Prof. Mussa Assad: Katiba Mpya ni Muhumu, itamjenga Rais na haitampunguzia chochote

Profesa Assad akihojiwa, amesema kuwa katiba mpya ni jambo la muhimu sana
Akasema somo tulilolipata katika utawala uliopita limetuonyesha umuhimu wa kuwa na katiba nzuri.

Profesa Assad amemuambia rais Samia kuwa, yeye kuleta katiba mpya hakutampunguzua chochote bali kutamuongezea credit

MY TAKE:
Samia asiipoteze nafasi hii adhimu ya kuwa kiongozi aliyefanya reforms za msingi za kisiasa na kiutawala katika nchi hii.
Samia afahamu tu kuwa Uchumi uko linked na nasuala ya utawala bora na siasa nzuri, haki katika nchi na mifumo bora na Imara. Msingi wa huvyo vyote ni Katiba bora.

Samia kama anadhani anataka kujenga uchumi chini ya katiba hii, badi atambue tu ni rahisi kweli kwa mtu ajaye kubomoabomoa uchumi alioujenga kwa sababu katiba hii i ampa haki ya kufanya hivyo bila consequences zozote.

 
Hakika, kama Rais Samia ana nia njema kwa Taifa hili, anatakiwa kushughulika na jambo la msingi kwa Taifa letu kuliko kuhangaika na matokeo.

Samia, shughulikia mchakato wa katiba.

Kama Rais atauweka mchakato wa katiba pembeni, yote anayoyafanya yatakuwa ni usanii tupu, ina maana atakuwa hana dhamira ya kutatua matatizo ya msingi yanayolikabili Taifa letu.
 
Back
Top Bottom