Prof. Mohamed Janabi achaguliwa kuongoza WHO AFRO
VOTING RESULTS:
1. 🇹🇿 Prof Yakub Janabi: 32
2. 🇨🇮 Dr N’da Konan Yao: 5
3. 🇬🇳 Mohamed Drame: 4
4. 🇹🇬 Prof Moustafa Mijiyawa: 4
Prof: Janabi kaongea vizuri sana ni umbumbu wa watanzania hawapendi maendeleo ya wengine
Ukweli WATANZANIA tuna udhaifu mkubwa sana wakutopenda vya kwetu
Hata mtu akifanya vizuri huko Ulaya badala ya watu wajuvunie sisi tunatafuta vya kumkosoa
Wenzetu wanajivunia watu wao wanao watoa kimasomaso kama Icon ya Nchi sisi kutwa kucha kuwachafua!
Ukitakua kahakikisha hilo; Mtafute Mbwana Samata; Hasheem Thabit nk mtu anaogopa hata kusema ametoka Tz kwa sababu ya upuuzi wa comment kutoka TZ
 
Nami natamani kujua, kama nchi kuna faida gani inapatikana kuwa na kiongozi ngazi hiyo huko WHO? Maana nakumbuka Migiro alikuwa UN, Salim Ahmed nae AU ila sidhani kama kuna tija yoyote kwa taifa.
WHO is a specialized and autonomous UN Agency not working under the office of the Secretary General of UN, Security Council or UNGA.

It means it is UN countries' club with a mandate of supervising all health issues. This includes soliciting funds, sharing technical experience, formulating policies & health standards and providing emergency relief in terms of crises.

In other words, if utilized well this position could offer massive Diplomatic Clout and Funds for TZ.

But since we hate MAMA and CCM, these initiatives must be seen as Mundane and a Corruption Extravaganza, which it kinda is 😂😂😂.

SHEKELI MINGI imetumika hapa​
 
Ngoja tukafukue uzi za wale wapumbavu wa chadema waliokuwa wanamuombea mabaya 😂
 
Mwamba ni mtu wa zari sanaaa naweza sema hivo NI MTU ANAYE AMINIKA SANAA((system ya nchi)) akipewa kazi mara chache ana fely nyingi ana faulu TUNA MA DR WENG MA PROF WENG wana mzidi hata elimu ILA MASWALA YA KIMKAKATI KIUTENDAJI MAAMUZI YALIO HARAKA YENYE UTULIVI WA HALI YA JUU prof janabi yupo vizuri pale WHO hatuja mpeleka kwa hasara nchi kama nchi TUTAFAIDI MENGI mshikaji wake sanaaa na ame msaidia sanaaa hongera nyingi JAKAYA MRISHO
 
Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika kutoka Tanzania, Prof. Mohammed Janabi, ametaja vipaumbele saba ambavyo amevinadi mbele ya Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani katika Bara la Afrika na kuomba ridhaa ya kumpitisha kushika nafasi hiyo.

Prof. Janabi amewasilisha vipaumbele hivyo leo May 18, 2025 alipokuwa akijinadi mbele ya Mawaziri hao na kuahidi kuwa endapo atachaguliwa atasimamia uboreshaji wa huduma za afya na kuweka mkazo zaidi kwenye uboreshaji wa huduma za afya ngazi ya msingi “Endapo nitachaguliwa naahidi kusimamia uboreshaji wa huduma za afya kwa wote ili kuweza kufikia malengo endelevu, hadi sasa ni 46% pekee wanapata huduma bora za afya Afrika huku lengo la kidunia ni kufikia 68% mwaka 2030, pili nitasimamia upatikanaji wa rasilimali fedha za kuwezesha kugharamia upatikanaji wa huduma bora za afya”

Kipaumbele cha tatu amekiainisha kuwa ni kuendelea kusimamia utayari wa nchi wanachama katika kukabiliana na majanga pamoja na dharura za afya na amesisitiza pia kuhusu kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa Mama na Mtoto pamoja na lishe akisema Afrika inachangia 70% ya vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na 56% ya vifo vya watoto wachanga duniani.

Kipaumbele cha tano amesema ataendelea kuweka msisitizo zaidi kwenye kupambana na magonjwa ambukizi yakiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria, Magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa yasiyopewa kipaumbele akiswma yanachangia katika kuzorotesha uchumi wa Bara la Afrika, kipaumbele cha sita amesema atasimamia jitihada za kupambana na changamoto ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa UVIDA.

Prof. Janabi amehitimsha na kipaumbele cha saba kwa kubainisha kuwa ataimarisha uzalishaji wa bidhaa za afya zikiwemo dawa, vifaa na vifaatiba pamoja na chanjo ndani ya Bara la Afrika.
#MillardAyoUPDATES
 

Attachments

  • IMG-20250518-WA0564.jpg
    IMG-20250518-WA0564.jpg
    91.8 KB · Views: 19
  • 20250518_180458.jpg
    20250518_180458.jpg
    253.5 KB · Views: 20
Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.

Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.

Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:

  • Moustafa Mijiyawa (Togo)
  • Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

View attachment 3338251
Hongera kwake
 
Back
Top Bottom