Ndugu zangu kama kwaida huwasikurupuki kuchangia mada humu nafanya utafiti kwanza. Kwa hili mtoa hojaameshindwa kuthibitishia umma ukweli wa swala hili, naungana na Satellitekuomba source ya aliyoaandika. Labda mimi niweke wazi unafiki wa mtoa mada nakuueleza umma kuwa mtoa mada is not matured interms of reasoning and factsearching bali ni mchochezi yeye pamoja na wanaowahamasisha wanafunzi wastrikebila kuwaeleza uwazi wa jambo lenyewe. Ingawa mimi siyo msemaji wa USDM wala waserikali ila tu mdau wa chuo kile kwa utafiti wangu napenda kujibu hoja kamaifuatavyo ili mwenye akili atafakari na mwenye kutafiti apinge majibu kwautafitina bila unafiki.
1. Kwenda Iringa: Ni kweli Prof. Mukandala na Msaidizi wake walienda Iringa
2. Kutembelea MUCE: Ukweli ni kwamba Prof. Mukandala alikwenda MUCE kuhudhuriamkutano wa 21 wa Governing Board Na sio just kutembelea chuo.
3.Hoja ya kukodi ndege: Ndege haijakodishwa ila Ukweli ni kwamba Prof.Mukandala na msaidizi wake walikwenda iringa kwa ndege ya shirika la ndegelinalojulikama kama Auric Air inayofanya safari zake kwenda Iringa na Mbeyakila siku kwenda asubuhi kurudi mchana. Kupata ukweli wa hili wasiliana naAuric Air kwa namba zifuatazo 0783233334.
4. Kukodi Ndege kwa Million nne (4): Hivi ni nani atakubali kutoa ndege yakekutoka Dar kwenda Iringa kwa milion 4? tuache uongo Kwenda Iringa kwa kukodindege nulizia Tanzaniair watakupa gharama ambazo ni minimum costs. Garamahalisi walizotumia kwenda Iringa kwa wote waeili wanazo Auric Air na unawezakupitia website yao. Nimefanikiwa kupata invoice na receipt ya malipoyaliyolipwa mkitaka kujua amount mseme nitawapatia.
5. Magari V8 kutangulia bila mtu: Acheni uongo wajameni muangalie tu UDSM wanaV8 ngapi? Kampuni yetu ndiyo inatengeneza magari yao ila fanyeni utafiti.Mukandala mwenyewe anatumia VX la kizamani. Hapa nipo Iringa na wakati Raisanasuburiwa kuingia Prof. Mukandala ndiyo alikua anaondoka na nimeona ameletwa naNissan ya Prof. Mushi wa MUCE sasa sijui hayo ma VX mawili yalienda kufanyanini huko? Tafakari
6. Kuhusu Ukwasi: Hapa siwezi sema mengi ila najua UDSM wanategemea pesa toaserikalini mtumeni CAG akafanye kazi yake kama ukwasi unatokana na matumizi mabovuau la.
7. Matumizi mabaya ya fiedha: Mi ninavyomjua huyu bwana anajaribu sanakupunguza matumizi na nikipiga mahesabu ya kwenda Iringa kwa gari yaani: Muda,mafuta, tahadhari, na posho za wote na siku watakazo kuwa huko utagundua ni kwakiasi gani huyu bwana alivyoliona hilo na kushukuru kampuni ya Auric kupelekausafiri wa ndiege Iringa. Tafakari!
8. Mliman City wanakula: ukweli ni kwamba mwekezaji lazima anataka kula lakiniMradi huu hakuuanza Mukandala ujue, pia tangu ameingia madarakani lazima tufanyeutafiti kujua chuo hicho kinafaidikaje na mradi huo. Nilikutana na moja wawakurugenzi wa pale nilopokwenda Botswana last week wakasema VC wa sasa paleUDSM anawabana sana.
9. Chuo Kimeharibika: Ukweli ni kwamba anayejenga na kubomoa chuo ni wewe, mimina waliopo chuoni pale; wewe unaambia wanafunzi waandamane kupinga kituulichotunga kisicho na ukweli, unwatakia mema wanafunzi na chuo kwa ujumla?watasoma saa ngapi? watatafiti pumba na makande saa ngapi kama mnawajazaemotional greefs.
Wandugu nitaendelea kusema ukweli hata kwa kifo uongo, majungu na fitina kwangumwiko. Tuache makelele, tuongee; tuache siasa za chuki tujenge hoja tuibuemijadala ya kifikra na kimaendeleo; tuache uvivu wa kufikiri na kutenda,tufanye kazi kwa bidii.