DOKEZO Prof. Esther William Dungumaro na Ubadhirifu wa Fedha MUCE

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,928
5,616
DNG.png

Profesa Esther William Dungumaro ni Mkuu (Principal) wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE). Kwa namna anavyoendesha chuo hiki cha umma, inaleta mashaka juu ya uadilifu wa uongozi wake katika masuala ya fedha. Taasisi za umma zinaendeshwa kwa mpango kazi wa kila mwaka na bajeti ya kila kazi inayopangwa kufanyika ktk mwaka husika.

Kwanini chuo kinashindwa kuwalipa wafanyakazi na watoa huduma wengine kwa zaid ya miez 6, kwa shughuli ambazo ni za msingi kwa taasisi? Unaendeshaje taasisi bila kutenga pesa kwa ajili ya shughuli za msingi za taasisi? Mbona pesa ya kuwakirimu viongozi wa kisiasa wanaokuja Iringa kwa ajili ya masuala yao binafsi anatoa kuanzia pesa mpaka magari?

Hakuna nia ovu katika kuweka wazi jambo hili. Kwakuwa linaathiri taswira ya taasisi ya umma na kushusha morali ya kazi, nashauri viongozi wafuatao wafanye uchunguzi wao kujiridhisha juu ya tuhuma hizi na kuchukua hatua:
  • Makamu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam: Prof. William Anangisye kwa sababu jambo hili linaathiri taswira ya chuo kizima cha UDSM na vyuo vyake vishiriki.
  • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia: Prof. Adolf Mkenda kwa sababu jambo hili linaathiri ufanisi wa huduma za ufundishaji, utafiti na ushauri kwa jamii.
  • Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kuna ishara za matumizi mabaya ya fedha au matumizi nje ya bajeti inayokuwa imepitishwa. Itakuwa vyema kama CAG atajiridhisha kama pesa ya umma inaenda ktk maeneo yenye tija.
 
Back
Top Bottom