Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 69,521
- 122,900
Profesa Kabudi ni namba ingine kwenye kitivo cha ufaulu wake WA digrii ya sheria chuo kikuu cha dar es salaam rekodi yake ya ufaulu haijawahi vunjwa na yeyote toka Tanzania ipate uhuru hadi leo kwa yeyote anayesoma digrii ya sheria. Mwanae pia aliweka rekodi ya ufaulu chuo kikuu cha ardhi ambayo haijawahi vunjwa tokea Tanzania ipate uhuru na haijavunjwa hadi Leo. Huyo huwezi mshindanisha na wapiga yowe na makelele Kama akina Lisu, mbowe, akina lema na Sugu the music rapper.Mwingine mwenye akili kupindukia ni profesa Lipumba alivunja rekodi ya ufaulu kwenye digrii ya uchumi chuo kikuu cha dar es salaam ambayo toka uhuru hadi sasa Hakuna mtanzania aliyevunja rekodi ya Lipumba
Sifa za kipuuzi, hao uliwataja kuwa ni wasomi ni kipi wamefanya cha maana katika nchi hii? Mwingine sio ndio huyo ameamua kugombania uenyekiti alioukataa na sasa anaendesha genge la mauaji huku akishirikiana na serekali? Kumbuka mtu kama Lipumba ndio walioandika proposal jinsi ya kubinafsisha viwanda leo hii vijana wanazunguka na chupi na soks tatu mkononi eti ni wamachinga. Nilitaraji ungetuonyesha kwa ufaulu wao wamefungua miradi gani ya uzalishaji mali iliyowapa ajira watanzania katika kupambana na umaskini. Sio unatuandikia eti ni wasomi waliovunja rekodi wakati wanashinda kwa waganga wa kienyeji wasikose ajira kwenye taasisi mbalimbali.
