwa rais ni mzima wakati alikuwa MAHUTUTI?
Ningepata nafasi ya kumfanyia CROSS-EXAMINATION mstaafu CDF ningeitumia taaluma yangu vyema. NINA MASWALI 50, HAYO NI YA UTANGULIZI TU" Wakili Mwita.
Mwanzo TV Plus